Monday 29 February 2016

ZIJUE FAIDA ZA KUTUMIA TANGAWIZI


Tangawizi ni moja kati ya mizizi ambao ina faida kubwa sana katika miili yetu.Tunashauriwa kutumia tangawizi kwa wingi ili kuweza kuzipata faida hizo.Zifuatazo ni baadhi ya faida za tangawizi mwilini

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA: Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea) . Hali hii ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya ujauzito,kupata harufu mbaya n.k.Kunywa chai ya tangawizi kwa wingi.

HUSAIDIA UFANYAJI MZURI WA KAZI
Hii ni pamoja na kusaidia uyeyushaji mzuri wa chakula na pia husaidia ufyonzaji wa chakula na virutubisho vyake.

INASAIDIA MZUNGUKO WA DAMU MWILINI
Ili kuimarisha uzungukaji wa damu mwilini kwa njia ya asili,unashauriwa kutumia kikombe kimoja au zaidi cha tangawizi kila siku.Ni njia inayoaminiwa ya kutumika nyumbani kusaidia matatizo ya mzunguko wa damu mwilini.

INASAIDIA KUTIBU HOMA.
Agenda rahisi hapa ni kuwa tangawizi inasaidia kuleta ujotoridi ambao unasaidia kupambana na matatizo ya kutokwa sana na jasho.Hii inasaidia kulirudisha joto la mwili katika hali ya asili na kutibu homa.

HUSAIDIA MATIBABU YA ATHMA.
Hii inawezekana kwa mapafu kutanuliwa kwa kupunguza 'phlegm' kwa kunywa tangawizi.Hii inasaidia matatizo ya upumuaji mwilini.Pia hupunguza tatizo la mzio kwa watu wa athma.

HULETA MTULIZO WA AKILI
Faida nyingine ya kuwa tangawizi ni kuondoa MSONGO mwilini.kikombe cha tangawizi kinatakiwa kukuongeza nguvu na mtulizo wa akili kuondokana na msongo.

HUIMARISHA MFUMO WA UZAZI
Unywaji wa tangawizi husaidia kuimarisha mbegu za uzazi za kina Baba na pia kuongeza uwezo wa kuzarisha.Pia husaidia uume kusimama vema kwa kina Baba.

HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO
Hii husababishwa na uwezo wa tangawizi kuunguza na kuyeyusha mafuta mwilini.Husaidia mwili kuwa na uzito sawa na pia kupunguza kiasi cha karoli mwilini.Hii ni faida kubwa sana kulingana matatizo yaliyokithiri ya uzito uliopitiliza.

HUSAIDIA MFUMO WA UPUMUAJI MWILINI
Tangawizi ina faidi nyingi sana.Inasaidia sana matatizo katika mfumo wa upumuaji.Kikombe kimoja tu kinaweza kutatua matatizo mengi sana ya mfumo wa upumuaji.Pia husaidia matatizo ya upumuaji yanayotokana na mazingira.

HUSAIDIA KUIMARISHA KINGA YA MWILI
Husiaidia sana kuimarisha mfumo wa asili wa kinga ya mwili.Hii hupelekea mwili kuwa na uwezo mkubwa sana wa kupambana na magojwa vamizi mwilini.

HUSAIDIA KUPUNGUZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI.
Unywaji wa tangawizi husaidia sana kupunguza maumivu wakati wa hedhi.Kama mtu ana matatizo ya hedhi hakikisha anapata walau vikombe viwili vya tangawizi kila siku.
Pia chukua taulo kisha loweka kwenye tangawizi moto na kumkanda chini ya kitovu na kuzunguka tumboni mgonjwa mwenye matatizo ya hedhi.
HUSAIDIA KUPAMBANA NA KANSA
Tangawizi husaidia kupambana na pia kutibu kansa.Husaidia kuzuia kuenea kwa kansa mwilini kwa kiwango kikubwa kuliko madawa ya kisasa.

HUSAIDIA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wengi wametumia tangawizi na kuondokana na harufu mbaya mdomoni nabkufanikiwa.

HULINDA INI
Tangawizi husaidia kuondoa sumu mwilini na hivyo kulisaidia ini  na kulifanya lipunguziwe mzigo na hivyo kuendelea kuwa na afya njema.

HUSAIDIA TUMBO
Hulisaidia tumbo kuwa lenye afya siku zote na kufanya vema kazi zake.

Na Michael Gussa kwa msaada wa mitandao

No comments:

Post a Comment