Wednesday 9 March 2016

MWANAMKE WA UINGEREZA AOLEWA NA MBWA NDOA YA KIFAHARI.

Mwanamke mmoja raia wa Uingereza Amanda Rodgers ameamua kuolewa na mvwa wake aitwae SHEBA baada ya kuachana na mumewe katika ndoa iliyodumu kwa miezi kadhaa.
Mwanamke huyo alifunga ndoa yake na mwanaume huyo miaka 20 iliyopita ndoa ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa halafu wakaachana.Amanda akaweka kiapo cha kutokupenda tena mwanaume na kwa muda wote huo akaamua kuwa na uhusiano na mbwa wake 'sheba'.
Amanda alisema kwamba ameamua kuolewa na mbwa huyo kwa kuwa mbwa huyo ametimiza vigezo vyote vya aina ya mpenzi anaemtaka.
     
               "Sheba amekuwa katika maisha yangu              kwa miaka kadhaa,amenifanya kuwa wa furaha na kuniliwaza ninapokuwa na huzuni."

Zaidi ya watu 200 walihudhuria sherehe hiyo ya harusi ya kushangaza iliyofanyika Split,Croatia.
Amanda alihakikisha kila kitu kinakwenda sana na harusi inakuwa ya kupendeza.Alisema

         "Niliota tangu mdogo kuwa na harusi iliyotimia na kuvaa mavazi bora ya harusi.Hakika hii imekuwa siku nzuri sana kwangu"

Amanda hajali watu wanasema nini juu yake.Anasema kuwa anajua kuwa ndoa hiyo haipo kisheria ila ilikuwa nzuri na kuonesha sheba ana umuhimu gani kwake.


No comments:

Post a Comment