Sunday 14 February 2016

Faida za kila tunda mwilini

Fahamu faida za matunda haya kwa ubora wa afya yako. Kuna faida nyingi za kula
matunda licha ya kupenda ladha tamu za matunda tunayokula. Matunda yana virutubisho vingi ikiwa vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda mengine. Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart diseases ), stroke ( kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol, aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi. Matunda yote yana manufaa kwa miili yetu lakini napenda ujue haya machache kuhusu faida za apple, parachichi, ndizi, zabibu, embe, chungwa, papai na nanasi. Matunda haya niliyoyataja huwa tumezoea kuyala lakini naamini wengi wetu hatujui sana kuhusu ni vitu gani tunanufaika kutokana na kula matunda haya. Zijue faida za matunda..... APPLE. -Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma ) -Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher ) vilevile apple husafisha meno kila unapotafuna. Je Unajua? Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu. PARACHICHI. -Ni chanzo cha vitamin E. -Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini. -Kwa afya njema ya moyo wako, kwenye sandwich au mkate tumia parachichi badala ya siagi. Je Unajua? Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa kwa mtoto na kuwa mwenye afya bora. NDIZI. -Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium. -Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu ( blood pressure ). Je Unajua? Watu wenye aleji na material ya mpira( rubber latex ) wanaweza pia kuathirika kwa aleji ya ndizi kwakuwa mpira na ndizi vyote zina aina moja ya protini. ZABIBU. -Ni chanzo cha madini ya manganese. -Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure ) -Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach cancer ) na utumbo ( colon cancer ). Je Unajua? Unaweza gandisha zabibu za kijani na nyekundu na ukazitumia kama barafu ( ice cubes ) kwenye kinywaji chako upendacho. EMBE. -Ni chanzo cha vitamin A na E. -Vitamin A iliyopo kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho yao. Je Unajua? Embe ni tamu sana likiwa limeiva lakini pia likiwa bichi unaweza kutumia embe kutengenezea kachumbari, achali, chutney na salad. CHUNGWA. -Ni chanzo cha vitamin C na madini ya potassium. -Chungwa lina vitamin inayojulikana kama ‘’folate’’ ( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito. -Chungwa lina kemikali zinazojulikana kama ‘’hesperidin’’ ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol kwenye damu. Je Unajua? Sehemu nyeupe ya chungwa ( gome lililo ndani ya chungwa ) lina thamani ya vitamin karibia sawa na nyama ya chungwa hivyo ni vyema kula chungwa lote baada ya kumenya maganda yake. PAPAI. -Ni chanzo cha vitamin A na C. -Papai lina enzyme ijulikanayo kama ‘’papain’’ ambayo husaidia katika kusaga au mmeng’enyeko wa chakula. -Pia vitamin A iliyopo kwanye papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako. Je Unajua? Mbegu nyeusi za papai zinaweza kuliwa japo kuwa ni chungu lakini unaweza kuzisaga na salad kwa kutumia blender badala ya pili. NANASI. -Nanasi lina enzyme asilia ijulikanayo kama ‘’bromelain’’ ambayo husaidia kuvunjavunja protini hivyo husaidia katika mmeng’enyeko wa chakula. -Vilevile enzyme ya bromelain husaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda kwa haraka. Kwa hayo machache hapo juu unaona ni jinsi gani matunda yalivyo muhimu kwa kujenga afya zetu na kutumika kama dama kwa miili yetu. Napendekeza upende kula angalau tunda moja kwa siku . Kiafya unatakiwa ule matunda aina tano kwa siku kupata faida zake zote mwilini. Faida za matunda hazihesabaki. Na hayatakiwi yaliwe pamoja na chakula- bali kabla- AU KATI KATI YA MILO MIKUBWA au baadaye. Tabia yetu wengi kuchanganya matunda na milo mikubwa kama wali, ugali, chapati na kadhalika – hausaidii – ni afadhali hata usile kabisa. UNAJUA KWA NINI NAKUSHAURI HIVI? -Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda lakini sio wote wanakula inavyotakiwa chakula kuwa tiba badala yake