Thursday 25 February 2016

TAMBUA NAMNA MSTARI KWENYE KIGANJA CHAKO UNAVYOHUSIKA KATIKA MAHUSIANO YAKO NA NDOA YAKO.


Mara nyingi watu huenda kwa wanaosoma viganja ili waweze kuelezewa kuhusu wakati wao ujao yaani utabiri na pia bahati zao.Utaalamu huu wa usomaji viganja mara nyingi sana umetumika na huwa kweli kwa asilimia kubwa hasa linapokuja suala la mapenzi na maisha.
Sitakuchosha saaana ila cha kufanya unganisha viganja vyako hapo ulipo.Ile sehemu unakoshikia chakula iwe juu.Mara baada ya kuviunganisha vema hakikisha mistari ya vidole inaendana vema.Baada ya hapo itizame kwa makini mistari mikubwa inayofuatia ilioko chini kabisa baada ya mstari wa mwisho wa kidole kidogo.
Tazama hapa chini kujua matokeo yake:

1)MISTARI INA UREFU SAWA.
Hii inaanisha kuwa mchumba wako atakubaliwa na kupendwa na wengi.Wengi watamfurahia na kumwona mke mzuri na mwema.Pia mtu huyu huwa mkuu,mwenye kujiamini ana asiependa shitukizo.



2)MSTARI WA MKONO WA KULIA UKIWA JUU
Hii inaonesha kuwa inakupasa uwe makini sana na uamuzi wowote ule utako ufanya katika maisha yako.Usikurupuke inapaswa uwe mtulivu sana.
Pia mtu wa aina hii hupendelewa zaidi na wakubwa,pia ana uwezekano wa kuoa au kuolewa na mtu alemzidi umri,mwenye uwezo wa kutambua watu wanaomzunguka,hali iliyopo na asiejali watu wanafikiri nini juu yake.


3)MSTARI WA MKONO WA KUSHOTO UKIWA JUU ZAIDI
Hii inamaanisha kuwa wewe ni mtu jasiri na anaethubutu kukabiliana na changamoto za kimapenzi.Pia hupendelea zaidi vitu visivyo na uhusiano na mahusiano yako.Huyu pia huweza kuoa au kuolewa na mwanafunzi au mgeni wa ng'ambo.Mara nyingi hawa ni watanashati na warembo.


Msimulizi: Rakshita Nagayach

2 comments: