Showing posts with label Habari kali. Show all posts
Showing posts with label Habari kali. Show all posts

Tuesday, 29 March 2016

JIONEE WATU WENYE UWEZO WA AJABU NA KUSHANGAZA


Je unafahamu kuwa watu wenye nguvu za ajabu kuliko uwezo halisi wa kibinadamu wapo?Ni kweli watu hao wapo na wengine wanaishi hadi sasa.Ni watu ambao wana vitu vya ajabu kama uwezo,nguvu na kuwa imara madhubuti.Wafuatao ni baadhi ya watu hao

1.WIM HOF
Huyu ana uwezo wa kukaa muda  mrefu sana eneo la baridi kali sana bila kupata madhara yoyote yale.Huyu ni mtu halisi anaweza kukaa muda mrefu sana eneo la baridi kali sana.Anazo tuzo 21 za Guinness ikiwemo ya kuoga kwenye maji ya barafu kwa muda mrefu.Huyu anaweza kukaa kilele cha mlima kilimanjaro kifua wazi kwa muda mrefu.

2.KELVIN RICHARDSON
Huyu ana uwezo mkubwa sana wa kuwaelewa wanyama.
Ana uwezo mkubwa sana wa kufanya urafiki hata na wanyama wakali zaidi duniani bila tabu yoyote.Ana uwezo wa kuwa na urafiki na chui,simba na fisi.Huwafanya marafiki na hata kulala nao pia.

3.CLAUDIO PINTO
Huyu anajulikana kama MACHO YA DARUBINI.Ana uwezo wa kuyatanua macho yake kipimo cha 7mm ambapo ni kiasi cha 95% ya mzunguko wa jicho lake.

4.HAROLD WILLIAMS
Anajulikana kama MWALIMU WA LUGHA.Huyu anasifika kwa kuwa na uwezo wa kujua lugha nyingi sana duniani.Je wewe una uwezo wa kujua lugha ngapi katika maisha yako yote?Huyu anafahamu lugha zaidi ya 58 ambazo anaziongea na kuandika bila shida yoyote ile.
Sio peke ake alie na kipaji hiki,pia wapo John Browning,Joseph Caspar na Doktar Carlos do Amaral Freire.

5.TIBETAN MONKS
Wana uwezo wa kuweka sawa JOTO la miili yao kwa kutumia akili au ufahamu wao.Wana uwezo qa kubadili joto la miili yao kwa kutumia akili yao tu.Wamewahi kurekodiwa wakibadili jotoridi lao kufikia kiasi cha nyuzi joto 8 za sentigredi.

6.RATHAKRISHNAN VELU
Anajulikana kuwa na meno ya ajabu yenye nguvu sana maarufu kama 'steel teeth'.Ana uwezo wa kuvuta treni ya mabehewa saba akitumia meno yake kuivuta kwa kutumia kamba ya chuma.Anajulikana pia kwa jina la KING TOOTH.

7.DANIEL BROWNING SMITH
Huyu anajulikana kama 'The rubber boy' ana uwezo wa kujipinda zaidi katika mikao mbali mbali.

8.STEPHEN WILTSHIRE
Ana uwezo mkubwa sana wa kukumbuka.Huyu ana uwezo wa kutazama kitu mara moja tu na kuweza kukichora kwa ufasaha kabisa.Ni maarafu sana kwa kuchora picha za miji mbali mbali kwa kuiangalia mara moja tu.Kama watu wengine hutizama mara kwa mara katika uchoraji huo,yeye hutizama mara moja tu na kuchora sehemu kubwa ya mji husika.

9.JESUS ACEVES
Huyu ni mtu mwenye nywele nyingi zaidi za usoni.Anapatikana katika familia ya kimexico yenye wanafamilia 24 ,huwa anazunguka duniani kuonesha watu muonekano wake huo.

10.DANIEL TAMMET
Ni mtaalamu sana wa mahesabu na hesabu kwa ujumla.Hufanya kwa kutumia akili yake hesabu nzito nzito tena kwa speed ya hali ya juu sana.Pia ana uwezo wa kuongea lugha saba bila shida.

