Monday 29 February 2016

ZIJUE FAIDA ZA KUTUMIA TANGAWIZI


Tangawizi ni moja kati ya mizizi ambao ina faida kubwa sana katika miili yetu.Tunashauriwa kutumia tangawizi kwa wingi ili kuweza kuzipata faida hizo.Zifuatazo ni baadhi ya faida za tangawizi mwilini

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA: Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea) . Hali hii ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya ujauzito,kupata harufu mbaya n.k.Kunywa chai ya tangawizi kwa wingi.

HUSAIDIA UFANYAJI MZURI WA KAZI
Hii ni pamoja na kusaidia uyeyushaji mzuri wa chakula na pia husaidia ufyonzaji wa chakula na virutubisho vyake.

INASAIDIA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI
Ili kuimarisha uzungukaji wa damu mwilini kwa njia ya asili,unashauriwa kutumia kikombe kimoja au zaidi cha tangawizi kila siku.Ni njia inayoaminiwa ya kutumika nyumbani kusaidia matatizo ya mzunguko wa damu mwilini.

INASAIDIA KUTIBU HOMA.
Agenda rahisi hapa ni kuwa tangawizi inasaidia kuleta ujotoridi ambao unasaidia kupambana na matatizo ya kutokwa sana na jasho.Hii inasaidia kulirudisha joto la mwili katika hali ya asili na kutibu homa.

HUSAIDIA MATIBABU YA ATHMA.
Hii inawezekana kwa mapafu kutanuliwa kwa kupunguza 'phlegm' kwa kunywa tangawizi.Hii inasaidia matatizo ya upumuaji mwilini.Pia hupunguza tatizo la mzio kwa watu wa athma.

HULETA MTULIZO WA AKILI
Faida nyingine ya kuwa tangawizi ni kuondoa MSONGO mwilini.kikombe cha tangawizi kinatakiwa kukuongeza nguvu na mtulizo wa akili kuondokana na msongo.

HUIMARISHA MFUMO WA UZAZI
Unywaji wa tangawizi husaidia kuimarisha mbegu za uzazi za kina Baba na pia kuongeza uwezo wa kuzarisha.Pia husaidia uume kusimama vema kwa kina Baba.

HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO
Hii husababishwa na uwezo wa tangawizi kuunguza na kuyeyusha mafuta mwilini.Husaidia mwili kuwa na uzito sawa na pia kupunguza kiasi cha karoli mwilini.Hii ni faida kubwa sana kulingana matatizo yaliyokithiri ya uzito uliopitiliza.

HUSAIDIA MFUMO WA UPUMUAJI MWILINI
Tangawizi ina faidi nyingi sana.Inasaidia sana matatizo katika mfumo wa upumuaji.Kikombe kimoja tu kinaweza kutatua matatizo mengi sana ya mfumo wa upumuaji.Pia husaidia matatizo ya upumuaji yanayotokana na mazingira.

HUSAIDIA KUIMARISHA KINGA YA MWILI
Husiaidia sana kuimarisha mfumo wa asili wa kinga ya mwili.Hii hupelekea mwili kuwa na uwezo mkubwa sana wa kupambana na magojwa vamizi mwilini.

HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI.
Unywaji wa tangawizi husaidia sana kupunguza maumivu wakati wa hedhi.Kama mtu ana matatizo ya hedhi hakikisha anapata walau vikombe viwili vya tangawizi kila siku.
Pia chukua taulo kisha loweka kwenye tangawizi moto na kumkanda chini ya kitovu na kuzunguka tumboni mgonjwa mwenye matatizo ya hedhi.
HUSAIDIA KUPAMBANA NA KANSA
Tangawizi husaidia kupambana na pia kutibu kansa.Husaidia kuzuia kuenea kwa kansa mwilini kwa kiwango kikubwa kuliko madawa ya kisasa.

HUSAIDIA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wengi wametumia tangawizi na kuondokana na harufu mbaya mdomoni nabkufanikiwa.

HULINDA INI
Tangawizi husaidia kuondoa sumu mwilini na hivyo kulisaidia ini  na kulifanya lipunguziwe mzigo na hivyo kuendelea kuwa na afya njema.

HUSAIDIA TUMBO
Hulisaidia tumbo kuwa lenye afya siku zote na kufanya vema kazi zake.

Na Michael Gussa kwa msaada wa mitandao

Friday 26 February 2016

WATU ISHIRINI WANAOSHANGAZA ZAIDI DUNIANI


Kila mtu ana kitu maalumu ambacho kinaweza kumtofautisha na wengine.Kitu hicho hutofautiana kati ya mtu na mtu.Lakini kuna wengine wana vitu vya ziada ambavyo huwafanya kuwa wa pekee zaidi duniani.Hawa ni baadhi ya watu hao:

MTU MWENYE MDOMO MKUBWA ZAIDI
Francisco Domingo Joaquim ni mtu mwenye kipaji cha kipekee.Yeye anashikilia rekodi ya kuwa na mdomo mkubwa zaidi duniani.Mdomo wake una ukubwa wa '6.69inches' kiasi kwamba ana uwezo wa kumeza soda ya kopo.

MVUMBUZI MAARUFU(DOKTA NAKAMATS)
Raia wa japan Yoshiro Nakamatsu alijulikana kwa kuwa mtu mwenye akili na mvumbuzi hodari zaidi.Huyu anashikilia rekodi ya kuvumbua vitu vingi zaidi.Pia ana sifa ya kupiga picha mlo wake na kuulezea kwa muda wa miaka 40.

MTU ANAEKULA VYUMA
Kwa muda wa miaka 40 raia huyu wa ufaransa Michel Lotito amekula zaidi ya tani 9 za maada(metal)ikiwemo chuma.Akiwa mdogo aliugua ugonjwa wa ukosefu madini mwilini na akaanza kula plastiki.Baadae alianza kula vitu vigumu kama vioo na baadae vyuma.

