Wednesday 30 March 2016

NI AJABU KWELI!!!JIONEE NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUZIBADILI HISIA ZA KISASI NA KUWA ZA KINDUGU

Pamoja na kuwa na uhasama mkubwa sana kati yao,Babu huyu raia wa afghanistan alikutwa akimpa mwanajeshi huyu wa marekani kikombe cha chai.Hii ni ishara ya UPENDO na kuthamini watu wengine pia.Dada mmoja ambae alikuwa na wenzie katika mashindano ya kukimbia mita 3200 aliamua kusimama na kumsaidia mwenzie aliekuwa ameumia ili kumaliza mbio.Japo walimaliza nafasi ya 14 na 15 lakini wote wawili walipewa tuzo maalumu ya heshima.Japo kulikuwa na vita kali sana inayoendelea,Mwanajeshi huyu muungwana aliamua kumchukua mbwa mmoja ambae alikuwa akiwafuatilia nyuma kwa umbali mrefu sana.Hatimae mwanajeshi huyu alimtoa mbwa huyo sehemu ya mateso na kumfikisha sehemu salama.Wakati wa maandamo yaliyotokea nchini Misri mwaka 2011 watu hawa hapa chini ni WAKRISTU waliokuwa wakiwalinda wenzao WAISLAMU waweze kufanya ibada vema.WAISLAMU pia walifanya vivyo hivyo kwa WAKRISTU.Ni dalili ya utu wema.Baada ya kutokea kwa kimbunga na upepo mkali katika jiji la New York nchini Marekani,sehemu kubwa ya jiji hilo iliharibika sana hasa ile ya nishati kama umeme na miundo mbinu mingine kama barabara.Katika picha wanaonekana watu wakitoa msaada wa kuchajisha simu kwa wale waliokosa huduma ya umeme.Daima tujifunze utu na kusaidia wengine pia.Share kwa wengine kama umeupenda UTU wao.Pia wasamehe na kuwajali adui zako pia.

No comments:

Post a Comment