Showing posts with label madhara. Show all posts
Showing posts with label madhara. Show all posts

Tuesday, 29 March 2016

JIONEE WATU WENYE UWEZO WA AJABU NA KUSHANGAZA


Je unafahamu kuwa watu wenye nguvu za ajabu kuliko uwezo halisi wa kibinadamu wapo?Ni kweli watu hao wapo na wengine wanaishi hadi sasa.Ni watu ambao wana vitu vya ajabu kama uwezo,nguvu na kuwa imara madhubuti.Wafuatao ni baadhi ya watu hao

1.WIM HOF
Huyu ana uwezo wa kukaa muda  mrefu sana eneo la baridi kali sana bila kupata madhara yoyote yale.Huyu ni mtu halisi anaweza kukaa muda mrefu sana eneo la baridi kali sana.Anazo tuzo 21 za Guinness ikiwemo ya kuoga kwenye maji ya barafu kwa muda mrefu.Huyu anaweza kukaa kilele cha mlima kilimanjaro kifua wazi kwa muda mrefu.

2.KELVIN RICHARDSON
Huyu ana uwezo mkubwa sana wa kuwaelewa wanyama.
Ana uwezo mkubwa sana wa kufanya urafiki hata na wanyama wakali zaidi duniani bila tabu yoyote.Ana uwezo wa kuwa na urafiki na chui,simba na fisi.Huwafanya marafiki na hata kulala nao pia.

3.CLAUDIO PINTO
Huyu anajulikana kama MACHO YA DARUBINI.Ana uwezo wa kuyatanua macho yake kipimo cha 7mm ambapo ni kiasi cha 95% ya mzunguko wa jicho lake.

4.HAROLD WILLIAMS
Anajulikana kama MWALIMU WA LUGHA.Huyu anasifika kwa kuwa na uwezo wa kujua lugha nyingi sana duniani.Je wewe una uwezo wa kujua lugha ngapi katika maisha yako yote?Huyu anafahamu lugha zaidi ya 58 ambazo anaziongea na kuandika bila shida yoyote ile.
Sio peke ake alie na kipaji hiki,pia wapo John Browning,Joseph Caspar na Doktar Carlos do Amaral Freire.

5.TIBETAN MONKS
Wana uwezo wa kuweka sawa JOTO la miili yao kwa kutumia akili au ufahamu wao.Wana uwezo qa kubadili joto la miili yao kwa kutumia akili yao tu.Wamewahi kurekodiwa wakibadili jotoridi lao kufikia kiasi cha nyuzi joto 8 za sentigredi.

6.RATHAKRISHNAN VELU
Anajulikana kuwa na meno ya ajabu yenye nguvu sana maarufu kama 'steel teeth'.Ana uwezo wa kuvuta treni ya mabehewa saba akitumia meno yake kuivuta kwa kutumia kamba ya chuma.Anajulikana pia kwa jina la KING TOOTH.

7.DANIEL BROWNING SMITH
Huyu anajulikana kama 'The rubber boy' ana uwezo wa kujipinda zaidi katika mikao mbali mbali.

8.STEPHEN WILTSHIRE
Ana uwezo mkubwa sana wa kukumbuka.Huyu ana uwezo wa kutazama kitu mara moja tu na kuweza kukichora kwa ufasaha kabisa.Ni maarafu sana kwa kuchora picha za miji mbali mbali kwa kuiangalia mara moja tu.Kama watu wengine hutizama mara kwa mara katika uchoraji huo,yeye hutizama mara moja tu na kuchora sehemu kubwa ya mji husika.

9.JESUS ACEVES
Huyu ni mtu mwenye nywele nyingi zaidi za usoni.Anapatikana katika familia ya kimexico yenye wanafamilia 24 ,huwa anazunguka duniani kuonesha watu muonekano wake huo.

10.DANIEL TAMMET
Ni mtaalamu sana wa mahesabu na hesabu kwa ujumla.Hufanya kwa kutumia akili yake hesabu nzito nzito tena kwa speed ya hali ya juu sana.Pia ana uwezo wa kuongea lugha saba bila shida.