MWALIMU MZEE WA YOGA.
Mwanamke huyu mwenye miaka 96 Tao Porchon Lynch amekuwa akijifunza mchezo huu zaidi ya miaka 70 sasa.Huwa anaamka alfajiri na kuwafundisha watoto jinsi ya kujinyoosha mwili,kujipiga na mapozi mengine magumu ya mchezo huu wa Yoga.

MALKIA WA CHUMA
Asha Rani amejitambulisha kwa kuwa na rekodi mbili za kushangaza kwa kunyanyua mizigo mizito kwa kutumia nywele zake pamoja na maskio yake.Akiwa na miaka 23 amepewa jina la 'Iron Queen' kutokana nabuwezo na nguvu zake.

RUBANI MZEE ZAIDI
Kutokana na rekodi za Guinness za dunia,Peter Weber Jr. ndie rubani aliekuwa mzee zaidi wakati akiwa kazini.Akiwa na miaka 95 yeye hurusha ndege mara mbili kwa mwezi na amefanya kazi kwa muda wa maika 72.

MTU MWENYE KIUNO CHEMBAMBA ZAIDI
Mwanamke mwenye umri wa miaka 26 Michele Kobke amekibana kiuno chake hadi kufikia inchi 25 kwa kuvaa mkanda kwa muda wa miaka 3.Anatarajia kukipunguza hadi kufikia inchi 14.

MWANAMKE MWENYE UWEZO WA KUKUMBUKA KILA KITU
Jill Price anasema anauwezo wa kukumbuka kila kitu tangu akiwa katika umri wa tineja.Ana kumbukumbu ya watu aliokutana nao wote na ni muda gani huamka.Kila kumbukumbu ya kila siku huihifadhi kwenye ubongo wake.

MWANAMME MZEE KUPANDA MLIMA EVEREST
Mwaka 2013,akiwa na miaka 80,Yuishiro Miura  alikuwa mtu mzee zaidi kufika kileleni mwa mlima mrefu zaidi duniani.Miura alianza kuwa maarufu mwaka 1970 baada ya kuwa mtu wa kwanza kuruka chini akitokea juu ya mlima Everest.

MWANAUME AMBAE DAIMA HUNYANYUA MKONO WAKE JUU
Mwaka 1973,Sadhu Amar alinyanyua mkono wake kumuheshimu mungu wa kihundu Shiva na kama hakuushusha tena.Watu wengi miongoni mwa wafuasi wake nao hawashusha mkono wao miongo kadhaa sasa.

MTU MWENYE OPARESHENI NYINGI ZAIDI DUNIANI
Eileen Brown kutoka England amefanyiwa oparesheni nyingi sana miaka 20 iliyopita kiasi kwamba sehemu ambazo bado zina uhalisia katika mwili wake ni hipsi ya kushoto na kiwiko cha kushoto.

MZEE ZAIDI KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE NDEGE NA KUELEA ANGANI
Georgina Harwood akiwa na umri wa miaka 100,alifurahia kujirusha na kuelea angani(SKYDIVING) nchini South Africa.Hii ilikuwa mara yake ya tatu ambapo mara kwanza alikuwa na miaka 92.

MWANAMKE ANAEJIPINDA ZAIDI DUNIANI
Julia Gunthel ambae ni mrusi,ambae pia anajulikana kwa jina la Zlata,ndie mwanamke anaweza kujipinda zaidi duniani.Kwa sasa anaishi na kufanya kazi Ujerumani na kwa sasa ameingia kwenye vitabu vya Guinness.

MTU ALIEFANYA KAZI MUDA MREFU ZAIDI
DUNIANI
Mtu aliefanya kazi moja kwa muda mrefu zaidi duniani ni Bibie Polly Gadsby akiwa na kampuni ya Archibald Turner & Co. iliyoko Leicester UK,akiwa na miaka 9.Ameifanya kazi hii kwa miaka 85 na katika umri wa miaka 95 bado anaendelea na kazi yake.

MCHEZA POLE MZEE ZAIDI
Huyu hufanya mazoezi ya POLE dancing akiwa na miaka 60,mjini Nanjing nchini China.Sun Fengqin alianza kucheza mwaka 2012 na kuwa mtu maarufu nchini China.

MTU MWENYE MUSTACHI MREFU ZAIDI DUNIANI
Huyu ameanza kufuga mustachi huu kwa muda mrefu zaidi hadi kuwa mrefu kiasi hiki.Yeye hutumia saa moja na nusu kila siku kuuchana mustachi huo.

MAPAFU  YENYE NGUVU ZAIDI
Manjit Singh,ndie anaeshikilia rekodi ya kuwa mtu mwenye mapafu yenye nguvu zaidi duniani.Alitumia mapafu yake kujaza ballon lenye kipenyo cha mita 2.5 kwa muda dakika 42.

MACHO YA X-RAY
Natasha Demkina raia wa Urusi anasema kuwa yeye ana macho yanayoona kama X-RAY  yanayomwezesha kuona ndani ya miili ya watu na kufanya uchunguzi wa kina kwa watu kuliko hata madakiktari bingwa wanaweza fanya.Hii imepelekea kufuatwa na waandishi wa habari,madaktari na watu wanaouamini uwezo wao.

MWANAMKE MWENYE PEMBE KICHWANI
Pembe hiyo inayojulikana kama DEVIL HORN
anayo mwanamke anaejulikana kama Zhang Ruifang.Pembe hiyo ilijulikana mwaka 2010.

MTU MWENYE MISULI ZAIDI
Anaitwa Romario Dos Santos Alves,ambae ni mjenga misuli wa kibrazil.Huyu aliamua kujifananisha na yule INCREDIBLE HULK wa filamu na kuamua kujidunga madawa na pombe pamoja na oil mishipani mwake.









Thursday 25 February 2016

TAMBUA NAMNA MSTARI KWENYE KIGANJA CHAKO UNAVYOHUSIKA KATIKA MAHUSIANO YAKO NA NDOA YAKO.