tunafanya chakula kilete athari katika miili yetu. Tatizo ni kwamba mipangilio ya milo yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti kabisa kutokana na aina ya chakula ulichokula. Mathalan vile vimeng'enya vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk. 1. MATUNDA YENYE MBEGU Matunda yote yenye mbegu dani (Berries) kama Cranberries, Blue Berries, Blackberries- siku hizi hupatikana katika juisi zinazotengenezwa bila sukari nyingi. Nadhani tatizo kubwa la nchi Afrika ni kutengeneza juisi za matunda zilizojaa maji na sukari zaidi kuliko matunda. Huu ni udanganyifu na uroho wa wafanyabiashara wetu. Shirikisho la Ulaya limekuwa makini miaka ya karibuni kuzuia tabia hiyo Uzunguni na kuweka mikakati mikali. Strawberries Stroberi (Strawberry) – tunda linalopatikana zadi Uzunguni- ambalo lina Vitamin C kwa wingi. NI MATUNDA MAZURI SANA KWA WALE WANAOPENDA KUONDOA MARADHI MBALI MBALI NA KUBORESHA KINGA YA MWILI. Tutaanza kuchambua matunda haya moja baada ya nyingine 2. MATUNDA YA CHACHU Ni muhimu kuzingatia kwamba matunda yanatakiwa kuliwa yakiwa katika kitengo kimoja- yaani chachu (“acid”), asidi au alkali (“alkaline”). Matunda hayo ya chachu ni maembe, mananasi, machungwa, zabibu, Kiwi, nk; . Matunda chachu (“asidi”) yanatakiwa yaliwe pamoja sio vizuri kuyachanganya na aina nyingine ya matunda katiks mlo wako maana mfumo wa kunyambua chakula mwilini hutaweza kufanya kazi kwa ufasaha. FAIDA CHACHE YA MATUNDA YENYE CHACHU Faida zake ni zifuatazo. 1. Kinga maradhi na kinga magonjwa (Anti-Oxidant) ambazo husaidia kukinga na kupambana na takataka zinazotolewa na mwili au zinazotoka katika mazingira machafu. 2. Vitamin C. Vitamin hii ni muhimu sana mwilini. Ukosefu wa Vitamin C husababisha uchovu, kukosa usingizi, uvivu, kutokuwa na hamu ya kula. Kwa siku mtu mzima unatakiwa upate gramu 40 za Vitamin C. Kwa wavuta sigara zidisha mara mbili. Ukila matunda yenye Vitamin C unapata kinga ya majeraha mwilini (vidonda Kupona haraka), huboresha wajihi, haiba na “nafsi” ya ngozi, mifupa, meno na mzunguko mzima wa damu mwilini- hivyo kusaidia usingizi ( na kwa watoto kusaidia kukua vizuri). 3. MATUNDA YA ALKALI (YENYE KUPUKUCHIKA) Mapapai na Maparachichi yanaangukia katika mkondo wa “alkali” na moja ya matunda yaliyowekwa katika Vyakula Vyenye Nguvu kuliko vyote (Superfoods) . Matunda hayo ni , Matikiti maji,ndizi mbivu, tufaha,mapea, Papai, Parachichi. Vyakula hivi vina faida sana mwilini. Mfano wa matunda yenye “alkali” yanayotakiwa kuliwa pamoja. BAADHI YA FAIDA YA MATUNDA YA ALKALI 1. Papai lina “papain” inayosaidia kuukinga mwili na kulainisha tumbo- ndiyo maana kama umevimbiwa au huendi haja kubwa sawasawa (“constipation”) ukila papai husaidia sana. 2. Mapapai na Maparachichi yana “Beta Carotene”(itokanayo na Vitamin A) inayopatikana pia katika nyanya, karote, maembe, mchicha (ambao haukupikwa hadi ukanyong’onyea), Faida zake ni pamoja na kusaidia mizunguko ya umajimaji na damu mwilini, ngozi na nywele (safi sana kwa kina dada wanaojipenda), kupunguza mafuta katika damu (cholestoral) na “presha” – mambo yanayoua sana watu weusi duniani leo. Ukiwa upungufu wa “Beta Karotene” macho hayaoni vizuri, unaugua upesi upesi hasa maradhi ya mapafu (mafua, kikohozi,nk). Kwa wanawake waja wazito ni rahisi kupoteza watoto au kuzaa watoto ambao hawako sawasawa. 3. Maparachichi yanayo mafuta asilia. Mafuta haya ni mazuri SANA kuliko yale tunayoyapata katika nyama au vitu vilivyokaangwa, maana yanausaidia na haya haribu mwili. Makisio yake ni kalori 400 kwa parachichi moja. Hiyo ni nguvu kubwa sana. Ndiyo maana Parachichi (na Papai) huhesabiwa kama mfalme wa matunda. Papai na Parachichi -nje Lazima izingatiwe kuwa chakula, mmea au tunda lolote lenye rangi nzito iliyokolea kama parachichi huwa na faida MARIDHAWA mwilini. Hivyo, kuanzia leo kama hukua ukithamini matunda haya mawili- kayatafute. Kuna watu wazima wanaosema eti matunda ni chakula cha watoto. Wanakosea. Mtu mzima anahitaji kuendelea kuukarabati mwili wake. Source:mitandao ya kitabibu

No comments:

Post a Comment