11.GARRY TURNER
Je ngozi yako ina uwezo wa kujivuta kwa kiasi gani?Kutana na jamaa huyu ambae ngozi yake hujivuta kama mpira.Huivuta ngozi yake kwa namna mbali mbali.Hii inatokana ngozi yake kupungua 'Collagen'

12.NOORSYAIDAH
Ni mwanamke wa kiindonesia ambae anasema kuwa mwili wake una tabia ya kuota waya kwa muda usiopungua miaka ishirini sasa.
Waya hizo huwa kiasi cha sentimita 10 hadi 20.

13AL HERPIN
Kqa kawaida baada ya kukaa siku chache bila kulala kabisa mwili HUZIMIA.Lakini kwa mtu huyu AL,hajawahi kabisa kulala katika maisha yake na hivi sasa ana miaka 94.
Wanasayansi wanaamini kuwa inawezekana hali hiyo ilisababishwa na jeraha alilopata mama yake siku chache kabla ya kumzaa.

14.LIEW THOW LIN
Anajulikana kama MAGNETIC MAN,raia huyu wa Malaysia ana uwezo wa ajabu sana amabpo mwili wake una uwezo wa kuvuta vitu vya chuma.


Sunday, 20 March 2016

SIMULIZI YA KIMAPENZI YENYE MAFUNDISHO


HADITHI FUPI.
************
“NITAKUBEBA KILA ASUBUHI MKE WANGU MPAKA KIFO KITAKAPO TUTENGANISHA”.
*************
MTUNZI: ELIA MWAIPOPO & SHUFAA.
************
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu.
Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu . Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini ?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike . Akatupa kijiko na akanikaripia , ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu . Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Husna. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Husna. Kwa kweli nilimdharau mke wangu !Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa , niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu .
Nilimuonea huruma kwa muda , rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Husna aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu , jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu .Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miezi kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi .Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani . Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka . Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika . Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika . Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mtoto wetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu . Hili halikuwa tatizo kwangu , nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada , aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku ya harusi yetu . Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa . Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu .Nilimsimulia Husna kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu . Husna alicheka sana , aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Husna tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki . Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana . Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja . Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni , halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu . Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka . Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba . Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote . Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake . Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana . Nikagundua hakuwa binti tena . Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe ! Ndoa yetu imekula urembo wake . Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi . Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea . Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa . Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya . Sikumwambia Husna kuhusu jambo hili . Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi . Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi .Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi . Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa . Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana , nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi . Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake . Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake . Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu . Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho . Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani , sebuleni halafu mpaka mlangoni . Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo . Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka .Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja . Mtoto wetu alishakwenda shuleni . Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo . Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango . Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Husna alifungua mlango nikamwambia, ‘ Samahan husna, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu , halafu akagusa kichwa changu . Akaniuliza ‘Unaumwa ?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Husna, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu . Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu , mimi na mke wangu , si kwamba hatupendani . Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu , nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenga
nisha.’ Ikawa kama Husna alizinduka usingizini . Akanizaba kibao cha nguvu , akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia . Nikashuka ngazi na kuondoka zangu . Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu . Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi . Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu , tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani , nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani . Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Husna sikuwa na muda wa kukaa na kujadili maisha wala matatizo ya mke wangu .
Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mtoto wetu kama ningelazimisha talaka mapema . Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….................Mungu amuweke mahala pema peponi mke wangu . Nitamkumbuka daima .
MWISHO****
KUMBUKA
SHARE, COMMENT & LIKE

Friday, 18 March 2016

MASKINI MTOTO HUYU AZALIWA BILA PUA!!!!


Tukio hili la mtoto anaezaliwa bila kuwa na pua huyokea mara chache sana ambapo kati ya watoto milioni 197 basi humkumba mtoto mmoja.Je mtoto huyo anaishi vipi?