Mara nyingi watu huenda kwa wanaosoma viganja ili waweze kuelezewa kuhusu wakati wao ujao yaani utabiri na pia bahati zao.Utaalamu huu wa usomaji viganja mara nyingi sana umetumika na huwa kweli kwa asilimia kubwa hasa linapokuja suala la mapenzi na maisha.
Sitakuchosha saaana ila cha kufanya unganisha viganja vyako hapo ulipo.Ile sehemu unakoshikia chakula iwe juu.Mara baada ya kuviunganisha vema hakikisha mistari ya vidole inaendana vema.Baada ya hapo itizame kwa makini mistari mikubwa inayofuatia ilioko chini kabisa baada ya mstari wa mwisho wa kidole kidogo.
Tazama hapa chini kujua matokeo yake:

1)MISTARI INA UREFU SAWA.
Hii inaanisha kuwa mchumba wako atakubaliwa na kupendwa na wengi.Wengi watamfurahia na kumwona mke mzuri na mwema.Pia mtu huyu huwa mkuu,mwenye kujiamini ana asiependa shitukizo.



2)MSTARI WA MKONO WA KULIA UKIWA JUU
Hii inaonesha kuwa inakupasa uwe makini sana na uamuzi wowote ule utako ufanya katika maisha yako.Usikurupuke inapaswa uwe mtulivu sana.
Pia mtu wa aina hii hupendelewa zaidi na wakubwa,pia ana uwezekano wa kuoa au kuolewa na mtu alemzidi umri,mwenye uwezo wa kutambua watu wanaomzunguka,hali iliyopo na asiejali watu wanafikiri nini juu yake.


3)MSTARI WA MKONO WA KUSHOTO UKIWA JUU ZAIDI
Hii inamaanisha kuwa wewe ni mtu jasiri na anaethubutu kukabiliana na changamoto za kimapenzi.Pia hupendelea zaidi vitu visivyo na uhusiano na mahusiano yako.Huyu pia huweza kuoa au kuolewa na mwanafunzi au mgeni wa ng'ambo.Mara nyingi hawa ni watanashati na warembo.


Msimulizi: Rakshita Nagayach

WASIRA AMSHUSHIA KICHAPO MWANDISHI WA HABARI


ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika Serikali ya awamu ya nne, Steven Wasira, jana nusura atembeze mkong’oto mahakamani.
Wasira alijikuta jaribio lake la kutaka kumpiga na kumnyang’anya kamera mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Michal Jamson likikwama baada ya kushindwa kumkamata.
Tukio hilo la aina yake lililovuta hisia za watu wengi waliokuwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lilitokea jana saa 5 asubuhi wakati Wasira alipotoka ndani ya mahakama hiyo baada ya ombi la wapigakura wake watatu kupewa ruhusa ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kutupwa.
Baada ya kutoka ndani ya mahakama hiyo, Wasira aliye maarufu kwa jina la utani la ‘Tyson’, alikutana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa nje wanamsubiri ambapo alizungumza nao.
Lakini baada ya mpigapicha huyo kufika na kuanza kutekeleza majukumu yake, Wasira alionekana kukereka na kutaka kumkamata kwa lengo la kutaka kumpora kamera.

HALI ILIVYOKUWA
Dalili za Wasira kumsaka mpigapicha wa Mwananchi zilianza kuonekana eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza saa 3:29 asubuhi kabla ya kuelekea jengo la Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.
Baada ya kubaini uwepo wa mpigapicha huyo, alimfuata na kumhoji ni chombo gani anachofanyia kazi au anatoka mtandao gani wa kijamii, ambapo alimjibu kuwa ni mpigapicha wa gazeti la Mwananchi.
Hatua hiyo ilimfanya Wasira atafakari kwa muda kabla ya kuamua kuingia ndani ya jengo la Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa kesi ya wananchi watatu waliomba kukata rufaa ya kupinga ubunge wa Bulaya.
Baada ya dakika 25 kupita, mahakama ilitoa uamuzi kuhusu maombi ya wapigakura hao, lakini Wasira alibaki ndani kwa dakika kadhaa, na kutuma wapambe wake kuangalia kama waandishi wa habari wameondoka eneo hilo.
Baadaye Wasira alitoka nje na wapigapicha wakaanza kutekeleza majukumu yao kitendo kilichosababisha arudi ndani.
Akiwa ndani hakukaa muda mrefu, akatoka tena nje, na moja kwa moja akamfuta Jamson, huku akihoji sababu za yeye kupigwa picha.
“We kijana njoo hapa usikimbie, unafanya nini hapa muda wote? Nimekuona muda mrefu unanifuatilia,” alisema Wasira huku akimsogelea kutaka kumkamata na kumnyang’anya kamera yake.
Mpigapicha huyo alipohisi hatari, aliamua kukimbia na Wasira alijaribu kumkimbiza bila mafanikio.
Baada ya kushindwa jaribio hilo, Wasira ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, aliamua kwenda katika gari lake dogo aina Toyota Mark X lenye namba za usajili T 399 DBG.
Alipanda ndani ya gari hilo pamoja na mmoja wa wapigakura wake waliofungua kesi ya kupinga ubunge wa Bulaya, aliyetambulika kwa jina la Janes Ezekiel.
Hatua hiyo iliwafanya wanahabari waliokuwa nje ya jengo la mahakama kupigwa na butwaa na ghafla waliona gari la Wasira likibadili mwelekeo na kuelekea kwa kasi eneo walipokuwa wamesimama.
Hali hiyo ilisababisha waandishi wa habari kukimbia ili kukwepa gari hilo lisiwagonge.
KAULI YA WASIRA
MTANZANIA lilipomtafuta Wasira kwa njia ya simu ili kujua sababu ya uamuzi wake wa kutaka kumpiga mpigapicha huyo, alisema kuwa alitaka kujua sababu za kumfuatilia kila eneo na hata kumpiga picha alipotoka msalani.
“Nashangaa hapakuwa na waandishi ila yeye tu,” alisema Wasira huku akimtaka mwandishi aliyempigia simu aonane naye ana kwa ana na kisha kukata simu.

