Showing posts with label huwezi amini. Show all posts
Showing posts with label huwezi amini. Show all posts

Tuesday, 29 March 2016

JIONEE WATU WENYE UWEZO WA AJABU NA KUSHANGAZA


Je unafahamu kuwa watu wenye nguvu za ajabu kuliko uwezo halisi wa kibinadamu wapo?Ni kweli watu hao wapo na wengine wanaishi hadi sasa.Ni watu ambao wana vitu vya ajabu kama uwezo,nguvu na kuwa imara madhubuti.Wafuatao ni baadhi ya watu hao

1.WIM HOF
Huyu ana uwezo wa kukaa muda  mrefu sana eneo la baridi kali sana bila kupata madhara yoyote yale.Huyu ni mtu halisi anaweza kukaa muda mrefu sana eneo la baridi kali sana.Anazo tuzo 21 za Guinness ikiwemo ya kuoga kwenye maji ya barafu kwa muda mrefu.Huyu anaweza kukaa kilele cha mlima kilimanjaro kifua wazi kwa muda mrefu.

2.KELVIN RICHARDSON
Huyu ana uwezo mkubwa sana wa kuwaelewa wanyama.
Ana uwezo mkubwa sana wa kufanya urafiki hata na wanyama wakali zaidi duniani bila tabu yoyote.Ana uwezo wa kuwa na urafiki na chui,simba na fisi.Huwafanya marafiki na hata kulala nao pia.

3.CLAUDIO PINTO
Huyu anajulikana kama MACHO YA DARUBINI.Ana uwezo wa kuyatanua macho yake kipimo cha 7mm ambapo ni kiasi cha 95% ya mzunguko wa jicho lake.

4.HAROLD WILLIAMS
Anajulikana kama MWALIMU WA LUGHA.Huyu anasifika kwa kuwa na uwezo wa kujua lugha nyingi sana duniani.Je wewe una uwezo wa kujua lugha ngapi katika maisha yako yote?Huyu anafahamu lugha zaidi ya 58 ambazo anaziongea na kuandika bila shida yoyote ile.
Sio peke ake alie na kipaji hiki,pia wapo John Browning,Joseph Caspar na Doktar Carlos do Amaral Freire.

5.TIBETAN MONKS
Wana uwezo wa kuweka sawa JOTO la miili yao kwa kutumia akili au ufahamu wao.Wana uwezo qa kubadili joto la miili yao kwa kutumia akili yao tu.Wamewahi kurekodiwa wakibadili jotoridi lao kufikia kiasi cha nyuzi joto 8 za sentigredi.

6.RATHAKRISHNAN VELU
Anajulikana kuwa na meno ya ajabu yenye nguvu sana maarufu kama 'steel teeth'.Ana uwezo wa kuvuta treni ya mabehewa saba akitumia meno yake kuivuta kwa kutumia kamba ya chuma.Anajulikana pia kwa jina la KING TOOTH.

7.DANIEL BROWNING SMITH
Huyu anajulikana kama 'The rubber boy' ana uwezo wa kujipinda zaidi katika mikao mbali mbali.

8.STEPHEN WILTSHIRE
Ana uwezo mkubwa sana wa kukumbuka.Huyu ana uwezo wa kutazama kitu mara moja tu na kuweza kukichora kwa ufasaha kabisa.Ni maarafu sana kwa kuchora picha za miji mbali mbali kwa kuiangalia mara moja tu.Kama watu wengine hutizama mara kwa mara katika uchoraji huo,yeye hutizama mara moja tu na kuchora sehemu kubwa ya mji husika.

9.JESUS ACEVES
Huyu ni mtu mwenye nywele nyingi zaidi za usoni.Anapatikana katika familia ya kimexico yenye wanafamilia 24 ,huwa anazunguka duniani kuonesha watu muonekano wake huo.

10.DANIEL TAMMET
Ni mtaalamu sana wa mahesabu na hesabu kwa ujumla.Hufanya kwa kutumia akili yake hesabu nzito nzito tena kwa speed ya hali ya juu sana.Pia ana uwezo wa kuongea lugha saba bila shida.

11.GARRY TURNER
Je ngozi yako ina uwezo wa kujivuta kwa kiasi gani?Kutana na jamaa huyu ambae ngozi yake hujivuta kama mpira.Huivuta ngozi yake kwa namna mbali mbali.Hii inatokana ngozi yake kupungua 'Collagen'

12.NOORSYAIDAH
Ni mwanamke wa kiindonesia ambae anasema kuwa mwili wake una tabia ya kuota waya kwa muda usiopungua miaka ishirini sasa.
Waya hizo huwa kiasi cha sentimita 10 hadi 20.

13AL HERPIN
Kqa kawaida baada ya kukaa siku chache bila kulala kabisa mwili HUZIMIA.Lakini kwa mtu huyu AL,hajawahi kabisa kulala katika maisha yake na hivi sasa ana miaka 94.
Wanasayansi wanaamini kuwa inawezekana hali hiyo ilisababishwa na jeraha alilopata mama yake siku chache kabla ya kumzaa.

