Tuesday 9 February 2016

KADUMA: JPM AREJESHE NYUMBA ZA SERIKALI Mwanasiasa mkongwe nchini, Ibrahim Kaduma amemshauri Rais John Magufuli kurejesha nyumba za Serikali zilizouzwa kwa watu binafsi wengi wao wakiwa waliokuwa watumishi wa umma, akisema ndiyo njia ya “kujisahihisha”. Kaduma, ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, aliyasema hayo wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na gazeti hili kuhusu mambo kadhaa juu ya mwenendo wa CCM na Serikali yake katika kipindi ambacho chama hicho kimeadhimisha miaka 39 tangu kianzishwe. “Kitu muhimu ambacho namshauri Rais, ni kuzirudisha nyumba za Serikali. Uuzaji wake haukuwafurahisha Watanzania walio wengi. Asimamie urudishaji huo ila afanye hivyo baada ya kutunga sheria ya maadili ya utumishi wa umma,” alisema. Nyumba hizo za Serikali ziliuzwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, chini ya Rais Benjamin Mkapa kwa usimamizi wa Dk Magufuli wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi Source:mwananchi
ğ

No comments:

Post a Comment