Friday 26 February 2016

WATU ISHIRINI WANAOSHANGAZA ZAIDI DUNIANI


Kila mtu ana kitu maalumu ambacho kinaweza kumtofautisha na wengine.Kitu hicho hutofautiana kati ya mtu na mtu.Lakini kuna wengine wana vitu vya ziada ambavyo huwafanya kuwa wa pekee zaidi duniani.Hawa ni baadhi ya watu hao:

MTU MWENYE MDOMO MKUBWA ZAIDI
Francisco Domingo Joaquim ni mtu mwenye kipaji cha kipekee.Yeye anashikilia rekodi ya kuwa na mdomo mkubwa zaidi duniani.Mdomo wake una ukubwa wa '6.69inches' kiasi kwamba ana uwezo wa kumeza soda ya kopo.

MVUMBUZI MAARUFU(DOKTA NAKAMATS)
Raia wa japan Yoshiro Nakamatsu alijulikana kwa kuwa mtu mwenye akili na mvumbuzi hodari zaidi.Huyu anashikilia rekodi ya kuvumbua vitu vingi zaidi.Pia ana sifa ya kupiga picha mlo wake na kuulezea kwa muda wa miaka 40.

MTU ANAEKULA VYUMA
Kwa muda wa miaka 40 raia huyu wa ufaransa Michel Lotito amekula zaidi ya tani 9 za maada(metal)ikiwemo chuma.Akiwa mdogo aliugua ugonjwa wa ukosefu madini mwilini na akaanza kula plastiki.Baadae alianza kula vitu vigumu kama vioo na baadae vyuma.

MWALIMU MZEE WA YOGA.
Mwanamke huyu mwenye miaka 96 Tao Porchon Lynch amekuwa akijifunza mchezo huu zaidi ya miaka 70 sasa.Huwa anaamka alfajiri na kuwafundisha watoto jinsi ya kujinyoosha mwili,kujipiga na mapozi mengine magumu ya mchezo huu wa Yoga.

MALKIA WA CHUMA
Asha Rani amejitambulisha kwa kuwa na rekodi mbili za kushangaza kwa kunyanyua mizigo mizito kwa kutumia nywele zake pamoja na maskio yake.Akiwa na miaka 23 amepewa jina la 'Iron Queen' kutokana nabuwezo na nguvu zake.

RUBANI MZEE ZAIDI
Kutokana na rekodi za Guinness za dunia,Peter Weber Jr. ndie rubani aliekuwa mzee zaidi wakati akiwa kazini.Akiwa na miaka 95 yeye hurusha ndege mara mbili kwa mwezi na amefanya kazi kwa muda wa maika 72.

MTU MWENYE KIUNO CHEMBAMBA ZAIDI
Mwanamke mwenye umri wa miaka 26 Michele Kobke amekibana kiuno chake hadi kufikia inchi 25 kwa kuvaa mkanda kwa muda wa miaka 3.Anatarajia kukipunguza hadi kufikia inchi 14.

MWANAMKE MWENYE UWEZO WA KUKUMBUKA KILA KITU
Jill Price anasema anauwezo wa kukumbuka kila kitu tangu akiwa katika umri wa tineja.Ana kumbukumbu ya watu aliokutana nao wote na ni muda gani huamka.Kila kumbukumbu ya kila siku huihifadhi kwenye ubongo wake.

MWANAMME MZEE KUPANDA MLIMA EVEREST
Mwaka 2013,akiwa na miaka 80,Yuishiro Miura  alikuwa mtu mzee zaidi kufika kileleni mwa mlima mrefu zaidi duniani.Miura alianza kuwa maarufu mwaka 1970 baada ya kuwa mtu wa kwanza kuruka chini akitokea juu ya mlima Everest.

MWANAUME AMBAE DAIMA HUNYANYUA MKONO WAKE JUU
Mwaka 1973,Sadhu Amar alinyanyua mkono wake kumuheshimu mungu wa kihundu Shiva na kama hakuushusha tena.Watu wengi miongoni mwa wafuasi wake nao hawashusha mkono wao miongo kadhaa sasa.

MTU MWENYE OPARESHENI NYINGI ZAIDI DUNIANI
Eileen Brown kutoka England amefanyiwa oparesheni nyingi sana miaka 20 iliyopita kiasi kwamba sehemu ambazo bado zina uhalisia katika mwili wake ni hipsi ya kushoto na kiwiko cha kushoto.

MZEE ZAIDI KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE NDEGE NA KUELEA ANGANI
Georgina Harwood akiwa na umri wa miaka 100,alifurahia kujirusha na kuelea angani(SKYDIVING) nchini South Africa.Hii ilikuwa mara yake ya tatu ambapo mara kwanza alikuwa na miaka 92.

MWANAMKE ANAEJIPINDA ZAIDI DUNIANI
Julia Gunthel ambae ni mrusi,ambae pia anajulikana kwa jina la Zlata,ndie mwanamke anaweza kujipinda zaidi duniani.Kwa sasa anaishi na kufanya kazi Ujerumani na kwa sasa ameingia kwenye vitabu vya Guinness.

MTU ALIEFANYA KAZI MUDA MREFU ZAIDI
DUNIANI
Mtu aliefanya kazi moja kwa muda mrefu zaidi duniani ni Bibie Polly Gadsby akiwa na kampuni ya Archibald Turner & Co. iliyoko Leicester UK,akiwa na miaka 9.Ameifanya kazi hii kwa miaka 85 na katika umri wa miaka 95 bado anaendelea na kazi yake.

MCHEZA POLE MZEE ZAIDI
Huyu hufanya mazoezi ya POLE dancing akiwa na miaka 60,mjini Nanjing nchini China.Sun Fengqin alianza kucheza mwaka 2012 na kuwa mtu maarufu nchini China.

MTU MWENYE MUSTACHI MREFU ZAIDI DUNIANI
Huyu ameanza kufuga mustachi huu kwa muda mrefu zaidi hadi kuwa mrefu kiasi hiki.Yeye hutumia saa moja na nusu kila siku kuuchana mustachi huo.

MAPAFU  YENYE NGUVU ZAIDI
Manjit Singh,ndie anaeshikilia rekodi ya kuwa mtu mwenye mapafu yenye nguvu zaidi duniani.Alitumia mapafu yake kujaza ballon lenye kipenyo cha mita 2.5 kwa muda dakika 42.

MACHO YA X-RAY
Natasha Demkina raia wa Urusi anasema kuwa yeye ana macho yanayoona kama X-RAY  yanayomwezesha kuona ndani ya miili ya watu na kufanya uchunguzi wa kina kwa watu kuliko hata madakiktari bingwa wanaweza fanya.Hii imepelekea kufuatwa na waandishi wa habari,madaktari na watu wanaouamini uwezo wao.

MWANAMKE MWENYE PEMBE KICHWANI
Pembe hiyo inayojulikana kama DEVIL HORN
anayo mwanamke anaejulikana kama Zhang Ruifang.Pembe hiyo ilijulikana mwaka 2010.

MTU MWENYE MISULI ZAIDI
Anaitwa Romario Dos Santos Alves,ambae ni mjenga misuli wa kibrazil.Huyu aliamua kujifananisha na yule INCREDIBLE HULK wa filamu na kuamua kujidunga madawa na pombe pamoja na oil mishipani mwake.









No comments:

Post a Comment