Saturday 26 March 2016

IJUE HISTORIA YA PASAKA NA MAANA YAKE...



Pasaka ni jina la sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo . Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania " פסח " (tamka: pasakh).
Pasaka ya Kiyahudi ni sikukuu ya kumbukumbu kwa kutoka kwa Wanaisraeli kutoka Misri wakati wa Musa mnamo miaka 1200 KK.

Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulibiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.
Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kifo na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo imeendelea kutumikwa kwa ajili ya sherehe ya kikristo.
Tarehe ya Pasaka

Pasaka ni sikukuu inayobadilika tarehe yake katika kalenda ya kawaida kila mwaka.
Pasaka ya Kiyahudi inafuata kalenda ya Kiyahudi ni tarehe 15 Nisan ambayo ni siku baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya sikusare ya machipuko (mnamo 21 Machi).
Pasaka ya Kikristo inaunganisha siku ya Jumapili (ni jumapili kila mwaka kwa sababu hii ni siku ya ufufuo katika mapokeo ya kikristo) pamoja na kumbukumbu ya pasaka ya Kiyahudi. Tangu mtaguso wa Nikea Wakristo walipatana kusheherekea Pasaka kwenye
jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu unaotokea baada ya sikusare ya 21 Machi. Kwa hiyo

Pasaka inaweza kutokea kati ya 22 Machi hadi 25 Aprili.
Tangu masahihisho ya kalenda ya Juliasi na kuanzishwa kwa kalenda ya Gregori mara nyingi kuna tofauti kati ya Pasaka ya kimagharibi (kanisa katoliki na makanisa ya kiprotestanti) na Pasaka ya Kimashariki ya makanisa ya Kiorthodoksi kwa sababu Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda ya Juliasi kwa ajili ya kukadiria sikukuu zao.

Majina ya Pasaka ya Kiyahudi na Pasaka ya Kikristo katika lugha mbalimbali
Katika lugha nyingi asili hii bado inaonekana ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa umbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

No comments:

Post a Comment