RUFAA YATUPWA

Awali kabla ya tukio hilo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi kuhusu maombi ya kukata rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa wapigakura wa Jimbo la Bunda ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila waliokuwa wakiwakilishwa na mawakili Denis Kahangwa na Costantine Mtalemwa dhidi Mbunge Bulaya, Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma uamuzi huo wa Jaji Sirilius Matupa, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Eugenea Rujwahukwa, alisema baada ya kutolewa uamuzi wa kutupiliwa mbali kesi hiyo Januari 25, mwaka huu, wapigakura hao hawakuridhishwa, hivyo kuwasilisha tena maombi ya kwenda Mahakama ya Rufaa.

Alisema katika maombi hayo, mawakili wa wapigakura, Mtalemwa na Kahangwa waliomba kufungua shauri Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili itoe ufafanuzi kuhusu haki ya mpigakura ya kuhoji matokeo na ni vigezo gani vinatakiwa vitimizwe ili mpigakura aweze kuhoji matokeo ya uchaguzi.

Rujwahukwa alisema katika hatua za usikilizwaji wa maombi hayo, wakili wa Serikali, Kidando, alileta pingamizi kuwa maombi hayo hayaendani na sura ya 141 sheria ya rufaa kifungu 15(2) na 1(2) ambapo licha ya mabishano hayo Jaji Matupa alikubaliana na sura hiyo.

“Jaji amekubaliana na sura 141 ya sheria ya rufaa na maombi haya ni ya msingi chini ya kifungu 15(a)(b), lakini yalipaswa kuwa chini ya  kifungu 15(c) ambacho ndiyo sahihi kwa ajili ya maombi kama haya, hivyo mahakama imeyatupilia mbali maombi haya ya rufaa kwa ajili ya uimarishaji wa haki na kwamba bado wanayo nafasi ya kuleta maombi mengine ndani ya muda wakizingatia vifungu hivyo vya sheria,” alisema Rujwahukwa.

Januari 25, mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mohamed Gwae, aliitupilia mbali kesi namba moja ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Bunda Mjini iliyofunguliwa na wapigakura hao kwa sababu waleta maombi hakuwa na mamlaka kisheria.


MWAKA 1998

Mwaka 1998, Wasira alidaiwa kumpiga Mhariri Mkuu wa gazeti la Hoja, Sadick Yassin nje ya Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), baada ya gazeti hilo kuandika kichwa cha habari ‘Swahiba wa Mrema aanzisha chama kuiondoa CCM madarakani’.

Wasira hakufurahishwa na neno ‘swahiba’ kwa madai kuwa ni tusi, wakati huo akiwa mwanzilishi wa chama cha upinzani cha National Development Congress (NDC) ambapo alikuwa mwenyekiti.

Katika tukio hilo, Wasira anadaiwa alimpiga ngumi mhariri huyo kisha kumkimbiza hadi ndani ya ofisi za Serikali, huku waandishi wakongwe Raphael Hokororo na Mayage S. Mayage wakishuhudia tukio hilo.

Baada ya tukio hilo, Wasira alijisalimisha Kituo cha Polisi cha Kati kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambako alihojiwa kutwa nzima.

Baada ya mahojiano kukamilika, siku iliyofuata alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi yake iliendeshwa kisha kufutwa baada ya walalamikaji kutohudhuria mahakamani.

Source:mtanzania.

Wednesday 24 February 2016

JE ULISHASHUHUDIA HARUSI YA KICHINA?


Harusi ni moja ya sherehe muhimu katika maisha ya karibu watu wote duniani, ambayo inaonesha mapenzi kati ya wanandoa na pia kuthibitisha wajibu na majukumu yao katika ndoa. Kila nchi na taifa lina utamaduni wake wa jadi kuhusu harusi, lakini mila na desturi hizo pia zinabadilika kwa kuendana na wakati.

Nchini China, rangi nyekundu inatumika kwenye harusi ya kijadi, kwa kuwa wachina wanaamini kuwa rangi hiyo inaonesha furaha, na inaleta bahati nzuri na neema. Nyumba ya harusi inatakiwa kupambwa kwa mapambo yenye rangi nyekundu, kama vile kubandika karatasi nyekundi zenye maandishi ya kichina Xi, maana yake ni Neema. Bibi na bwana harusi wanatakiwa kuvaa nguo za jadi za rangi nyekundu, na maua ya rangi nyekundu kifuani. Bibi harusi pia anatakiwa kufunika sura yake kwa kitambaa chekundu, kabla ya kuingia kwenye kiti kilichofunikwa kwa mapambo kinachobebwa na watu, ambacho kwa kichina kinaitwa "Jiaozi". Kwenye harusi ya jadi nchini China, bibi harusi hatembei mwenyewe, anatakiwa kubebwa kwenye kiti hicho kutoka nyumbani kwao hadi nyumbani kwa bwana harusi, halafu bwana harusi atafunua kitambaa hicho, ili kuwaonesha ndugu zake sura ya bibi harusi.
Hiyo ni harusi ya jadi nchini China, kutokana na utandawazi wa kiutamaduni duniani, harusi za vijana wa China nazo zimeanza kuchanganya mitindo ya kigeni. Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, mara baada ya China kutekeleza mageuzi na kufungua mlango kwa nje, harusi ilikuwa rahisi tu, wanandoa wapya huandaa sherehe na tafrija ndogo, wengine waliamua kufanya utalii wenyewe badala ya sherehe ya harusi.
Wakati huo, gharama za harusi zilikuwa chini, hata yuan mia kadhaa zilikuwa zinatosha kabisa. Mahari ya bibi harusi pia haikuwa kubwa, watu wa wakati huo walipendelea saa, baiskeli, cherehani na radio, hata masofa walitengeneza kwa mafundi seremala. Picha za harusi za miaka ya 80, ni tofauti na za sasa. Picha hizo zilikuwa za rangu nyeusi na nyeupe, na huwa zilipigwa ndani ya studio ya kupigia picha.
Tukiingia miaka 90 karne iliyopita, vijana walipendelea tena harusi za jadi za kichina, lakini walifanya sherehe za harusi kwenye hoteli za kifahari. Baadhi ya vijana wanaopenda mtindao wa maisha ya magharibi walifanya harusi zao za kimagharibi kwenye ukumbi wa kanisa. Gharama za harusi ziliongezeka kulingana na za miaka ya 80, asilimia 73 ya harusi ziligharimu zaidi ya dola za kimarekani 1,600, na asilimia 27 ya harusi zilitumia zaidi ya dola za kimarekani 4,800. Kwa upande wa mahari, vijana wa wakati huo walipendelea vifaa vya umeme vya nyumbani, kama vile televisheni za rangi, kiyoyozi, mashine ya kufulia, na jokofu, na pia walianza kutilia maanani mapambo ya ndani. Wakati huo, picha za harusi zilikuwa zinachanganya na mtindo wa kimagharibi, yaani bibi harusi huvaa gauni jeupe la harusi na bwana harusi huvaa suti.