Mtoto huyo Eli,alizaliwa katika eneo la Alabama nchini Marekani mnamo tarehe 4 mwezi wa tatu.Mara baada ya madaktari kumkabidhi mtoto huyo mama,mara moja mama yake aitwae Brand MvGlathery aligundua kuwa mwanae amezaliwa bila kuwa na pua.Aliamua kumpeleka katika hospitali ya 'USA Children's and women's Hospital in mobile' iliyoko pale pale Alabama ili kuona wataalamu wanaoweza kumsaidia mwan
ae. Aliweza kupumua bila shida baada ya kutoka hospitalini pale.

Mama yake amekuwa karibu sana na madaktari kuhakikisha kuwa anapata maelezo sahihi ya namna ya kumtunza vema mtoto huyo.
Tukio kama hili liliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1931 na linajulikana kitaalamu kama *Congenital Arhinia*

Inaweza kuwa ni ngumu kuishi kwa hali hii kuelekea utu uzima lakini kuna watoto wameweza kukua wakiwa na hali hii hadi kuwa watu wazima.Mama wa mtoto huyo amekuwa karibu sana na wazazi wa watoto wengine waliozaliwa bila pua na kuweza kukua vema hadi ukubwani licha ya kupata changamoto ya mfumo wa upumuaji.Mama huyo anasema hii imemsaidia sana kuweza kupata taarifa muhimu pia ya namna ya kumlea mtoto wake.

Yuko sawa kwa hali aliyonayo.Pia kunabnjia mbafala ya kumfanyia upasuaji ili kumwekea umbo la pua yaani pua bandia kwa hiyo mama yake analitumainia hilo.Mama yake anasubiri aje aamue mqenyewe ukubwani kama anahitaji pua bandia ama la.
     
           "Hadi pale atakapohitaji pua bandia,sisi hatutafanya lolote lile,tutasubiri uamuzi wake pale atakapoweza kuwa na maamuzi yake mwenyewe"

Alimalizia mama wa mtoto huyo.


Kama umeoendezwa nayo waweza share
Karibu tena kwenye ukurasa huu.

Wednesday, 16 March 2016

MWANAMKE MIAKA 62 AOLEWA NA KIJANA WA MIAKA 9!!!!!


Mvulana mwenye umri wa miaka 9 anaejulikana kama Saneie Masilela amekuwa mume mdogo zaidi duniani baada ya kumwoa mwanamke mwenye umri wa miaka 62 ambaye alimchumbia tangu mwaka jana.

Akiwa ndani ya suti yake ya kupendeza mvulana huyo mdogo aliunyanyua mkono wa Bi kizee huyo ambae ni mchumba wake,Helen Shabangu mwenye watoto  watano  na kvisha pete ya ndoa.Watoto wa mama huyo wana umri kati ya miaka 28 na 35.
Mvulana huyo alisema kuwa aliamua kumuoa kabisa baada ya uchumba ili iwe rasmi lakini majirani zake wa vijiji vya Ximhungwe eneo la Mpulanga wanaona kama ni uchizi.
Sherehe ya harusi hiyo ilifanyika mbele ya mume qa zamani wa mwanamke huyo,Alfred Shabangu ,66,ambae pia alihudhuria sherehe za uchumba wao mwaka uliopita.

"Watoto wangu wana furaha sna na ndoa hiina hawana matatizo kwa mimi kuolewa na mvulana huyu mdogo,pia sijali watu wanasema nini juu ya hili."Alisema mwanamama huyo.

Mume huyo mdogo duniani alisema
         "Nilimwambia mama yangu kuwa nahitaji kuoa na kiukweli nilikuwa nahitaji sana.Nina furaha  kumuoa Helen,nampenda lakini nitahakikisha narudi shule na kusoma kwa bidii.Nitakapokuwa mkubwa nitaoa mwanamke wa umri wangu.Nimechagua yeye kwa kuwa sikai nae muda mwingi,huwa nakutana nae eneo ambalo mama yangu anafanyia kazi.“

Mama wa kijana huyo nae alikuwa na ya kuongezea
          "Mwanangu Sanele alikuwa nsawanna mwenye furaha kwa sababu aliitaka ndoa hii na hakuwa na aibu hata kidogo.Alifurahi sana kiasi kwamba alihitaji tena kusherehekea.Wati wengi waliniuliza je wataishi pamoja?Watalala pamoja?Je watapata watoto pamoja?Niliwajibu kuwa baada ya ndoa kila kitu kitakwenda kama kawaida,hakunabkinachobadilika."

