Wednesday 30 March 2016

NI AJABU KWELI!!!JIONEE NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUZIBADILI HISIA ZA KISASI NA KUWA ZA KINDUGU

Pamoja na kuwa na uhasama mkubwa sana kati yao,Babu huyu raia wa afghanistan alikutwa akimpa mwanajeshi huyu wa marekani kikombe cha chai.Hii ni ishara ya UPENDO na kuthamini watu wengine pia.Dada mmoja ambae alikuwa na wenzie katika mashindano ya kukimbia mita 3200 aliamua kusimama na kumsaidia mwenzie aliekuwa ameumia ili kumaliza mbio.Japo walimaliza nafasi ya 14 na 15 lakini wote wawili walipewa tuzo maalumu ya heshima.Japo kulikuwa na vita kali sana inayoendelea,Mwanajeshi huyu muungwana aliamua kumchukua mbwa mmoja ambae alikuwa akiwafuatilia nyuma kwa umbali mrefu sana.Hatimae mwanajeshi huyu alimtoa mbwa huyo sehemu ya mateso na kumfikisha sehemu salama.Wakati wa maandamo yaliyotokea nchini Misri mwaka 2011 watu hawa hapa chini ni WAKRISTU waliokuwa wakiwalinda wenzao WAISLAMU waweze kufanya ibada vema.WAISLAMU pia walifanya vivyo hivyo kwa WAKRISTU.Ni dalili ya utu wema.Baada ya kutokea kwa kimbunga na upepo mkali katika jiji la New York nchini Marekani,sehemu kubwa ya jiji hilo iliharibika sana hasa ile ya nishati kama umeme na miundo mbinu mingine kama barabara.Katika picha wanaonekana watu wakitoa msaada wa kuchajisha simu kwa wale waliokosa huduma ya umeme.Daima tujifunze utu na kusaidia wengine pia.Share kwa wengine kama umeupenda UTU wao.Pia wasamehe na kuwajali adui zako pia.

Tuesday 29 March 2016

JIONEE WATU WENYE UWEZO WA AJABU NA KUSHANGAZA


Je unafahamu kuwa watu wenye nguvu za ajabu kuliko uwezo halisi wa kibinadamu wapo?Ni kweli watu hao wapo na wengine wanaishi hadi sasa.Ni watu ambao wana vitu vya ajabu kama uwezo,nguvu na kuwa imara madhubuti.Wafuatao ni baadhi ya watu hao

1.WIM HOF
Huyu ana uwezo wa kukaa muda  mrefu sana eneo la baridi kali sana bila kupata madhara yoyote yale.Huyu ni mtu halisi anaweza kukaa muda mrefu sana eneo la baridi kali sana.Anazo tuzo 21 za Guinness ikiwemo ya kuoga kwenye maji ya barafu kwa muda mrefu.Huyu anaweza kukaa kilele cha mlima kilimanjaro kifua wazi kwa muda mrefu.

2.KELVIN RICHARDSON
Huyu ana uwezo mkubwa sana wa kuwaelewa wanyama.
Ana uwezo mkubwa sana wa kufanya urafiki hata na wanyama wakali zaidi duniani bila tabu yoyote.Ana uwezo wa kuwa na urafiki na chui,simba na fisi.Huwafanya marafiki na hata kulala nao pia.

3.CLAUDIO PINTO
Huyu anajulikana kama MACHO YA DARUBINI.Ana uwezo wa kuyatanua macho yake kipimo cha 7mm ambapo ni kiasi cha 95% ya mzunguko wa jicho lake.

4.HAROLD WILLIAMS
Anajulikana kama MWALIMU WA LUGHA.Huyu anasifika kwa kuwa na uwezo wa kujua lugha nyingi sana duniani.Je wewe una uwezo wa kujua lugha ngapi katika maisha yako yote?Huyu anafahamu lugha zaidi ya 58 ambazo anaziongea na kuandika bila shida yoyote ile.
Sio peke ake alie na kipaji hiki,pia wapo John Browning,Joseph Caspar na Doktar Carlos do Amaral Freire.

5.TIBETAN MONKS
Wana uwezo wa kuweka sawa JOTO la miili yao kwa kutumia akili au ufahamu wao.Wana uwezo qa kubadili joto la miili yao kwa kutumia akili yao tu.Wamewahi kurekodiwa wakibadili jotoridi lao kufikia kiasi cha nyuzi joto 8 za sentigredi.

6.RATHAKRISHNAN VELU
Anajulikana kuwa na meno ya ajabu yenye nguvu sana maarufu kama 'steel teeth'.Ana uwezo wa kuvuta treni ya mabehewa saba akitumia meno yake kuivuta kwa kutumia kamba ya chuma.Anajulikana pia kwa jina la KING TOOTH.

7.DANIEL BROWNING SMITH
Huyu anajulikana kama 'The rubber boy' ana uwezo wa kujipinda zaidi katika mikao mbali mbali.

8.STEPHEN WILTSHIRE
Ana uwezo mkubwa sana wa kukumbuka.Huyu ana uwezo wa kutazama kitu mara moja tu na kuweza kukichora kwa ufasaha kabisa.Ni maarafu sana kwa kuchora picha za miji mbali mbali kwa kuiangalia mara moja tu.Kama watu wengine hutizama mara kwa mara katika uchoraji huo,yeye hutizama mara moja tu na kuchora sehemu kubwa ya mji husika.

9.JESUS ACEVES
Huyu ni mtu mwenye nywele nyingi zaidi za usoni.Anapatikana katika familia ya kimexico yenye wanafamilia 24 ,huwa anazunguka duniani kuonesha watu muonekano wake huo.

10.DANIEL TAMMET
Ni mtaalamu sana wa mahesabu na hesabu kwa ujumla.Hufanya kwa kutumia akili yake hesabu nzito nzito tena kwa speed ya hali ya juu sana.Pia ana uwezo wa kuongea lugha saba bila shida.

11.GARRY TURNER
Je ngozi yako ina uwezo wa kujivuta kwa kiasi gani?Kutana na jamaa huyu ambae ngozi yake hujivuta kama mpira.Huivuta ngozi yake kwa namna mbali mbali.Hii inatokana ngozi yake kupungua 'Collagen'

12.NOORSYAIDAH
Ni mwanamke wa kiindonesia ambae anasema kuwa mwili wake una tabia ya kuota waya kwa muda usiopungua miaka ishirini sasa.
Waya hizo huwa kiasi cha sentimita 10 hadi 20.

13AL HERPIN
Kqa kawaida baada ya kukaa siku chache bila kulala kabisa mwili HUZIMIA.Lakini kwa mtu huyu AL,hajawahi kabisa kulala katika maisha yake na hivi sasa ana miaka 94.
Wanasayansi wanaamini kuwa inawezekana hali hiyo ilisababishwa na jeraha alilopata mama yake siku chache kabla ya kumzaa.

14.LIEW THOW LIN
Anajulikana kama MAGNETIC MAN,raia huyu wa Malaysia ana uwezo wa ajabu sana amabpo mwili wake una uwezo wa kuvuta vitu vya chuma.


Saturday 26 March 2016

IJUE HISTORIA YA PASAKA NA MAANA YAKE...



Pasaka ni jina la sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo . Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania " פסח " (tamka: pasakh).
Pasaka ya Kiyahudi ni sikukuu ya kumbukumbu kwa kutoka kwa Wanaisraeli kutoka Misri wakati wa Musa mnamo miaka 1200 KK.

Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulibiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.
Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kifo na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo imeendelea kutumikwa kwa ajili ya sherehe ya kikristo.
Tarehe ya Pasaka

Pasaka ni sikukuu inayobadilika tarehe yake katika kalenda ya kawaida kila mwaka.
Pasaka ya Kiyahudi inafuata kalenda ya Kiyahudi ni tarehe 15 Nisan ambayo ni siku baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya sikusare ya machipuko (mnamo 21 Machi).
Pasaka ya Kikristo inaunganisha siku ya Jumapili (ni jumapili kila mwaka kwa sababu hii ni siku ya ufufuo katika mapokeo ya kikristo) pamoja na kumbukumbu ya pasaka ya Kiyahudi. Tangu mtaguso wa Nikea Wakristo walipatana kusheherekea Pasaka kwenye
jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu unaotokea baada ya sikusare ya 21 Machi. Kwa hiyo

Pasaka inaweza kutokea kati ya 22 Machi hadi 25 Aprili.
Tangu masahihisho ya kalenda ya Juliasi na kuanzishwa kwa kalenda ya Gregori mara nyingi kuna tofauti kati ya Pasaka ya kimagharibi (kanisa katoliki na makanisa ya kiprotestanti) na Pasaka ya Kimashariki ya makanisa ya Kiorthodoksi kwa sababu Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda ya Juliasi kwa ajili ya kukadiria sikukuu zao.

Majina ya Pasaka ya Kiyahudi na Pasaka ya Kikristo katika lugha mbalimbali
Katika lugha nyingi asili hii bado inaonekana ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa umbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

Friday 25 March 2016

TUMIA MUDA WAKO KUSOMA KISA HIKI CHA KIMAPENZI CHENYE KUELIMISHA NA MAFUNZO TELE!!!!



1st year
nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo.
Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why
2nd year
Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
3rd year
Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda.
katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Graduation Day
siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it.
kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Miaka michache baadae
Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it.
but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Kwenye Mazishi
Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo'
Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi
I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me!
Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!!
Vunja ukimya

Thursday 24 March 2016

KUTANA NA DOGVINCI,MBWA MAARAFU KWA UCHORAJI


Sio tu binadamu wenye uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu.Hata wanyama wana uwezo wa kufanya mambo mengine tena katika kiwango kikubwa zaidi ya binadamu.

Mbwa anaeitwa Dagger amekuwa mchoraji maarufu sana baada ya kufundishwa na mlezi wake Yvonne.

       "Mara nyingi amekuwa akiniangalia sana wakati nachora hadi akapata hamu ya kujifunza.Baadae akaanza kunisumbua sana na nikamuuliza unataka kuchora?Akaanza kutingisha mkia kama ishara ya kukubali.Nikamwambia sawa"
Alisimulia Yvonne akihojiwa na gazeti la ABC 7New York.

Baada ya kutumia muda kumfundisha mbwa huyo,hivi sasa anaitwa DOGVINCI pale New York kutokana na uchoraji wake wa hali ya juu.

Michoro ya mbwa huyo inauzwa kati ya dola $20 hadi $200 za kimarekani kwa mchoro mmoaja.Faida kubwa inayopatikana inapelekwa kwenye organization ya "Canine Companions for Independence".
Ama kweli haya ni maajabu!!!!!Jionee picha zaidi


Wednesday 23 March 2016

YAJUE MADHARA YA KUVAA NGUO PENDWA ZA KUBANA SANA MWILI!!!


Mbali na ukweli kwamba baadhi ya mitindo ya mavazi inasababisha adha kubwa kwa watumiaji, mitindo mingine husababisha atharimbaya kwa afya kwa watumiaji na jamii kwa ujumla.Miongoni mwa mitindo ya mavazi inayosababisha athari mbaya za kiafya ni ile ya mavazi yanayobana sana.

Tafiti kadhaa za kisayansi zinabainisha kuwa miongoni mwa nguo zinazoathiri afya ni nguo za ndani za wanaume zinazobana sana maarufu kama kama boksa pamoja na suruali za jeans zinazobana maarufu kama ‘skinny jeans’ ambazo mara nyingi huvaliwa na wanawake.Nguo zinazobana sana husababisha mishipa midogomidogo inayosafirisha damu kubanwa na kuathiri usambazaji wa damu kwenye baadhi ya maeneo ya mwili.Kutokana na hali ya kubana, nguo hizo husababisha uharibifu wa misuli na mishipa ya fahamu katika mapaja na miguu hasa kwa wanawake.

Mara nyingi madhara ya nguo hizi hujitokeza kama dalili ya miguu kufa ganzi au hisia za miguu kuwaka moto na ni mara chachewahusika kutambua kuwa dalili hizo chanzo chake ni mavazi.Katika ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa Juni mwaka 23, mwaka jana na Jarida la Neurology, Neurosurgery and Psychiatry, inaonyesha kuwa watafiti katika Hospitali ya Royal Adelaide nchini Australia walihusisha nguo za kubana sana za aina ya jeans na kutokea kwa tatizo la misuli lijulikanalo kitabibu kamacompartiment syndromeambalo alilipata mwanamke mmoja nchini humo.“Ugonjwa wa mwanamke huyu unaonyesha madhara mapya ya uvaaji wa jeans zinazobana.”  alisema

Dk Thomas Kimber, mmoja wa watafiti waliotoa ripoti hiyo alipokuwa akizungumza kuhusu madhara ya mavazi ya kubana.Mtaalamu wa mishipa ya fahamu na mwanachama wa chama cha Madaktari wa Mishipa ya Fahamu cha Marekani (AAM), Dk John England, anasema:

“Mishipa ya fahamu kwa baadhi ya watu, inaweza kukandamizwa kwa urahisi. Mshipa wafemoral cutaneousunaotoka kwenye nyonga na kuingia mapajani kwa ajili ya kuchukua hisia, unaweza kubanwa na kitu chochote kinachobana mapaja au eneo la kiuno.”

Hali ya kubanwa kwa mishipa ya fahamu kama itakuwa ya kujirudia rudia inaweza kusababisha madhara ya kudumu.Madhara ya nguo za kubanaKwa wanawake nguo zinazobana kupita kiasi zinaweza kusababisha damu kuganda ndani yamishipa, uvimbe wa mishipa ya damu kwenye miguu na magonjwa ya fangasi ya ngozi yanayoambatana na muwasho.Hii inaweza kutokea kwa sababu ya jasho linalozalisha kwa wingi katika nguo zinazobana na kufanya ngozi ikose hewa safi.Uvimbe wa mishipa ya damu miguuni maarufu kama vericose veins, ni moja ya matatizo yanayowapata mara kwa mara wanawake wajawazito na wale wanaotumia vidonge, vipandikizi na sindano za kupanga uzazi bila kufanya mazoezi ya mwili.

Tatizo jingine kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa mwaka 2004 katika toleo namba117(2) la Jarida la Ejog (Europian Journal of Obstetrics & Gynaecology and Reproductive Biology) ni ongezeko la kuzaliana kwa bakteriawaharibifu ambao wanasababisha mwanamke kutokwa na usaha katika sehemu za siri.Hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wanawake wanene na watu wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari.Kwa wanaume, mavazi haya yanaweza kuathiriutendaji wa figo pamoja na kibofu cha mkojo na kuchochea kutokea kwa maambukizi katika njia ya mfumo wa mkojo.Yanaweza pia kusababisha uvimbe wa mishipa ya korodani au makende na kuathiri ubora wa mbegu za kiume. Hali hii wakati mwingine huwani chanzo cha ugumba na upungufu wa nguvu za kiume kutokana na athari za maumbile ya kianatomi pamoja na athari za kisaikolojia.