Baada ya kuingia karne ya 21, harusi zimekuwa za aina mbalimbali, jadi kwa kisasa, rahisi kwa fahari, na hata kuna zile zinazokusudia kuvunja rekodi ya dunia. Wakati huo, katika miji 30 mikubwa nchini China ikiwemo Beijing, Shanghai, Nanjing na Dalian, wastani wa wanandoa wapya milioni 3.73 walitumia zaidi ya dola za kimarekani elfu 20 katika harusi zao, ikiwa ni gharama ya sherehe pekee, kama zikiwekwa pamoja gharama za kununua nyumba na magari, kwa jumla harusi katika miji ya Shanghai, Beijing na Hangzhang itazidi dola za kimarekani laki 1.6, na kwa sehemu za pwani, inafikia dola za kimarekani elfu 64. Wakati huo, nyumba imeanza kuwa sehemu muhimu ya mahari, na pia ni mzigo mkubwa kwa wanandoa na hata familia zao. Kutokana na kuathirika na tamaduni kutoka nje, vijana wa karne mpya wanapendelea picha za harusi zenye ubunifu, kama vile picha za harusi kwenye vilele vya milima ya theluji au chini ya maji.
Ripoti ya uchunguzi kuhusu sekta ya harusi nchini China kati ya mwaka 2006 hadi 2007 inaonesha kuwa, wakati huo wastani wa gharama za harusi ilizidi dola za kimarekani elfu 19. Kwa mfano mjini Shanghai, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006, wastani wa gharama za harusi ilizidi dola za kimarekani elfu 25, ambayo iliongezeka kwa mara tatu kuliko miwaka mitatu iliyopita.

Hiyo ni hali ya mijini, kwenye sehemu za vijijini, gharama za harusi ni mzigo mkubwa zaidi zikilinganishwa na mapato yao. Mtaalamu wa mambo ya ndoa na harusi nchini China Bi. Li Yinhe amesema, gharama ya harusi ni kama mara 10 ya pato la jumla la familia kwa mwaka mmoja. Kijana Liu Jian anatoka kijiji kimoja wilayani Daokou katika mji wa Anyang mkoani Henan, sasa anafanya kazi za vibarua mjini Beijing. Anasema, hivi sasa harusi kijijini kwake hugharimu dola za kimarekani elfu 32 hadi elfu 48, lakini pato la jumla la familia nzima katika mwaka moja ni dola za kimarekani 300 hadi 500 tu.
Tofauti na hali ya zamani, harusi za leo ni kama maonesho makubwa. Wanandoa wapya wanashindana ufahari wa harusi zao, jambo lililoifanya sherehe hiyo kuwa mzigo mkubwa wa kifedha kwa familia za pande zote.

Source:CRI swahili

Tuesday 23 February 2016

Huzuni yaikumba Hip Hop Marekani,rapa Lil Wayne abakiza mwezi wa kuishi.


Huzuni kubwa yaikumba Hip Hop Marekani baada ya mwanahipop Lil wayne kutangaza kuwa amebakiza mwezi mmoja wa kuishi katika maisha yake.
Hii ni habari mbaya zaidi katika game ya music nchini marekani baada ya Lil wayne kuitisha kikao na waandishi wa habari na kuwaeleza hayo.Aliitisha kikao hicho jijini Atalanta na kuelezea kuwa na tatizo la KANSA YA NGOZI ambayo wataalamu wa afya walimwambia kuwa ana majuma matano tu ya kuishi hapa duniani.
Akionekana akiwa na afya iliyo dhaifu sana alisema kuwa daktari alimwambia kuwa ana kansa iliyoko "STAGE 4" yani hawawezi kumsaidia zaidi ya kusubiri umauti.
Haya ni maneno aliyosema daktari  huyo kwa Lil wayne
             " With 80% percent of his body covered in tattoos our scanners were always falling to detect the cancer in his skin all the time until it reaches stage 4…The only thing we advice him is to enjoy the few days he got left. Wayne always visited me for regular check ups so we were close, The only thing he pissed me off with was stealing my cough syrup every time he visited”. Joked Dr Williams.

Lil wayne amepanga kutumia maisha yake yaliyobakia akiwa na wenzie wa kundi lake la YMCMB.
Hapa chini ni maneno aliongezea rapa Lil wayne kwenye kikao hicho
         " I would be grateful if someone can always pour a bottle of codeine and promethazine cough syrup every week on my tomb while two red bones twerk on either side of my grave…I’m dying a happy man and I hope ya’ll remember me”
  Alipomaliza kusema maneno hayo aliondoka huku akiacha mshituko mkubwa sana kwa waandishi wa habari na washabiki wake.
Hivi karibuni alikwenda kwa mtaalamu wake wa kumchora "Tattoo" yenye neno "FUCK CANCER" lakini mtaalamu huyo alimkatalia katakata rapa huyo.