14.LIEW THOW LIN
Anajulikana kama MAGNETIC MAN,raia huyu wa Malaysia ana uwezo wa ajabu sana amabpo mwili wake una uwezo wa kuvuta vitu vya chuma.


Sunday, 20 March 2016

SIMULIZI YA KIMAPENZI YENYE MAFUNDISHO


HADITHI FUPI.
************
“NITAKUBEBA KILA ASUBUHI MKE WANGU MPAKA KIFO KITAKAPO TUTENGANISHA”.
*************
MTUNZI: ELIA MWAIPOPO & SHUFAA.
************
“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu.
Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu . Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini ?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike . Akatupa kijiko na akanikaripia , ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu . Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Husna. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Husna. Kwa kweli nilimdharau mke wangu !Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa , niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu .
Nilimuonea huruma kwa muda , rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Husna aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu , jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu .Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa miezi kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi .Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani . Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka . Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika . Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika . Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mtoto wetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu . Hili halikuwa tatizo kwangu , nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada , aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku ya harusi yetu . Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa . Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu .Nilimsimulia Husna kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu . Husna alicheka sana , aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Husna tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki . Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana . Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja . Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni , halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu . Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka . Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba . Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote . Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake . Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana . Nikagundua hakuwa binti tena . Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe ! Ndoa yetu imekula urembo wake . Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi . Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea . Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa . Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya . Sikumwambia Husna kuhusu jambo hili . Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi . Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi .Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi . Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa . Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana , nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi . Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake . Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake . Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu . Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho . Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani , sebuleni halafu mpaka mlangoni . Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo . Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka .Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja . Mtoto wetu alishakwenda shuleni . Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo . Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango . Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Husna alifungua mlango nikamwambia, ‘ Samahan husna, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu , halafu akagusa kichwa changu . Akaniuliza ‘Unaumwa ?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Husna, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu . Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu , mimi na mke wangu , si kwamba hatupendani . Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu , nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenga
nisha.’ Ikawa kama Husna alizinduka usingizini . Akanizaba kibao cha nguvu , akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia . Nikashuka ngazi na kuondoka zangu . Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu . Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi . Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu , tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani , nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani . Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Husna sikuwa na muda wa kukaa na kujadili maisha wala matatizo ya mke wangu .
Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mtoto wetu kama ningelazimisha talaka mapema . Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….................Mungu amuweke mahala pema peponi mke wangu . Nitamkumbuka daima .
MWISHO****
KUMBUKA
SHARE, COMMENT & LIKE

Friday, 18 March 2016

MASKINI MTOTO HUYU AZALIWA BILA PUA!!!!


Tukio hili la mtoto anaezaliwa bila kuwa na pua huyokea mara chache sana ambapo kati ya watoto milioni 197 basi humkumba mtoto mmoja.Je mtoto huyo anaishi vipi?

Mtoto huyo Eli,alizaliwa katika eneo la Alabama nchini Marekani mnamo tarehe 4 mwezi wa tatu.Mara baada ya madaktari kumkabidhi mtoto huyo mama,mara moja mama yake aitwae Brand MvGlathery aligundua kuwa mwanae amezaliwa bila kuwa na pua.Aliamua kumpeleka katika hospitali ya 'USA Children's and women's Hospital in mobile' iliyoko pale pale Alabama ili kuona wataalamu wanaoweza kumsaidia mwan
ae. Aliweza kupumua bila shida baada ya kutoka hospitalini pale.

Mama yake amekuwa karibu sana na madaktari kuhakikisha kuwa anapata maelezo sahihi ya namna ya kumtunza vema mtoto huyo.
Tukio kama hili liliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1931 na linajulikana kitaalamu kama *Congenital Arhinia*

Inaweza kuwa ni ngumu kuishi kwa hali hii kuelekea utu uzima lakini kuna watoto wameweza kukua wakiwa na hali hii hadi kuwa watu wazima.Mama wa mtoto huyo amekuwa karibu sana na wazazi wa watoto wengine waliozaliwa bila pua na kuweza kukua vema hadi ukubwani licha ya kupata changamoto ya mfumo wa upumuaji.Mama huyo anasema hii imemsaidia sana kuweza kupata taarifa muhimu pia ya namna ya kumlea mtoto wake.

Yuko sawa kwa hali aliyonayo.Pia kunabnjia mbafala ya kumfanyia upasuaji ili kumwekea umbo la pua yaani pua bandia kwa hiyo mama yake analitumainia hilo.Mama yake anasubiri aje aamue mqenyewe ukubwani kama anahitaji pua bandia ama la.
     
           "Hadi pale atakapohitaji pua bandia,sisi hatutafanya lolote lile,tutasubiri uamuzi wake pale atakapoweza kuwa na maamuzi yake mwenyewe"

Alimalizia mama wa mtoto huyo.


Kama umeoendezwa nayo waweza share
Karibu tena kwenye ukurasa huu.