Utafiti ulioongozwa na Dk F. Parazzini wa nchini Italy na kuchapishwa mwaka 1995 katika Jarida la International of andrology toleo namba 18(3), ulionyesha kuwa, uvaaji wa nguo zinazobana unaathiri uwezo wa wanaume kuzalisha mbegu za kutosha.Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake naUzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe anasema athari za mavazi hayayapo mengi na mbaya zaidi ni yale yanayogandamiza mfumo wa uzazi wa mwanaume. Anaonya kwamba watu wengi wanaovutiwa na mavazi hayo hasa vijana, wanapaswa kuwa makini kwa sababu tafiti zilizofanywa zimethibitisha watu kuathirika.

“Mwanaume ili kuhifadhi vizuri mbegu zake, anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” anasema Dk Massawe.

Kutokana na athari za muda mfupi na zile za muda mrefu za mavazi yanayobana sana mwili, mtaalamu huyo wa afya anaonya jamii haina budi kuzingatia afya na usalama kwanzakabla ya kufikiria urembo na kupendeza.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa urembo na utanashati bila afya njema ni sawa na kujificha katika kichaka cha karanga,” anaonya kwa usemi huo wa Kiswahili.

Karanga ni mmea unaoota kwa mfano wa kichaka lakini urefu wake hauzidi sentimita 20 hivyo hauwezikumsitiri mtu, ili ajifiche, asionekane.

Je, tabia hii yaweza kukoma?Ni vigumu kubadili mitindo ya mavazi ambayo inashabikiwa hasa ikizingatiwa kuwa athari zake si za wazi. Mtu anaweza kusema kuwa amevaa mavazi ya namna hiyo kwa muda mrefu lakini hajaona madhara. Lakini ukweli ni kwamba athari zake zinaweza zisionekane wazi lakini zikawa ni za polepole na ambazo zitasababisha madhara makubwa miaka ijayo.Suala la kubadili tabia ni la mtu binafsi na ni jambo ambalo litatokana na mhusika baada yakupima faida na madhara ya mavazi haya yanayopendwa zaidi.

Ni suala la mtu kujiuliza; nionekane mtu wa kisasa kwa wakati huu mbele za watu na baadaye niwe na matatizo ya kiafya au niachane na mambo ya kuiga ili niwe na afya njema maishani.Kuonekana nadhifu na mtanashati siyo lazimakuvaa mavazi yanayobana sana. Waweza kuvaa mavazi yanayoruhusu mwili kutoathirika na ukaonekana nadhifu.Tatizo hapa ni ile hali ya kuvaa mavazi yanayobana mwili na wengine ingawa wanajihisi vibaya huvumilia. Kumbuka kuwa na afya bora kwa sasa na siku za baadaye za maisha yako ni jambo muhimu katika kukufanya uishi miaka mingi duniani.

Sunday 20 March 2016

SIMULIZI YA KIMAPENZI YENYE MAFUNDISHO


HADITHI FUPI.
************
“NITAKUBEBA KILA ASUBUHI MKE WANGU MPAKA KIFO KITAKAPO TUTENGANISHA”.
*************
MTUNZI: ELIA MWAIPOPO & SHUFAA.
************
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu.
Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu . Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini ?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike . Akatupa kijiko na akanikaripia , ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu . Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Husna. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Husna. Kwa kweli nilimdharau mke wangu !Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa , niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu .
Nilimuonea huruma kwa muda , rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Husna aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu , jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu .Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miezi kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi .Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani . Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka . Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika . Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika . Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mtoto wetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu . Hili halikuwa tatizo kwangu , nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada , aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku ya harusi yetu . Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa . Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu .Nilimsimulia Husna kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu . Husna alicheka sana , aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Husna tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki . Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana . Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja . Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni , halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu . Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka . Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba . Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote . Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake . Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana . Nikagundua hakuwa binti tena . Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe ! Ndoa yetu imekula urembo wake . Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi . Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea . Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa . Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya . Sikumwambia Husna kuhusu jambo hili . Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi . Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi .Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi . Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa . Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana , nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi . Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake . Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake . Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu . Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho . Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani , sebuleni halafu mpaka mlangoni . Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo . Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka .Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja . Mtoto wetu alishakwenda shuleni . Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo . Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango . Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Husna alifungua mlango nikamwambia, ‘ Samahan husna, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu , halafu akagusa kichwa changu . Akaniuliza ‘Unaumwa ?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Husna, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu . Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu , mimi na mke wangu , si kwamba hatupendani . Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu , nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenga
nisha.’ Ikawa kama Husna alizinduka usingizini . Akanizaba kibao cha nguvu , akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia . Nikashuka ngazi na kuondoka zangu . Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu . Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi . Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu , tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani , nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani . Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Husna sikuwa na muda wa kukaa na kujadili maisha wala matatizo ya mke wangu .
Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mtoto wetu kama ningelazimisha talaka mapema . Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….................Mungu amuweke mahala pema peponi mke wangu . Nitamkumbuka daima .
MWISHO****
KUMBUKA
SHARE, COMMENT & LIKE

Friday 18 March 2016

MASKINI MTOTO HUYU AZALIWA BILA PUA!!!!


Tukio hili la mtoto anaezaliwa bila kuwa na pua huyokea mara chache sana ambapo kati ya watoto milioni 197 basi humkumba mtoto mmoja.Je mtoto huyo anaishi vipi?

Mtoto huyo Eli,alizaliwa katika eneo la Alabama nchini Marekani mnamo tarehe 4 mwezi wa tatu.Mara baada ya madaktari kumkabidhi mtoto huyo mama,mara moja mama yake aitwae Brand MvGlathery aligundua kuwa mwanae amezaliwa bila kuwa na pua.Aliamua kumpeleka katika hospitali ya 'USA Children's and women's Hospital in mobile' iliyoko pale pale Alabama ili kuona wataalamu wanaoweza kumsaidia mwan
ae. Aliweza kupumua bila shida baada ya kutoka hospitalini pale.

Mama yake amekuwa karibu sana na madaktari kuhakikisha kuwa anapata maelezo sahihi ya namna ya kumtunza vema mtoto huyo.
Tukio kama hili liliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1931 na linajulikana kitaalamu kama *Congenital Arhinia*

Inaweza kuwa ni ngumu kuishi kwa hali hii kuelekea utu uzima lakini kuna watoto wameweza kukua wakiwa na hali hii hadi kuwa watu wazima.Mama wa mtoto huyo amekuwa karibu sana na wazazi wa watoto wengine waliozaliwa bila pua na kuweza kukua vema hadi ukubwani licha ya kupata changamoto ya mfumo wa upumuaji.Mama huyo anasema hii imemsaidia sana kuweza kupata taarifa muhimu pia ya namna ya kumlea mtoto wake.

Yuko sawa kwa hali aliyonayo.Pia kunabnjia mbafala ya kumfanyia upasuaji ili kumwekea umbo la pua yaani pua bandia kwa hiyo mama yake analitumainia hilo.Mama yake anasubiri aje aamue mqenyewe ukubwani kama anahitaji pua bandia ama la.
     
           "Hadi pale atakapohitaji pua bandia,sisi hatutafanya lolote lile,tutasubiri uamuzi wake pale atakapoweza kuwa na maamuzi yake mwenyewe"

Alimalizia mama wa mtoto huyo.


Kama umeoendezwa nayo waweza share
Karibu tena kwenye ukurasa huu.