Source: http://www.viroshare.com/celebrities

Monday 22 February 2016

LULU azushiwa kifo mitandaoni

Msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amezushiwa kifo katika mitandao ya kijamii na hivyo kupelekea taharuki kubwa miongoni mwa washabiki wake.Akiliongelea suala hilo kwenye mtando wa instagram Lulu amesema haya hapa chini
 
       "   Nasikia Nimekufa
Wewe uliyePost hii. Kama wewe utakuwepo TUTAONANA TENA 2017 Inshaallah
Alafu jifunze na kuandika ELIZABETH vizuri kwanza
(Niki report LIVE kutoka heaven)
This shows how Jina Langu lina KiKi😋nishasema MNIACHE JMN😪watsup!???
Kufa ntakufa SIKATAI lkn mpk nimalize MIAKA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA"

Sunday 21 February 2016

Download Ben Paul & Jux-Nakuchana.mp3

BEN PO & JUX-NAKUCHANA.mp3                                                                                                                                                                                                                                                                    
                                                                                                                    























 To download click DOWNLOAD NOW









Download MIRROR FEAT BARAKA DA PRINCE-NAOGOPA audio

Download Mirror feat Baraka da Prince-Naogopa

















click DOWNLOAD 
or you can also DOWNLOAD HERE

WAJUE wanyanyua vyuma(nondo) 8 waliozidisha kiasi duniani

Ulimwengu wa kujenga misuli ni miongoni mwa michezo ambayo inaweza kukupa faida kama tuzo n.k kwa wengine pia inaweza kuleta inaweza kuleta uharibifu wa mwili kwa wengine pia.Wanaojihusisha na michezo hii hufanya mazoezi kwa bidii kuweza kupata maumbile wanayoyahitaji.Wakati mwingine hulazimika kuzidisha mazoezi ili kuweza kupata maumbile wanayoyahitaji.
Wafuatao ni wanamieleka 8 ambao walishindwa kuendana na ratiba maalumu ya ufanyaji mazoezi na kujikuta wamezidisha kipimo na hivyo kupelekea kuharibu miili,afya na hata umauti.

1.ANDREAS MUNZER
Huyu alikufa akiwa na umri wa miaka 32 mwaka mnamo 1996 kutokana na kushindwa kufaanya kazi kwa viungo mbali mbali vya mwilini mwake pia baada ya kuishiwa kabisa mafuta mwilini mwake.Wakati anakufa MOYOwake ulikuwa mkubwa kulko saizi ya kawaida ya binadamu na pia INI lake lilikuwa na matatizo pia.

2. GARY HIMING
Huyu alijulikana sana katika mashindano ya kutunisha misuli kwa miaka kadhaa.Alizidisha kutanua misuli yake hadi akafariki akiwa stejini mwaka 2009 wakati akishiriki mashindano ya IFBB jijini Victoria,AUSTRALIA.Inasemekana alifariki kutokana na ugonjwa wa shambulizi la moyo 'heart attack'.Cha ajabu ni kuwa baada ya kifo chake mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa hospitali lakini shindano liliendelea kama kawaida.

3.MOUSTAFA ISMAIL
Huyu alikuwa na umbo lisilo la kawaida na alifanikiwa kushinda katika rekodi za Guinness za dunia kwa kuwa mtu mwenye misuli misuli mikubwa zaidi ya mkononi 'Biceps' ilikuwa na '31 inches'.Alijulikana pia kwa jina la EGYPTIAN POPEYE.Hakutumia madawa ya aina yoyote ispokuwa alikuwa na mlo mkubwa sana uliojulisha kiasi kikubwa cha protein,kiasi cha kaa wa baharini karibu kilo kumi na vidumu vitatu vya maji.

4.BERTIL FOX
Bertil Fox alipata umaarufu mkubwa sana kwa muda mchache tangu ajiunge na mchezo huu na alifanikiwa kushinda mataji mengi kwa muda mfupi.Lakini kutokana na kutumia kiasi kikbwa sana cha homoni za ukuaji,mwili wake na ubongo vilianza kufanya kazi kinyume na kawaida ya binadamu.Hali hii ilimsababisha kuwa na tabia mbaya sana hali iliyopelekea hadi akamuua aliekuwa mpenzi wake na mamake mpenzi wake mwaka 1997 kabla hawajaachana.Hii ilipelekea ahukumiwe KIFO lakini baadae alipunguziwa adhabu na kuwa kifungo cha maisha gerezani.

5.ROMARIO DOS SANTOS
Huyu ni kijana mwenye umri wa miaka 25 ambae hutunisha misuli yake kwa kujidunga mafuta pamoja na pombe.Yeye hutumia LETHAL INJECTIONS kujidunga mishipani mwake ili kuitunisha misuli yake. ambayo ilifikia '25 inches' kiasi ambacho sasa anakabiliwa na matatizo makubwa sana kifya.

5.GREGG VALENTINO
Gregg Valentino  aliathirika zaidi na mchezo huu hadi kufikia hatua ya mwili wake 'kulipuka' mara baada ya misuli yake ya mkononi kupata maambukizo kutokana na kutumia sana sindano ili kujidunga madawa ya kusaidia kutunisha misuli yake.

 7.MARKUS RUHL
Markus Ruhl ndie mshiriki aliekuwa na mabega mapana zaidi kuliko washiriki wote wa mchezo huu.Pia inasaidikiwa na kuaminiwa kuwa Markus ni mmoja kati ya watunisha misuli wenye nguve zaidi kuwahi kutokea duniani.

