Thursday 10 March 2016

CHRIS BROWN:NIMECHOKA KUABUDU MASHETANI





Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa amechoka kuoan shetani akiyaharibu maisha yake.Katika post aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa instagram hivi karibuni ameandika kuwa shetani anajaribu kuyaharibu maisha yake.Pia ameandika kuhusu kuwa na mawazo ya kujiua na kuisikia sauti ya MUNGU ikimsihi kwa mara ya kwanza.Haya ndo aliyoyaandika
     
   "Pale unapochoka shetani anapoyaharibu maisha yako na unapoiskia sauti ya MUNGU kwa mara ya kwanza.Hakuna ajuae nachokifanya siku baada ya siku.Mtu wa kawaida hawezi umiza kichwa au akili yake ila ni uoga tu.Wengi hawafahamu ufahamu na uzuri ni katika mabadiliko na kujifunza ila wale walio na muelekeo wa kishetani huyapata kwa muda mfupi mafanikio.
Roho yangu daima itakuwa yenye haki na safi.Unavyoniona kwa muonekano wa nje sivyo ila ndani nina mvulana mdogo anaehitaji msaada na mwongozo pia.Watu hunambia KUWA MWANAUME.Sawa ila haiwezi kuondoa maumivu unayoyapitia.Nahitaji kutoka katika njia hii na kujikita na muziki wangu.Ninapenda niweze kuwa Baba bora.Sina uvumilivu tena na vitu au kitu kitakachosababisha kujiharibia maisha yangu."



Je ni ushahadi wa wazi kuwa Chris Brown nae yuko katika vyama vya siri vya waabudu mashetani?

No comments:

Post a Comment