Thursday 17 March 2016

MASKINI JIDE TARAKA YAANZA KUMTESA!!!

Jambo limezua jambo! Siku chache baada ya kukabidhiwa talaka na aliyekuwa mumewe, Gardner G. Habash ‘Captain’, mali za mrembo wa nguvu, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ zinadaiwa kuzua kizaazaa baada ya kusemekana kutokea mvutano wa baadhi ya ndugu wa mwanamuziki huyo kutaka amgawie mtalaka wake  huyo, Amani lina ubuyu kamili.TUANZE NA TALAKABaada ya Jide au Lady Jaydee kuishi kwa zaidi ya miaka 9 ndani ya ndoa na Gardner, Februari 12, mwaka huu, wawili hao walivunja rasmi ndoa yao katika Mahakama ya Mwanzo Manzese- Sinza jijini Dar na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka hivyo hadi leo zimepita siku 35 tangu walipotengana.USTAWI WA JAMII WALIAMUALicha ya kupeana talaka, awali vikao vya ugawaji wa mali katika Idara ya Ustawi wa Jamii, Magomeni jijini Dar viliamua kuwa Gardner hakuwa na chake katika mali kwa kile kilichoelezwa kwamba, alikuwa kama mwajiriwa katika kazi za sanaa za Jide.Mjengo wa Jide ulioko maeneo ya Kimala.TWENDE KWA NDUGU WA JIDENdugu wa Jide aliyejitambulisha kwa jina moja la Jack, aliliambia Amani kwamba, baadhi yao wamecharuka na kumwambia Jide atende haki kwa kumgawia mwenzake (Gardner) kwani hawana kinyongo naye na walimtambua kama mume kwa kipindi chote cha ndoa yao.“Ni mvutano! Kuna ambao wanataka Jide agawe asilimia hamsini kwa hamsini ya mali zake kwa vile licha ya kwamba alikuwa kama meneja wake katika kazi, lakini kwa upande mwingine alikuwa ni baba wa familia. Lakini kwa upande wa ndugu wa Gardner, hatujasikia wakisema lolote.

”WENGINE HAWATAKI KUSIKIA“Hata hivyo, kuna ambao hawataki kusikia Gardner anapewa hata sentitano kwani wanaamini ndugu yao (Jide) hana hatia hivyo Gardner ale jeuri yake maana alishindwa mwenyewe kuheshimu ndoa na kusababisha migogoro,” alisema ndugu huyo na kuongeza:WATOLEANA MANENO MAKALI“Hali imefika pabaya, imefika mahali wale ambao wanataka Jide asimpe chochote Gardner wanawapa maneno makali wale wanaotaka apewe. Kila mmoja anavutia kwake.”KESI YATAJWAKwa mujibu wa chanzo chetu kingine cha habari, baadhi ya ndugu hawaridhiki na kizaazaa hicho hivyo kutaka kumshawishi Gardner akafungue madai ya mali mahakamani ambapo wanaamini atapata haki yake.“Wamekasirika! Wanaona bora wamtafute Gardner wamuume sikio aende mahakamani,” kilisema chanzo hicho.

JIDE BIZE NA PROJEKTI MPYAWakati ndugu hao wakisigana hadi kutoleana maneno makali, imeelezwa kuwa Jide ‘ameziba’ masikio akiwa ameelekeza nguvu zake katika projekti yake mpya ya Naamka Tena.“Wamempelekea taarifa za mvutano, Jide hataki hata kuwasikiliza. Yupo bize na projekti yake ya Naamka Tena, si unajua zimebaki siku chache arudi upya kwenye soko? Hawajibu kama atamgawia mali hizo au la,” kilisema chanzo.Jide akiwa na mkoko wake aina ya Range Rover Evoque.JIDE HUYU HAPAJitihada za Amani kutaka kujua undani wa habari hiyo ziligonga mwamba kufuatia simu ya Jide ya mkononi kuita bila kupokelewa.Hata hivyo, Amani lilitumia njia ya meneja wake aliyeomba hifadhi ya jina na kufanikiwa kumpata Jide waliyekuwa naye pamoja ambapo alikiri kutokea kwa mvutano huo wa ndugu lakini akaomba aachwe kwani yupo bize na shughuli za ujio wake mpya.“Jamani mvutano ni wa kawaida. Mimi nipo bize na ujio wangu mpya, mbona hamniulizi kuhusu kazi yangu mpya ya Naamka Tena? Kuhusu mali mimi naheshimu uamuzi wa Ustawi wa Jamii,” alisikika Jide.GARDNER SASABaada ya kumalizana na Jide, Amani lilimgeukia Gardner, mtangazaji maarufu Bongo wa Redio EFM ili kumsikia anazungumziaje kuhusu mvutano huo wa mali na namna ambavyo baadhi ya ndugu wa Jide wanamtetea.“Hivi kuna ndugu wana huruma hiyo? Mungu awabariki sana. Kwa upande wangu mimi namshukuru Mungu ni mzima wa afya, napambana kutafuta maisha yangu. Sina mpango wa kudai mali, najua Mungu atanipa tu,” alisema Gardner.

MALI ZENYEWE NI ZIPI?Mali ambazo zipo mikononi mwa Jide hadi sasa ni pamoja na nyumba zilizopo Tegeta, Kimara-Temboni na Kiwalani jijini Dar. Pia kuna shamba (haikujulikana ekari ngapi) lililopo Bagamoyo, Pwani.Gari aina ya Nissan Murano analo Jide,  Range Rover Evoque analo Jide na basi  nk





Source:bongomovies


















Wednesday 16 March 2016

MWANAMKE MIAKA 62 AOLEWA NA KIJANA WA MIAKA 9!!!!!


Mvulana mwenye umri wa miaka 9 anaejulikana kama Saneie Masilela amekuwa mume mdogo zaidi duniani baada ya kumwoa mwanamke mwenye umri wa miaka 62 ambaye alimchumbia tangu mwaka jana.

Akiwa ndani ya suti yake ya kupendeza mvulana huyo mdogo aliunyanyua mkono wa Bi kizee huyo ambae ni mchumba wake,Helen Shabangu mwenye watoto  watano  na kvisha pete ya ndoa.Watoto wa mama huyo wana umri kati ya miaka 28 na 35.
Mvulana huyo alisema kuwa aliamua kumuoa kabisa baada ya uchumba ili iwe rasmi lakini majirani zake wa vijiji vya Ximhungwe eneo la Mpulanga wanaona kama ni uchizi.
Sherehe ya harusi hiyo ilifanyika mbele ya mume qa zamani wa mwanamke huyo,Alfred Shabangu ,66,ambae pia alihudhuria sherehe za uchumba wao mwaka uliopita.

"Watoto wangu wana furaha sna na ndoa hiina hawana matatizo kwa mimi kuolewa na mvulana huyu mdogo,pia sijali watu wanasema nini juu ya hili."Alisema mwanamama huyo.

Mume huyo mdogo duniani alisema
         "Nilimwambia mama yangu kuwa nahitaji kuoa na kiukweli nilikuwa nahitaji sana.Nina furaha  kumuoa Helen,nampenda lakini nitahakikisha narudi shule na kusoma kwa bidii.Nitakapokuwa mkubwa nitaoa mwanamke wa umri wangu.Nimechagua yeye kwa kuwa sikai nae muda mwingi,huwa nakutana nae eneo ambalo mama yangu anafanyia kazi.“

Mama wa kijana huyo nae alikuwa na ya kuongezea
          "Mwanangu Sanele alikuwa nsawanna mwenye furaha kwa sababu aliitaka ndoa hii na hakuwa na aibu hata kidogo.Alifurahi sana kiasi kwamba alihitaji tena kusherehekea.Wati wengi waliniuliza je wataishi pamoja?Watalala pamoja?Je watapata watoto pamoja?Niliwajibu kuwa baada ya ndoa kila kitu kitakwenda kama kawaida,hakunabkinachobadilika."