8.ARLINDO DE SOUZA
Huyu alijulikana pia kwa jina la utani la "The Mountain".Alikuwa na misuli ya mkononi yenye saizi ya '29 inchs' na alikuwa anajidunga madawa pia ya kusaidia kutunisha misuli.Amempoteza rafiki yake wa karibu zaidi kutokana na tabia hii ya kutumia madawa ya kutunisha misuli ila ndo kwanza hajali na anaendelea nayo kama kawaida

Saturday 20 February 2016

IJUE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NA DALILI ZAKE..

KANSA YA SHINGO YA KIZAZI.
Shingo ya kizazi(CERVIX) ni sehemu ya mfuko wa kizazi kuelekea kwenye njia ya uke.Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo:1.Kupitisha mbegu za kiume kuelekea ktk mirijga ya uzazi ili kupevusha yai.2.Kupitisha damu ya hedhi.3.Ndio mlango anaopita mtoto wakati wa kuzaliwa kutoka ktk mfuko wa uzazi hatimaye ukeni.
Kama zilivyosehemu zingine za mwili,sehemu nayo inaweza kupata maradhi ikiwemo kansa.
Ugonjwa huu uwaathiri wanawake wengi wa rika zote waliokatika umri wa kuzaa.Miaka ya nyuma kabla ya maambukizi ya Ukimwi kugundulika Kansa ya Shingo ya Kizazi ilikuwa ikiwapata zaidi wanawake wenye umri wa miaka 45 na kuendelea.Lakini miaka ya hivi karibuni mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa anaweza kupata tatizo hili.
SABABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.
Ugonjwa una sababishwa na virusi viitwavyo Human papiloma.Ambapo mtu anaweza kupatwa na hawa virusi wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi.
DALILI.
1.Kutokwa na majimaji au uchafu usio wa kawaida ukeni.
2.Kutokwa na damu ukeni hali ya kuwa siyo hedhi au umri wa kupata hedhi umekoma lakini anaona damu inatoka.
3.Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
4.Kutokwa na damu baada ya kujamiiana.
5.Kuwa na maumivu makali ya tumbo hasa chini kitovu au kwenye nyonga.
TABIA HATARISHI AU WALIOHATARINI
Je, ni tabia zipi hatarishi zinazoweza kupelekea kupata ugonjwa huu
1.Kuanza ngono mapema katika umri mdogo chini ya miaka 18
2.Uvutaji wa sigara
3.Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi
4.Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi
5.Kutokula mboga za majani na matunda
6.Kuzaa mara kwa mara
7.Wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
TIBA.
Kansa ya shingo ya kizazi inatibika iwapo itagundulika mapema ikiwa katika hatua za mwanzo.
Saratani ya shingo ya kizazi inapogundulika katika hatua za mwisho, uwezekano wa kutibika unakuwa ni mdogo na gharama za matibabu zinakuwa kubwa!
Utagunduaje mapema kama una saratani ya shingo ya kizazi?
Kufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi angalau mara 1 kwa mwaka
KUMBUKA KANSA HII NDIYO KANSA INAYONGOZA KUSABABISHA VIFO NCHINI.

Thursday 18 February 2016

Historia ya UISLAM na dini ya kiislamu



Historia ya Uislamu
Historia ya dini ya kiislamu haikuanza na Mtume Muhammad (SAW) kama wanavyofikiria watu wengi bali imeanza tangu alipoletwa Nabii wa kwanza ulimwenguni, ambaye kwa mujibu wa Waislamu ni Nabii Adam alipoteremshwa ulimwenguni na kupewa mwongozo na Mwenyezi Mungu wa namna gani kuishi hapa duniani kwa njia nzuri ya wema na hisani kwa kushikamana na mafunzo yake Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.
Masimulizi ya historia hii ya Uislamu yameelezwa katika vitabu vitakatifu vya Mitume mbali mbali waliokuja duniani na kadhalika katika Qurani Tukufu. Umma mbali mbali zilizopita huko nyuma zimetajwa katika Qurani na kuelezwa namna gani zilivyoangamizwa kwa kutokubali ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuwakataa Mitume yake nao wakaletewa adhabu kali ya upepo au mvua au mafuriko na kadhalika.

Inasemekana katika historia ya Uislamu kuwa Mwenyezi Mungu alileta Mitume na Manabii kiasi cha 124,000 kwa ajili ya kuwaongoza binadamu kutokana na giza la ujinga na ujahili na utumwa wa kuabudu miungu mingi kuwatia kwenye nuru na mwangaza wa elimu na maarifa na ujuzi wa kumjua Mwenyezi Mungu wao aliyewaumba na kuwafanya wawakilishi wake hapa duniani. Mitume hawa na Manabii waliletwa na Mola wao kuwafahamisha wanadamu ukweli na haki iko wapi na wengine katika wao wakapewa vitabu ili wawaongoze wenziwao katika wanadamu kuwaelekeza kwenye njia ya haki.
Visa vya Mitume na Manabii hawa vinatueleza mengi kuhusu hawa wajumbe watukufu wa Mwenyezi Mungu na kuwa wote walitumwa na Mola wao kutangaza Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye hana mshirika na pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki asishirikishwe na chochote au yeyote katika viumbe vyake wakiwa ni binadamu wenziwao au mizimu au majini au wanyama au vyenginevyo katika viumbe vyake.

Zama za Adam hadi Isa (Amani iwe juu yao)
Historia ya Uislamu imegawanyika zama mbili kubwa. Moja ni tangu alipoletwa Nabii Adam ulimwenguni mpaka alipoletwa Nabii Isa, na muda huu ni muda ambao Mwenyezi Mungu alikuwa akileta Mitume na Manabii kwa watu fulani na makabila fulani na ujumbe wake ulikuwa wakati huu kwa watu maalumu tu si kwa wanadamu wote kama inavyoeleza dini ya Uislamu. Zama za pili za historia ya Uislamu zinaanza tangu alipoletwa Muhammad (Amani iwe juu yake) mpaka siku ya Kiyama.