Je mnakubaliana na ndoa hii ya ajabu??????

Share tafadhari kama umeipenda.

Asante kwa kuingia ukurasa huu karibu sana kwa habari tamu tamu.

         

Thursday, 25 February 2016

WASIRA AMSHUSHIA KICHAPO MWANDISHI WA HABARI


ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika Serikali ya awamu ya nne, Steven Wasira, jana nusura atembeze mkong’oto mahakamani.
Wasira alijikuta jaribio lake la kutaka kumpiga na kumnyang’anya kamera mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Michal Jamson likikwama baada ya kushindwa kumkamata.
Tukio hilo la aina yake lililovuta hisia za watu wengi waliokuwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lilitokea jana saa 5 asubuhi wakati Wasira alipotoka ndani ya mahakama hiyo baada ya ombi la wapigakura wake watatu kupewa ruhusa ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kutupwa.
Baada ya kutoka ndani ya mahakama hiyo, Wasira aliye maarufu kwa jina la utani la ‘Tyson’, alikutana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa nje wanamsubiri ambapo alizungumza nao.
Lakini baada ya mpigapicha huyo kufika na kuanza kutekeleza majukumu yake, Wasira alionekana kukereka na kutaka kumkamata kwa lengo la kutaka kumpora kamera.

HALI ILIVYOKUWA
Dalili za Wasira kumsaka mpigapicha wa Mwananchi zilianza kuonekana eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza saa 3:29 asubuhi kabla ya kuelekea jengo la Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.
Baada ya kubaini uwepo wa mpigapicha huyo, alimfuata na kumhoji ni chombo gani anachofanyia kazi au anatoka mtandao gani wa kijamii, ambapo alimjibu kuwa ni mpigapicha wa gazeti la Mwananchi.
Hatua hiyo ilimfanya Wasira atafakari kwa muda kabla ya kuamua kuingia ndani ya jengo la Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa kesi ya wananchi watatu waliomba kukata rufaa ya kupinga ubunge wa Bulaya.
Baada ya dakika 25 kupita, mahakama ilitoa uamuzi kuhusu maombi ya wapigakura hao, lakini Wasira alibaki ndani kwa dakika kadhaa, na kutuma wapambe wake kuangalia kama waandishi wa habari wameondoka eneo hilo.
Baadaye Wasira alitoka nje na wapigapicha wakaanza kutekeleza majukumu yao kitendo kilichosababisha arudi ndani.
Akiwa ndani hakukaa muda mrefu, akatoka tena nje, na moja kwa moja akamfuta Jamson, huku akihoji sababu za yeye kupigwa picha.
“We kijana njoo hapa usikimbie, unafanya nini hapa muda wote? Nimekuona muda mrefu unanifuatilia,” alisema Wasira huku akimsogelea kutaka kumkamata na kumnyang’anya kamera yake.
Mpigapicha huyo alipohisi hatari, aliamua kukimbia na Wasira alijaribu kumkimbiza bila mafanikio.
Baada ya kushindwa jaribio hilo, Wasira ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, aliamua kwenda katika gari lake dogo aina Toyota Mark X lenye namba za usajili T 399 DBG.
Alipanda ndani ya gari hilo pamoja na mmoja wa wapigakura wake waliofungua kesi ya kupinga ubunge wa Bulaya, aliyetambulika kwa jina la Janes Ezekiel.
Hatua hiyo iliwafanya wanahabari waliokuwa nje ya jengo la mahakama kupigwa na butwaa na ghafla waliona gari la Wasira likibadili mwelekeo na kuelekea kwa kasi eneo walipokuwa wamesimama.
Hali hiyo ilisababisha waandishi wa habari kukimbia ili kukwepa gari hilo lisiwagonge.
KAULI YA WASIRA
MTANZANIA lilipomtafuta Wasira kwa njia ya simu ili kujua sababu ya uamuzi wake wa kutaka kumpiga mpigapicha huyo, alisema kuwa alitaka kujua sababu za kumfuatilia kila eneo na hata kumpiga picha alipotoka msalani.
“Nashangaa hapakuwa na waandishi ila yeye tu,” alisema Wasira huku akimtaka mwandishi aliyempigia simu aonane naye ana kwa ana na kisha kukata simu.