Je mnakubaliana na ndoa hii ya ajabu??????

Share tafadhari kama umeipenda.

Asante kwa kuingia ukurasa huu karibu sana kwa habari tamu tamu.

         

Monday 14 March 2016

MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO 17

Mwanamke mmoja nchini Marekani amevunja rekodi ya dunia ya kujifungua watoto wengi kwa wakati mmoja alipojifungua watoto 17 kwa wakati mmoja.Alitumia takribani masaa 29 ambao ni sawa na siku nzima moja na masaa 5.
Akitoa ushuhuda,daktari aliemsaidia kujifungua watoto hao alisema
       
"Watoto waliendelea kutoka na kutoka.Nahisi ni jambo la kushangaza ambalo litakaa moyoni mwangu kwa muda mrefu sana."

MWanamke huyo Catherine Rodgers na mumewe,walijaribu mara kadhaa kupata mtoto mtoto lakini hawakufanikiwa hadi walipotembelea kituo cha masuala ya uzazi kilichopo katika kisiwa cha Rhodes na kufanikiwa kupata tiba iliyopelekea mwananmke huyo kupata ujauzito wa watoto hao.

Watoto hao ambao wote ni wa kiume wamepewa majina haya
James, Jacob, Jarod, Jarvis, Jason, Jeffrey, Jeremy, Jerome, Jesse, Jimmy, Joachim, Jonathan, Jonas, Joseph, Julian, Jimbo,Darth na Porkinus.

Saturday 12 March 2016

JELA KWA KUMKATA SEHEMU ZA SIRI MKEWE


MKAZI wa kata ya Mbugani mjini Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kwenda jela miaka saba baada ya kupatikana na hatia ya kumkata mkewe sehemu za siri kwa imani za kishirikina ili ajipatie mali.

Aidha, Maziku na mshirika wake ambaye ni mganga wa kienyeji, Kahele Paul, wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kula njama ya kutenda kosa. Walihukumiwa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Jackton Rushwela baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.

Hakimu Rushwela alisema anamhukumu Maziku kwenda jela miaka saba, iwe fundisho kwa wananchi wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina huku wakiwasababishia madhara watu wengine.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Idd Mgeni, washtakiwa walitenda makosa hayo mwaka juzi, kati ya Oktoba 29 na Novemba 2 katika eneo la Kazaroho kata ya Mbugani mjini Tabora.

Ilidaiwa kwamba Maziku aliambiwa na mganga wa kienyeji ambaye ni mshtakiwa wa pili , kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata Sh milioni tano. Mahakama ilielezwa kwamba, Maziku baada ya ushauri huo huku akiwa na tamaa ya kujipatia mali, alimchukua mkewe (jina tunalihifadhi) na kwenda kumnywesha pombe kabla ya kutimiza ukatili huo.

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne ambao waliiambia Mahakama kwamba mshtakiwa baada ya kumnywesha pombe nyingi mkewe alichukua kisu na kumkata sehemu za siri na kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na akatoweka.

Walibainisha kuwa mama huyo alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi na aliokolewa na majirani na kumpeleka hospitali ya mkoa kwa matibabu.

Maziku baada ya kukamatwa na kuhojiwa, alikana akidai kwamba yeye aliondoka na kumwacha mkewe akiwa ni mzima, lakini ulipofanyika upekuzi, nyama ya nyeti hizo zilikutwa kwenye mfuko wa suruali yake.

Upande wa mashitaka uliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa, kwani vitendo vya ukatili vya aina hiyo kwa ajili ya kujipatia mali, vimekuwa vinawasababishia madhara watu wasiokuwa na hatia.

ALIKIBA-SIJAWAHI KUMPENDA JOKETI...

Staa anayesumbua na wimbo wa Lupela, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amedaiwa kumlipua Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa kusema hakuwahi kuwa na mpango wa kudumu naye penzini, Risasi Jumamosi linakupa ubuyu kamili.Hivi karibuni, Jokate alizungumza na wanahabari wa Global Publishers na kudai amemchoka mpenzi wake huyo hivyo ameamua kumuacha rasmi Kiba ambapo habari hiyo ilichapwa jana kwenye Gazeti la Ijumaa.Kiba na Jokate.Chanzo kilicho karibu na Kiba kimeweka bayana kuwa mkali huyo hakuwa na mpango na penzi la Jokate lakini alilazimika kuwa naye karibu kwa shughuli za kikazi (muziki).“Tunamshangaa Jokate kusema eti amemchoka Kiba leo wakati anajua kitambo tu Kiba hakuwa na mpango naye. Kiba alilazimika ‘ku-fake’ penzi kwa sababu walikuwa wanafanya kazi za pamoja, hakuwa na jinsi.Jokate“Jokate mwenyewe anajua kwamba Kiba hakuwa na mpango naye. Nafikiri kajitokeza kwenye ‘media’ ili aonekane yeye ndiyo kamuacha Kiba kumbe mwenzake hata hakuwa na mpango wa kuwa naye,” kilisema chanzo hicho.Gazeti hili lilimtafuta Kiba katika simu yake ambapo alidai hapendi sana kuanika mambo yake binafsi kwenye vyombo vya habari lakini mmoja wa mameneja wake aliyeomba hifadhi ya jina, alifafanua suala hilo.“Kiba hakuwa na mpango na Jokate na ndiyo maana kila siku tunapokuwa kwenye kazi zetu hapendi umtajie ishu za Jokate hata kidogo na alikuwa akisisitiza kweli lakini sisi tulikuwa tunalazimisha waendelee kwa sababu tulikuwa tunafanya kazi za pamoja,” alisema meneja huyo.

MCHUNGAJI:WANAWAKE MARUFUKU KUVAA CHUP* KANISANI


Mchungaji mmoja nchini Kenya amewaambia wanawake waumini wa kanisa lake waache kuvaa nguo za ndani wanapohudhuria ibada  ili "mungu aweze kuwaingia vema na kwa urahisi"
Mchungaji huyo anaejulikana kwa jina Njohi wa kanisa la  *Lord's Propeller Redemption Church* la Nairobi amesema hayo kwa wanawake wa kanisa hilo huku akiongezea kuwa kuingia kanisani bila nguo ya ndani kunasaidia mtu kuwa huru kimwili na kiroho ili kumpokea vema kristu kwa mujibu wa "Kenyan Dialy Post"
Pia amewaonya kuwa wafuate maagizo hayo kuepuka madhara watakayoyapata kama hawatafuata maagizo hayo.Lakini inaaminika kuwa maagizo hayo hawajapewa wanaume wa kanisa hilo.
Wanawake wa kanisa hilo wameanza kufuata maagizo hayo ya kuhudhuria ibada bila nguo za ndani na mchungaji amewambia wanawake hao kuwafuatilia mabinti zao kama nao wanafuatilia agizo hilo.
Kanisa hili liko eneo la Dandora mashariki mwa jiji la Nairobi.
Je kama wewe ni muumini wa kanisa hili utaendelea kusali?????Je ndizo zama za mwisho na manabii wa UONGO????

