Sunday 21 February 2016

WAJUE wanyanyua vyuma(nondo) 8 waliozidisha kiasi duniani

Ulimwengu wa kujenga misuli ni miongoni mwa michezo ambayo inaweza kukupa faida kama tuzo n.k kwa wengine pia inaweza kuleta inaweza kuleta uharibifu wa mwili kwa wengine pia.Wanaojihusisha na michezo hii hufanya mazoezi kwa bidii kuweza kupata maumbile wanayoyahitaji.Wakati mwingine hulazimika kuzidisha mazoezi ili kuweza kupata maumbile wanayoyahitaji.
Wafuatao ni wanamieleka 8 ambao walishindwa kuendana na ratiba maalumu ya ufanyaji mazoezi na kujikuta wamezidisha kipimo na hivyo kupelekea kuharibu miili,afya na hata umauti.

1.ANDREAS MUNZER
Huyu alikufa akiwa na umri wa miaka 32 mwaka mnamo 1996 kutokana na kushindwa kufaanya kazi kwa viungo mbali mbali vya mwilini mwake pia baada ya kuishiwa kabisa mafuta mwilini mwake.Wakati anakufa MOYOwake ulikuwa mkubwa kulko saizi ya kawaida ya binadamu na pia INI lake lilikuwa na matatizo pia.

2. GARY HIMING
Huyu alijulikana sana katika mashindano ya kutunisha misuli kwa miaka kadhaa.Alizidisha kutanua misuli yake hadi akafariki akiwa stejini mwaka 2009 wakati akishiriki mashindano ya IFBB jijini Victoria,AUSTRALIA.Inasemekana alifariki kutokana na ugonjwa wa shambulizi la moyo 'heart attack'.Cha ajabu ni kuwa baada ya kifo chake mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa hospitali lakini shindano liliendelea kama kawaida.

3.MOUSTAFA ISMAIL
Huyu alikuwa na umbo lisilo la kawaida na alifanikiwa kushinda katika rekodi za Guinness za dunia kwa kuwa mtu mwenye misuli misuli mikubwa zaidi ya mkononi 'Biceps' ilikuwa na '31 inches'.Alijulikana pia kwa jina la EGYPTIAN POPEYE.Hakutumia madawa ya aina yoyote ispokuwa alikuwa na mlo mkubwa sana uliojulisha kiasi kikubwa cha protein,kiasi cha kaa wa baharini karibu kilo kumi na vidumu vitatu vya maji.

4.BERTIL FOX
Bertil Fox alipata umaarufu mkubwa sana kwa muda mchache tangu ajiunge na mchezo huu na alifanikiwa kushinda mataji mengi kwa muda mfupi.Lakini kutokana na kutumia kiasi kikbwa sana cha homoni za ukuaji,mwili wake na ubongo vilianza kufanya kazi kinyume na kawaida ya binadamu.Hali hii ilimsababisha kuwa na tabia mbaya sana hali iliyopelekea hadi akamuua aliekuwa mpenzi wake na mamake mpenzi wake mwaka 1997 kabla hawajaachana.Hii ilipelekea ahukumiwe KIFO lakini baadae alipunguziwa adhabu na kuwa kifungo cha maisha gerezani.

5.ROMARIO DOS SANTOS
Huyu ni kijana mwenye umri wa miaka 25 ambae hutunisha misuli yake kwa kujidunga mafuta pamoja na pombe.Yeye hutumia LETHAL INJECTIONS kujidunga mishipani mwake ili kuitunisha misuli yake. ambayo ilifikia '25 inches' kiasi ambacho sasa anakabiliwa na matatizo makubwa sana kifya.

5.GREGG VALENTINO
Gregg Valentino  aliathirika zaidi na mchezo huu hadi kufikia hatua ya mwili wake 'kulipuka' mara baada ya misuli yake ya mkononi kupata maambukizo kutokana na kutumia sana sindano ili kujidunga madawa ya kusaidia kutunisha misuli yake.

 7.MARKUS RUHL
Markus Ruhl ndie mshiriki aliekuwa na mabega mapana zaidi kuliko washiriki wote wa mchezo huu.Pia inasaidikiwa na kuaminiwa kuwa Markus ni mmoja kati ya watunisha misuli wenye nguve zaidi kuwahi kutokea duniani.

8.ARLINDO DE SOUZA
Huyu alijulikana pia kwa jina la utani la "The Mountain".Alikuwa na misuli ya mkononi yenye saizi ya '29 inchs' na alikuwa anajidunga madawa pia ya kusaidia kutunisha misuli.Amempoteza rafiki yake wa karibu zaidi kutokana na tabia hii ya kutumia madawa ya kutunisha misuli ila ndo kwanza hajali na anaendelea nayo kama kawaida

7 comments:

  1. Hahahaaaaa thanx Mr Saggy man

    ReplyDelete
  2. Pamoja sana keep on it....fanya mazoezi kwa sana

    ReplyDelete
  3. Bora wewe! Kuliko wanaolazimisha views kwa story Na vidio fake, weka vitu tofauti Kama hivi, dairy ntakuja kukutembelea humu.

    ReplyDelete
  4. Pamoja sana Mabula tuko pamoja mkuu

    ReplyDelete