RUFAA YATUPWA

Awali kabla ya tukio hilo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi kuhusu maombi ya kukata rufaa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa wapigakura wa Jimbo la Bunda ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila waliokuwa wakiwakilishwa na mawakili Denis Kahangwa na Costantine Mtalemwa dhidi Mbunge Bulaya, Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma uamuzi huo wa Jaji Sirilius Matupa, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Eugenea Rujwahukwa, alisema baada ya kutolewa uamuzi wa kutupiliwa mbali kesi hiyo Januari 25, mwaka huu, wapigakura hao hawakuridhishwa, hivyo kuwasilisha tena maombi ya kwenda Mahakama ya Rufaa.

Alisema katika maombi hayo, mawakili wa wapigakura, Mtalemwa na Kahangwa waliomba kufungua shauri Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili itoe ufafanuzi kuhusu haki ya mpigakura ya kuhoji matokeo na ni vigezo gani vinatakiwa vitimizwe ili mpigakura aweze kuhoji matokeo ya uchaguzi.

Rujwahukwa alisema katika hatua za usikilizwaji wa maombi hayo, wakili wa Serikali, Kidando, alileta pingamizi kuwa maombi hayo hayaendani na sura ya 141 sheria ya rufaa kifungu 15(2) na 1(2) ambapo licha ya mabishano hayo Jaji Matupa alikubaliana na sura hiyo.

“Jaji amekubaliana na sura 141 ya sheria ya rufaa na maombi haya ni ya msingi chini ya kifungu 15(a)(b), lakini yalipaswa kuwa chini ya  kifungu 15(c) ambacho ndiyo sahihi kwa ajili ya maombi kama haya, hivyo mahakama imeyatupilia mbali maombi haya ya rufaa kwa ajili ya uimarishaji wa haki na kwamba bado wanayo nafasi ya kuleta maombi mengine ndani ya muda wakizingatia vifungu hivyo vya sheria,” alisema Rujwahukwa.

Januari 25, mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mohamed Gwae, aliitupilia mbali kesi namba moja ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Bunda Mjini iliyofunguliwa na wapigakura hao kwa sababu waleta maombi hakuwa na mamlaka kisheria.


MWAKA 1998

Mwaka 1998, Wasira alidaiwa kumpiga Mhariri Mkuu wa gazeti la Hoja, Sadick Yassin nje ya Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), baada ya gazeti hilo kuandika kichwa cha habari ‘Swahiba wa Mrema aanzisha chama kuiondoa CCM madarakani’.

Wasira hakufurahishwa na neno ‘swahiba’ kwa madai kuwa ni tusi, wakati huo akiwa mwanzilishi wa chama cha upinzani cha National Development Congress (NDC) ambapo alikuwa mwenyekiti.

Katika tukio hilo, Wasira anadaiwa alimpiga ngumi mhariri huyo kisha kumkimbiza hadi ndani ya ofisi za Serikali, huku waandishi wakongwe Raphael Hokororo na Mayage S. Mayage wakishuhudia tukio hilo.

Baada ya tukio hilo, Wasira alijisalimisha Kituo cha Polisi cha Kati kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambako alihojiwa kutwa nzima.

Baada ya mahojiano kukamilika, siku iliyofuata alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi yake iliendeshwa kisha kufutwa baada ya walalamikaji kutohudhuria mahakamani.

Source:mtanzania.