Share tafadhari kama umeipenda.
Asante kwa kuhudhuria katika ukurasa huo,karibu kwa habari motomoto.

Thursday 10 March 2016

CHRIS BROWN:NIMECHOKA KUABUDU MASHETANI





Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa amechoka kuoan shetani akiyaharibu maisha yake.Katika post aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa instagram hivi karibuni ameandika kuwa shetani anajaribu kuyaharibu maisha yake.Pia ameandika kuhusu kuwa na mawazo ya kujiua na kuisikia sauti ya MUNGU ikimsihi kwa mara ya kwanza.Haya ndo aliyoyaandika
     
   "Pale unapochoka shetani anapoyaharibu maisha yako na unapoiskia sauti ya MUNGU kwa mara ya kwanza.Hakuna ajuae nachokifanya siku baada ya siku.Mtu wa kawaida hawezi umiza kichwa au akili yake ila ni uoga tu.Wengi hawafahamu ufahamu na uzuri ni katika mabadiliko na kujifunza ila wale walio na muelekeo wa kishetani huyapata kwa muda mfupi mafanikio.
Roho yangu daima itakuwa yenye haki na safi.Unavyoniona kwa muonekano wa nje sivyo ila ndani nina mvulana mdogo anaehitaji msaada na mwongozo pia.Watu hunambia KUWA MWANAUME.Sawa ila haiwezi kuondoa maumivu unayoyapitia.Nahitaji kutoka katika njia hii na kujikita na muziki wangu.Ninapenda niweze kuwa Baba bora.Sina uvumilivu tena na vitu au kitu kitakachosababisha kujiharibia maisha yangu."



Je ni ushahadi wa wazi kuwa Chris Brown nae yuko katika vyama vya siri vya waabudu mashetani?

Wednesday 9 March 2016

MWANAMKE WA UINGEREZA AOLEWA NA MBWA NDOA YA KIFAHARI.

Mwanamke mmoja raia wa Uingereza Amanda Rodgers ameamua kuolewa na mvwa wake aitwae SHEBA baada ya kuachana na mumewe katika ndoa iliyodumu kwa miezi kadhaa.
Mwanamke huyo alifunga ndoa yake na mwanaume huyo miaka 20 iliyopita ndoa ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa halafu wakaachana.Amanda akaweka kiapo cha kutokupenda tena mwanaume na kwa muda wote huo akaamua kuwa na uhusiano na mbwa wake 'sheba'.
Amanda alisema kwamba ameamua kuolewa na mbwa huyo kwa kuwa mbwa huyo ametimiza vigezo vyote vya aina ya mpenzi anaemtaka.
     
               "Sheba amekuwa katika maisha yangu              kwa miaka kadhaa,amenifanya kuwa wa furaha na kuniliwaza ninapokuwa na huzuni."

Zaidi ya watu 200 walihudhuria sherehe hiyo ya harusi ya kushangaza iliyofanyika Split,Croatia.
Amanda alihakikisha kila kitu kinakwenda sana na harusi inakuwa ya kupendeza.Alisema

         "Niliota tangu mdogo kuwa na harusi iliyotimia na kuvaa mavazi bora ya harusi.Hakika hii imekuwa siku nzuri sana kwangu"

Amanda hajali watu wanasema nini juu yake.Anasema kuwa anajua kuwa ndoa hiyo haipo kisheria ila ilikuwa nzuri na kuonesha sheba ana umuhimu gani kwake.


Monday 7 March 2016

ATHARI ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI


Mobile Phone Tips Tricks & More.Simu yako ni HATARI SANA kwenye Afya yako.Fuhamu MADHARA yatokanayo na simu yako na JINSI YA KUYAPUNGUZA.Simu tunazozitumia hutoa mionzi (radiations) hatari sana ijulikanayo kama"Electromagnetic waves" wakati wa kupiga/kupokea simu, kuperuzi Internet,nk..

Madhara ya Mionzi hii;
1. Husababisha Saratani ya Ubongo (Brain Cancer) na ngozi (Skin Cancer).
2. Husababisha hitilafu kwenye Ubongo na hii hupelekea kupoteza kumbukumbu, uwezo mdogo wa kupambanua mambo na umakini (Concentration).
3. Husababisha upungufu wa mbegu za kiume na hata utasa (Impotence) kwa wanaume.
4. Huongeza shinikizo la damu.

Jinsi ya kupunguza Athari zitokanazo na Mionzi hii hatari;
1. Weka vifaa maalum vya kupunguza mionzi (Radiation absorbers) kwenyesimu yako. Vinapatikana madukani.
2. Usipende kuweka simu mfukoni endapo huitumii. Wakati wa kulala weka mbali angalao SM 30 kutoka ulipo.
3. Simu iwapo mfukoni, upande wa Vitufe na kioo cha simu ndio kielekee mwili wako!
4. Tumia "headsets" au "Kipaza sauti (Loud Speaker). Hii hukusaidia kuwa mbali na mionzi wakati wa kupiga/kupokea simu.
5. Usiitumie simu yako iwapo ina "bar" moja au mbili za "network" (Low Network Signal). Wakati huu simu inafanya kazi kupita kiwango cha kawaida hivyo huongeza wingi wa mionzi.
6. Wakati wa kupiga simu, subiri ipokelewe ndio uisogeze karibu ya mwili (mf. Masikioni).
7. Iwezekanapo, penda kuwasiliana kwa ujumbe wa sauti (text msg) kulipo kupiga simu.Simu ni muhimu sana katika Maisha yetu ya sasa. Hutuunganisha na ulimwengu uliogubikwa na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.Sanjari na hili, tunapaswa kuwa makini katika juhudi za kujaribu kepuka Madhara yatokanayo na simu kama ilivyoainishwa hapo juu.