Zama za Mtume Muhammad (SAW) mpaka siku ya Malipo
Historia ya Uislamu baada ya kuletwa Mtume Muhammad (SAW) ilibadilika sana hasa baada ya Waislamu kuenea sehemu zote za duniani. Nao muda huu wa historia ya Uislamu umegawanyika sehemu mbali mbali. Kwa ufupi, zama zifuatazo ndizo zinazozungumzia historia ya Uislamu:

1- Maisha ya Muhammad - Tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad mpaka kufa kwake. 2- Makhalifa Waongofu - Tangu aliposhika ukhalifa Abubakar mpaka alipouliwa Ali bin Abi Talib 3- Ukhalifa wa Bani Umayya 4- Ukhalifa wa Bani Abbas 5- Ukhalifa wa Wafatimi 6- Salajiqa 7- Vita vya Misalaba 8- Mamaliki 9- Hujuma za Wamongoli 10-Ukhalifa wa Maothmani - mpaka 1924 11-Utawala wa Wazungu 12-Kupata uhuru dola za kiislamu 13-Historia ya Uislamu mamboleo
Marejeo
http://en.wikipedia.org/wiki/Muslim_history#Timeline
http://www.fordham.edu/halsall/islam/islamsbook.html

Wednesday 17 February 2016

Ney wa mitego nae afunguka kufuatia mimba ya Wema kutoka


Nay wa mitego ameenelea kutoa ya moyoni kufuatia sakata lake na wema.Ney wa Mitego alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Maskani cha Efm kinachotangazwa na Gadner G Habash,alisema kuwa kama binadamu hawezi kufurahia tukio hilo.
     "Mimi kama binadamu siwezi kufurahia kuwa mimba ya dadangu imetoka.Mimi ni mtu ninaependa sana watoto au kuona mwenzangu anapata watoto.kama ni kweli nampa pole ila kama ni kiki alikuwa anatafuta bas ndo mwisho wake"
Hilo limekuja baada ya Ney kushambuliwa na mashabiki wa wema mara baada ya kupost picha ilikuwa inaonesha tumbo bandia la mimba katika mtandao wake wa Instagram...
Pia Ney amefunguka kwa BASATA na kusema kuwa mbina nyimbo nyingi za nje hazina maadili lakini zinaoneshwa na kupigwa radioni????

Download here:http://downloads.ziddu.com/download/25234056/Adele_Hello.mp3.html

Mimba ya Wema Sepetu yaharibika..😯




Mimba ya msanii wa Bongo movie Wema Sepetu imeharibika.Haya yamesemwa na boyfriend wake Idris Sultani kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Idris ameandika ujumbe ukionyesha kuhuzunishwa kwa kuharibika kwa ujauzito huo, kwani walikuwa wenye furaha huku wakiwatarajia watoto hao ambao inasemekana walikuwa mapacha.
"To my unborn twins, So quickly you came into our lives, So quickly torn away. Never got the chance to meet you, There's so much I want to say. All these thoughts running through my head, It's enough to drive me insane. Though you lived only 13 short weeks, You were loved so very much. I wish that I could hold you, I long to feel your touch. I pray that in another life, We get the chance to meet. God brings and takes as he plans and we cannot complain but only pray that all that was for a better reason and a better plan in store for us. We have learnt lessons painfully but wont stop trying again and again and do swear by the time your brothers and sisters are made to come to this world we will be more than ready for them.
Sincerely Your Dad. ❤️
Akimaanisha....... (Kwa mapacha wangu ambao hamjazaliwa, kwa haraka sana mlikuja katika maisha yetu, haraka sana mliondoka, sikupata nafasi ya kukutana nanyi, kuna mengi sana nataka kusema, mawazo haya yote yanazunguka kichwa changu, inanifanya mwendawazimu, ingawa muliishi kwa wiki fupi 13 tu, mulipendwa sana, nilitamani ningewabeba, nilitamani nihisi mguso wenu, naomba kwamba kwenye maisha mengine tutapata nafasi ya kuonana. Mungu hutoa na kutwaa kadri ya mipango yake na hatuwezi laumu, ila tunaomba ni kwa sababu na mipango mizuri aliyotuwekea sisi, tumejifunza kwa maumivu sana lakini hatutaacha kujaribu tena na tena, na naapa muda ambao kaka zenu na dada zenu wakija duniani, hii dunia itakuwa zaidi ya tayari kwa ajili yao.
baba yenu mpendwa.)
Post hiyo imeibua hisia nyingi huku wengi wao wakuwapa pole, na wengine wakiwapondea na kusema kuwa walikuwa wanadanganya kwani mwandada

Tuesday 16 February 2016

Je wajua kuwa kufanya mapenzi kuna FAIDA NYINGI SANA?Zisome hapa

Na Dokta Khamis Khalfan(maalumu kwa +18 na walio kwenye mahusiano)

Tendo la ndoa ni tendo linalohitaji raha na nafasi.Zifuatazo ni faida za kufanya mapenzi
 Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.

Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi ( menopausal women ) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya
oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.

Hupunguza msongo wa mawazo : Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle relaxant ), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.


. Hupunguza maumivu : Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi
upunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume: Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.

Huongeza uwezo wa kunusa: Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo ( brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu (brain olfactory bulb ).

Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi
uongeza kinga ya mwili: Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.


 Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke: Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa.
udhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida : Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa

Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini : Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.
uongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke ( vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection ).

kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini : Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.

Kuongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako: Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda.

Kusaidia kuishi kwa muda mrefu: Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.

Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi , kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano.

Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba:
Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne. chanzo.
Faida 17 za Kiafya za Kufanya Mapenzi Salama (Sex and its Health Benefits)

Viwango vya timu,wachezaji vyatoka EPL





Viwango vipya vya ligi ya EPL vyatoka kwa mzunguko huu wa 26 wa ligi.wachezaji wa Leicester nao wamo wakichuana vikali na wachezaji wa timu kubwa..
Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa skysports.