11.GARRY TURNER
Je ngozi yako ina uwezo wa kujivuta kwa kiasi gani?Kutana na jamaa huyu ambae ngozi yake hujivuta kama mpira.Huivuta ngozi yake kwa namna mbali mbali.Hii inatokana ngozi yake kupungua 'Collagen'

12.NOORSYAIDAH
Ni mwanamke wa kiindonesia ambae anasema kuwa mwili wake una tabia ya kuota waya kwa muda usiopungua miaka ishirini sasa.
Waya hizo huwa kiasi cha sentimita 10 hadi 20.

13AL HERPIN
Kqa kawaida baada ya kukaa siku chache bila kulala kabisa mwili HUZIMIA.Lakini kwa mtu huyu AL,hajawahi kabisa kulala katika maisha yake na hivi sasa ana miaka 94.
Wanasayansi wanaamini kuwa inawezekana hali hiyo ilisababishwa na jeraha alilopata mama yake siku chache kabla ya kumzaa.

14.LIEW THOW LIN
Anajulikana kama MAGNETIC MAN,raia huyu wa Malaysia ana uwezo wa ajabu sana amabpo mwili wake una uwezo wa kuvuta vitu vya chuma.


Thursday, 24 March 2016

KUTANA NA DOGVINCI,MBWA MAARAFU KWA UCHORAJI


Sio tu binadamu wenye uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu.Hata wanyama wana uwezo wa kufanya mambo mengine tena katika kiwango kikubwa zaidi ya binadamu.

Mbwa anaeitwa Dagger amekuwa mchoraji maarufu sana baada ya kufundishwa na mlezi wake Yvonne.

       "Mara nyingi amekuwa akiniangalia sana wakati nachora hadi akapata hamu ya kujifunza.Baadae akaanza kunisumbua sana na nikamuuliza unataka kuchora?Akaanza kutingisha mkia kama ishara ya kukubali.Nikamwambia sawa"
Alisimulia Yvonne akihojiwa na gazeti la ABC 7New York.

Baada ya kutumia muda kumfundisha mbwa huyo,hivi sasa anaitwa DOGVINCI pale New York kutokana na uchoraji wake wa hali ya juu.

Michoro ya mbwa huyo inauzwa kati ya dola $20 hadi $200 za kimarekani kwa mchoro mmoaja.Faida kubwa inayopatikana inapelekwa kwenye organization ya "Canine Companions for Independence".
Ama kweli haya ni maajabu!!!!!Jionee picha zaidi


Wednesday, 23 March 2016

YAJUE MADHARA YA KUVAA NGUO PENDWA ZA KUBANA SANA MWILI!!!


Mbali na ukweli kwamba baadhi ya mitindo ya mavazi inasababisha adha kubwa kwa watumiaji, mitindo mingine husababisha atharimbaya kwa afya kwa watumiaji na jamii kwa ujumla.Miongoni mwa mitindo ya mavazi inayosababisha athari mbaya za kiafya ni ile ya mavazi yanayobana sana.

Tafiti kadhaa za kisayansi zinabainisha kuwa miongoni mwa nguo zinazoathiri afya ni nguo za ndani za wanaume zinazobana sana maarufu kama kama boksa pamoja na suruali za jeans zinazobana maarufu kama ‘skinny jeans’ ambazo mara nyingi huvaliwa na wanawake.Nguo zinazobana sana husababisha mishipa midogomidogo inayosafirisha damu kubanwa na kuathiri usambazaji wa damu kwenye baadhi ya maeneo ya mwili.Kutokana na hali ya kubana, nguo hizo husababisha uharibifu wa misuli na mishipa ya fahamu katika mapaja na miguu hasa kwa wanawake.