Source: Internet
Prepared by;••Athanas Chriss••

IJUE HISTORIA YA KWARESIMA NA IBADA KAMILI



Nini maana ya Kwaresima?
Kwa Kilatini na Kiitaliano neno Kwaresima lilimaanisha “40” yaani siku 40 za kufunga za wiki kati ya Jumatano ya Majivu hadi Jumamosi Kuu. Kwa Kijerumani Kwaresima maana yake “Kipindi cha kufunga.”
Kwaresima ilianzaje?
Kabla ya kuona Kwaresima jinsi ilivyoanza, ni vizuri kuongea kidogo kuhusu Sikukuu ya Pasaka ili tuweze kupata mwanga wa kuelewa mwanzo wa kipindi hiki muhimu cha Kwaresima.
Habari Njema yatuambia kwamba YESU KRISTO alifufuka “Siku ya kwanza ya juma.” “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.” (Mt.28:1) Hii ni kwasababu Wakristo walianza kukutana pamoja kwa sikukuu ya ufufuko wa BWANA kila wiki sio Jumamosi kama Wayahudi, bali siku iliyo fuata. “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza -`maneno yake hata usiku wa manane.” (Mdo.20:7). “Siku ya Kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake: ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja.” (1Kor.16:2), siku ambayo Warumi waliita “Siku ya Jua”. Mara moja jina hilo lilibadilika na kuwa “Siku ya BWANA”
Kanisa la mwanzoni halikusherehekea sikukuu kama vile Noel, Sikukuu kwa heshima ya Mama Bikira Maria au sikukuu yeyote ile. Kulikuwepo na adhimisho la ufufuko wa BWANA kila wiki na hakuna zaidi.
Miaka mingi ikapita kanisa likiwa katika hali hii. Baadaye kulikuwepo na hitaji la kusherehekea tukio la kiini cha imani yetu kwa namna ya pekee. Wakristo waliona umuhimu wa kuwa na muda kwa sikukuu ya kwanza kati ya sikukuu zao yaani “Jumapili ya Pasaka”, ambayo ilifikiriwa kama “Mama wa Jumapili zote”, “Mama wa skikukuu zote”. Waliiona sikukuu hiyo kama “Malkia wa sikukuu zote, wa Jumapili zote, na kiujumla kama Malkia wa siku zote za mwaka. Tangu mwanzoni mwa karne ya pili, Jumuiya zote za Kikristo walikuwa wanasherehekea sikukuu hii ya Pasaka. Sherehe zilikuwa zinahitimishwa na kusanyiko la sala lililofanyika usiku na kumalizikia na Ekaristi. Ushiriki wa kwenye ibada hiyo, ulichukuliwa kama ni kitu muhimu sana kwa mkristo.
Kuanza kwa Kwaresima
Wote tunafahamu kwamba, ufanisi au mafanikio yoyote ya sikukuu au ya jambo lolote yanategemea sana maandalizi yake. Miaka miambili hivi baada ya KRISTO, Wakristo walitaka kuvuna matunda ya kiroho ya Paska kwa wingi. Ili kufanikisha hili, walianzisha utamaduni wa kuwa na siku tatu kabla ya Pasaka kwa sala, tafakari na kufunga kwa nia ya kuonyesha masikitiko yao juu ya kifo cha YESU KRISTO. Kutokana na ukubwa na umuhimu wa sikukuu hii, mbali ya kuona umuhimu wa maandalizi, walitafuta njia za kuongeza muda wa furaha na utajiri wa kiroho utokanao na Pasaka. Hivyo walianzisha “Wiki Saba,” yaani siku 50 za Pentekoste ambapo walisherehekea na kuzipitisha siku hizo kwa hali ya furaha. Askofu Mt. Ireneus alisema kuwa muda huo wa siku 50 ni kama Sikukuu ya Siku moja yenye umuhimu sawa na Jumapili. Katika kipindi cha siku za Pentekoste, sala zilikuwa zinasaliwa hali wamesimama, kufunga kulikatazwa na sakramenti ya ubatizo ilikuwa ikiadhimishwa. Ni kama vile sikukuu ya Pasaka ilidumu kwa kipindi chote cha siku 50. Miaka 150 ilipita na mwishoni mwa mwaka 350 B.K., Wakristo waliona kama siku tatu hazikutosha kwa maandalizi ya sikukuu kama hii. Hivyo waliongeza hadi kufikia siku 40. Hivi ndivyo Kwaresima ilivyoanza.
Kwa nini siku 40?
Tunaposema kuku wanne au kilo saba za mchele tuna maana kama ilivyo yaani kuku wanne na kilo saba za mchele. Si zaidi au pungufu.
Namba au tarakimu mbalimbali tunazokutana nazo katika Biblia zinaashiria lugha za picha na siyo kuchukulia katika thamani ya kuhesabu. Hivyio basi, tunapokutana na namba kama 40 huenda isimaanishe 40 kama tunavyo hesabu fedha. Kati ya maana nyingi zilizotolewa kwa namba 40, kuna moja yenye maana ya pekee, inamaana ya kipindi cha maandalizi cha kutosha kisichokuwa na muda maalum, kwa tukio kubwa. Kwa mfano , Gharika ilidumu kwa siku 40 usiku

Friday 4 March 2016

MAKALIO YA KICHINA YAWAPONZA KINA DADA


Makalio ya kichina yageuka shubiri kwa kina dada waliotukia dawa za kuyapata.Hali si hali maana wanajuta sana.
Katika tukio jipya la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hamisa ambaye alidai ni mke wa mtu alisema kuwa, alishawishiwa na rafiki yake kutumia dawa hizo ili naye awe na ‘zigo’ lakini ameanza kuona zinamletea matatizo. “Nimekuwa nikisikia kuwa dawa hizi zina madhara lakini kuna rafiki yangu mmoja ambaye aliwahi kutumia na yuko poa ndiye aliyenipeleka kwenye duka moja lililopo Kijitonyama na kununua. Awali sikuona tatizo lakini kadiri siku zinavyokwenda nahisi maumivu f’lani, najuta kuzitumia dawa hizi kwa kweli,” alisema mwanamke huyo.
Kidoa. OFM mtaani Baada ya kupata malalamiko hayo, waandishi wetu walifanya uchunguzi na kubaini kuwa dawa hizo zinauzwa kwa siri sana tangu serikali icharuke na kutoa tamko la kuwashughulikia wale wanaoziuza. Katika uchunguzi huo, yamegundulika maduka kibao mitaa ya Kariakoo, Kinondoni na Mwenge jijini Dar ambapo wauzaji huziuza dawa hizo ‘kimagutu’ kana kwamba wanauza madawa ya kulevya au bangi.
Mwandishi wetu alifika kwenye duka moja lililopo Msimbazi baada ya kulengeshwa kuwa dawa hizo zinauzwa hapo, muuzaji alipoulizwa uwepo wa dawa hizo, kwanza alikataa lakini baadaye alikubali huku akionekana ni mwenye wasiwasi.
Afisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Gaudensia Simwanza. Dukani kwa Maimartha
Ilidaiwa kuwa, asilimia kubwa ya mastaa wanaotumia dawa hizo wanazinunua kwenye duka la Mtangazaji wa Azam TV, Maimartha Jesse na ili kujiridhisha OFM walitinga kwake na kumkuta dada ambaye jina lake halikufahamika ambaye alisema dawa hizo hawana dukani hapo ila mwandishi akitaka anaweza kutafutiwa. Baada ya mwandishi kujifanya anazihitaji kwa udi na uvumba, mdada huyo alimpigia simu mtu ambaye haikujulikana ni nani na ndani ya muda mfupi akawa amezileta dawa hizo ambazo zipo kwenye mfumo wa losheni. Alipopigiwa simu Maimartha na kabanwa juu ya kudaiwa kuwaharibu wanawake wenzake kwa kuwauzia dawa hizo, aliruka kimanga na kusema:
“Mimi sitaki kuzungumzia kuwa nauza au siuzi kwa sababu naiheshimu sana serikali na nafuata maelekezo wanayotoa, lakini ninavyojua dawa hizo zinauzwa kwa siri sana na wanaotaka kuuziwa ni wengi.” Aidha, wasanii wengi hawa wa kike wamekuwa wakidaiwa kutumia dawa hizo huku mastaa wa kizazi cha sasa kama vile Gift Stanford Gigy, Glasnost Kalinga ‘Gilla’, Asha Salumu ‘Kidoa’, Janet Jackson ‘Jayjay’ na wengine wakidaiwa kuwa maumbile waliyonayo siyo ‘orijino’.
Ijumaa lilipata fursa ya kuzungumza na wadada hao ambao sasa ni habari ya mjini kutokana na maumbo yao ambapo kila mmoja alifunguka kivyake:
Gigy: Kusema ukweli sijawahi kutumia dawa hizo, nazisikia tu. Umbo langu ni orijino na wala hayo masponji zivai, hata nikivua sasa. Kidoa: Shepu yangu ni ya kuzaliwa nayo, najua dawa za Kichina ni shida hivyo siwezi kuthubutu kuzitumia.
Gilla: Mh! Wapo wanaoniambia natumia dawa hizo, kiukweli nimezaliwa hivyo na hivi sasa nimepungua hapo mwanzo si ndo mgenishangaa. TFDA wanasemaje?
Baada ya OFM kufanya uchunguzi wake, waandishi wetu walizungumza na Afisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Gaudensia Simwanza ambaye alisema wanapambana kuhakikisha dawa hizo haziingii nchini na atakayekamatwa cha moto atakiona. “Lakini kwa kuongeza tu ni kwamba kuhusu watumiaji wanaopata madhara kwa matumizi ya dawa hizo wengi unakuta hatuna taarifa nao kwa sababu huwa hawaji kwetu moja kwa moja, wanakwenda mahospitali na sehemu nyingine kupata tiba, ila tunapopata taarifa kama hizi tunafuatilia na kuzitendea kazi,” alisema Simwanza. Aidha, dokta mmoja anayefanya kazi katika wizara ya afya ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema kuwa, sasa hivi wako makini kuhakikisha uuzwaji holela wa dawa zenye madhara kwa watumiaji unakoma. “Unajua hiki siyo kipindi cha mchezo, TFDA wanafanya kazi yao lakini wizara ya afya nayo inapambana, kikubwa ni tahadhari kwa watumiaji wa dawa hizo, wajue kwamba kuna madhara makubwa ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao hivyo waache,” alisema dokta huyo.

