Saturday 13 February 2016

UMUHIMU NA NAMNA YA KUPATA CHETI CHA KUZALIWA,NDOA NA HATA URITHI.


Kutokana na umuhimu wa kiwa na cheti cha kuzaliwa au cha ndoa nimeona si vibaya kama tukapeana habari namna ya kuvipata kwa wasio navyo au kukumbushana umuhimu wake pia....
Mimi ni Mtanzania niliyezaliwa ng’ambo; ninaweza kupata cheti cha kuzaliwa kutoka ofisini kwako?
Mtanzania aliyezaliwa ng’ambo hawezi kupata cheti cha kuzaliwa Tanzania bara. Sheria inayoongoza usajili wa vizazi na vifo hairuhusu kusajili matukio ya vizazi vilivyotokea

Mimi ni Mtanzania ninayeishi ng’ambo. Nilifunga ndoa kule. Ninaweza kuisajili ndoa hii Tanzania?
Ndiyo unaweza kuisajili ndoa hii kwa kuomba kwa msajili mkuu (ofisi za RITA).
Jaza fomu ya RGMF 7 na 48.
Ambatisha nakala ya Kiingereza au Kiswahili ya cheti chako cha ndoa (iwapo cheti chako cha ndoa hakiko katika Kiingereza au Kiswahili cheti

Kulingana na sheria kizazi kinatakiwa kuandikishwa ndani ya siku 90 tangu kutokea kwake na kifo ndani ya siku 30 na tukio hilo lazima liwe limetokea ndani ya mipaka ya Tanzania Bara. Pamoja na takwa hili sheria inaruhusu usajili kufanyika nje ya muda huu.
Je umeshasajili kupata cheti chako?

Neno la asubuhi:
"Utakutana na majaribu mengi katika maisha yako lakini hata siku moja usikubali majaribu yakakushinda.

Cheti cha Kuzaliwa nini?
Ni nyaraka ya muhimu kwa kila mwananchi kwani hutumika kupata huduma nyingine za msingi katika maisha ikiwa pamoja na elimu, afya,makazi, nk.
Je chako umechukulia wilaya gani?
Kwa wilaya ya Arusha, kampeni ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa unaanza tarehe 8/2/2016. Mtu yeyote aliyezaliwa katika ardhi ya Tanzania anaruhusiwa kujisajili huko.

WILAYA YA ARUSHA: KAMPENI YA USAJILI NA KUTOA VYETI
Wapi vinapatikana Vyeti vya Kuzaliwa?
• Ofisi zote za Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara
• Makao Makuu ya RITA (Mtaa wa Makunganya, Dar es Salaam)

WILAYA YA ARUSHA: KAMPENI YA USAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KUANZA KARIBUNI...

JAJI MKUU WA TANZANIA, MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN ATEMBELEA BANDA LA RITA, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA:
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman atembelea Banda la RITA Viwanja vya Mnazi Mmoja katika… More

Mtoto wa nje ya ndoa ni yupi?
Aliyezaliwa kabla ya baba na mama hawajaoana, alizaliwa bila ndoa na baadaye mzazi mmoja akaoa ama kuolewa kwingine, aliyezaliwa wakati ndoa iko hai kwa baba ama mwanamke mwingine.
Sheria inasemaje?
Mtoto ana haki sawa haijalishi amepatikana kwa mazingira yapi. Yapo masharti ya Sheria za nchi na za Kimila kuhusu… More


Kamwe usitumie mawakala, watakulia pesa yako bure na waweza kukupa cheti cha bandia. Fika RITA sasa!


Natumai ulikuwa na mapumziko mema ya mwisho wa wiki, Unaianza vipi wiki yako? Tunakutakia kila la kheri katika shughuli zako za siku ya leo.

Kizazi au Kifo kikitokea hospitali au kituo cha Afya
HAKIKISHA mhusika huondoki hospitalini au kituo
cha Afya bila kupatiwa TANGAZO LA KIZAZI kwa
kizazi au KIBALI CHA MAZISHI kwa kifo. Nyaraka
hizi ni muhimu katika uandikishaji na hutolewa
BURE.
Kwa kizazi/kifo kilichotokea nyumbani, wasiliana
na ofisi ya mtendaji wa kijiji au mtaa ili kupatiwa
waraka wowote wa kuthibitisha kutokea kwa Kizazi
au Kifo.





Habari kwa msaada wa RITA .



No comments:

Post a Comment