Source:globalpublishers

MASKINI MR NICE ANAISHA


Picha inayomuonesha Nice akiwa amepungua mwili ilizagaa mapema wiki hii kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliochangia mjadala wa picha hiyo, walisema staa huyo aliyetikisa kwa utajiri enzi hizo, kwa sasa atakuwa anaumwa sana huku mjadala mkubwa ukawa ni ya lini?

Baada ya Ijumaa kuinasa picha hiyo, lilifanya jitihada za kumpata msanii huyo kwa kumvutia waya alipopatikana, alifunguka kwa kirefu kuhusu afya yake:

“Kwanza hiyo picha ni ya kitambo sana. Si unakumbua lile sakata langu la mimi kulishwa sumu kwenye chakula? Basi ndiyo kipindi kile.

“Namshukuru Mungu niliiwahi ile sumu na kupewa dawa ambazo natumia mpaka sasa. Kweli nilipungua lakini ni wakati huo, kwa sasa sipo hivyo kama kwenye hiyo picha inayosambazwa mitandaoni,” alisema Mr. Nice.

Akaongeza kuwa ni kweli afya yake haiko poa sana kwa kuwa bado anaendelea kutumia dawa za kuimaliza sumu ile lakini siyo kama vile anavyoonekana kwenye picha hiyo.

Source :ijumaa

Thursday 3 March 2016

STORI KALI YA KIMAPENZI


SIMULIZI FUPI: NILIKUWA NA MPENZI
MTUNZI: George Iron Mosenya SIMU: 0655 727325
Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..Nilij isikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale. Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule, nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine. Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili atanitangazaje kwa marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidh uru lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotak a kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria yake, kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale nilipokuwa. Sikuwa nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia wasamalia wema, binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa zimenitoka na niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu. Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu ya kustaajabisha niliyokutana nayo. “Mpenzi Christopher mwanaume wa maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi wangu …nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu, nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE MTUMWA!!!!

SHARE KWA WENGINE MWISHO!!!

Tuesday 1 March 2016

JIONEE MAAJABU YA BARMUDA TRIANGLE.


Bermuda Triangle, ambayo pia inajulikana kama Devil's Triangle, ni eneo la magharibi wa bahari ya Atlantiki ya kaskazini ambapo idadi kumbwa ya ndege na vyombo vya baharini vinanadaiwa kutoweka katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama makosa ya binadamu, uharamia, hitilafu ya vifaa, au au maafa ya kiasili. Tamaduni maalufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida.Jisomee hapa chini baadhi ya maajabu ya eneo hili


1. Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi. Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa mud wa miaka 500.

2. Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic. Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda katika kisiwa kaskazini mwa kisiwa cha Atlantic.

3. Ajali/mgongano kati ya kimondo na dunia
Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Mgongano huo ulitokea katika eneo la bahari la Dunia na kusababisha bahari kuzama kwa futi 10,000 chini ya usawa wa bahari. Kimondo hicho kiliacha mionzi ambayo ambayo husababisha ndege kupoteza uelekeo inapofika katika eneo hilo na kuzamsha meli, ndege pamoja na binadamu.

4. Viumbe vigeni viishivyo sayari nyingine (aliens).
Inasemekana kuwa viumbe viishivyo angani, huwa vinakaa aktika eneo hilo la Bermuda triangle na hilo ni kama Mecca yao. Viumbe hao wana teknolojia ambayo hukinzana na teknolojia yetu ya Duniani, kwahiyo basi ndege, meli pamoja na binadamu wanapopita pale huvutwa na kani ya uvutano ambayo ni kubwa sana toka kwa wale viumbe waishio katika ilo eneo hilo la bermuda.

5. Kituo cha majaribio ya silaha.
Inasemekana serikali huwa zinajaribia silaha ambazo zinakuwa zimetengenezwa na uangalizi wa silaha hizo, pia inasemekana kwamba serikali ikishirikiana na viumbe watokao  sayari (Aliens) zingine huhusika katika majaribio hayo. Na hiyo teknolojia ni kubwa kiasi cha kukinzana na teknolojia ya duniani na hatimaye kusababisha madhara kwa meli na ndege pia.

6. Mji uliopotea
Inasemekana katika eneo hilo kulikuwa na mjia wa kale chini ya maji katika bahari ya Atlantic, ulioitwa Atlantis, mji huo ulikuwa umejengeka kwa barafu ambazo zilikuwa kama kioo ambazo pia zilikuwa ni chanzo cha nishati. Na huo mji ulisahaulika milele kwahiyo basi Bermuda iko kwenye huo mji uliozikwa kitambo ambapo kuna kani kubwa ambayo huharibu meli na ndege

7. Kituo cha Maharamia
Inasemekana Bermuda ni eneo kwa ajili ya maharamia kufanya kazi zao, maharamia hao ni wale wanaojulikana kwa bendera nyeusi zenye picha ya fuvu. Lakini dhana hii imeshindwa kuelezea ni kwanini ndege na meli huwa zunapotea katika eneo hilo kwani wachunguzi wa mambo wamehusisha na utekaji nyara wa meli baharini ambao hufanywa na maharamia hao.

8. Volkano.
Inasemekana Volkano pamoja na gesi ya methane katika eneo la Bermuda hupunguza mgandamizo wa maji katika eneo hilo na kufanya meli kupoteza uwezo wa kuelea na hatimaye kuzama. Eneo hilo mlimekuwa likitoa gesi hiyo ya Methane tangu miaka 15,000 iliyopita.

9. Ukungu wenye hali ya ki-electronic na sumaku
Ukungu wenye nguvu ya kuzalisha umeme ambapo husababisha dira hupoteza uelekeo na kuwachanganya marubani pamoja na manahodha. Na hatimaye ndege pamoja na Meli hizo hupotelea katika ilo eneo la Bermuda.

10. Mawimbi na hali ya hewa kubadilika kwa kasi.
Eneo la bahari ya Atlantic hasa upande wa Caribbean hukumbwa na kimbunga kikali pamoja na mawingu mazito, Bermuda ni eneo ambalo limepakana sana na Caribbean na hukabiliwa na upepo na wingu zito ambavyo husababisha mushkeli kwa ndege, meli
pamoja na binadamu.