Mara nyingi madhara ya nguo hizi hujitokeza kama dalili ya miguu kufa ganzi au hisia za miguu kuwaka moto na ni mara chachewahusika kutambua kuwa dalili hizo chanzo chake ni mavazi.Katika ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa Juni mwaka 23, mwaka jana na Jarida la Neurology, Neurosurgery and Psychiatry, inaonyesha kuwa watafiti katika Hospitali ya Royal Adelaide nchini Australia walihusisha nguo za kubana sana za aina ya jeans na kutokea kwa tatizo la misuli lijulikanalo kitabibu kamacompartiment syndromeambalo alilipata mwanamke mmoja nchini humo.“Ugonjwa wa mwanamke huyu unaonyesha madhara mapya ya uvaaji wa jeans zinazobana.”  alisema

Dk Thomas Kimber, mmoja wa watafiti waliotoa ripoti hiyo alipokuwa akizungumza kuhusu madhara ya mavazi ya kubana.Mtaalamu wa mishipa ya fahamu na mwanachama wa chama cha Madaktari wa Mishipa ya Fahamu cha Marekani (AAM), Dk John England, anasema:

“Mishipa ya fahamu kwa baadhi ya watu, inaweza kukandamizwa kwa urahisi. Mshipa wafemoral cutaneousunaotoka kwenye nyonga na kuingia mapajani kwa ajili ya kuchukua hisia, unaweza kubanwa na kitu chochote kinachobana mapaja au eneo la kiuno.”

Hali ya kubanwa kwa mishipa ya fahamu kama itakuwa ya kujirudia rudia inaweza kusababisha madhara ya kudumu.Madhara ya nguo za kubanaKwa wanawake nguo zinazobana kupita kiasi zinaweza kusababisha damu kuganda ndani yamishipa, uvimbe wa mishipa ya damu kwenye miguu na magonjwa ya fangasi ya ngozi yanayoambatana na muwasho.Hii inaweza kutokea kwa sababu ya jasho linalozalisha kwa wingi katika nguo zinazobana na kufanya ngozi ikose hewa safi.Uvimbe wa mishipa ya damu miguuni maarufu kama vericose veins, ni moja ya matatizo yanayowapata mara kwa mara wanawake wajawazito na wale wanaotumia vidonge, vipandikizi na sindano za kupanga uzazi bila kufanya mazoezi ya mwili.

Tatizo jingine kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa mwaka 2004 katika toleo namba117(2) la Jarida la Ejog (Europian Journal of Obstetrics & Gynaecology and Reproductive Biology) ni ongezeko la kuzaliana kwa bakteriawaharibifu ambao wanasababisha mwanamke kutokwa na usaha katika sehemu za siri.Hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wanawake wanene na watu wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari.Kwa wanaume, mavazi haya yanaweza kuathiriutendaji wa figo pamoja na kibofu cha mkojo na kuchochea kutokea kwa maambukizi katika njia ya mfumo wa mkojo.Yanaweza pia kusababisha uvimbe wa mishipa ya korodani au makende na kuathiri ubora wa mbegu za kiume. Hali hii wakati mwingine huwani chanzo cha ugumba na upungufu wa nguvu za kiume kutokana na athari za maumbile ya kianatomi pamoja na athari za kisaikolojia.

Utafiti ulioongozwa na Dk F. Parazzini wa nchini Italy na kuchapishwa mwaka 1995 katika Jarida la International of andrology toleo namba 18(3), ulionyesha kuwa, uvaaji wa nguo zinazobana unaathiri uwezo wa wanaume kuzalisha mbegu za kutosha.Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake naUzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe anasema athari za mavazi hayayapo mengi na mbaya zaidi ni yale yanayogandamiza mfumo wa uzazi wa mwanaume. Anaonya kwamba watu wengi wanaovutiwa na mavazi hayo hasa vijana, wanapaswa kuwa makini kwa sababu tafiti zilizofanywa zimethibitisha watu kuathirika.

“Mwanaume ili kuhifadhi vizuri mbegu zake, anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” anasema Dk Massawe.

Kutokana na athari za muda mfupi na zile za muda mrefu za mavazi yanayobana sana mwili, mtaalamu huyo wa afya anaonya jamii haina budi kuzingatia afya na usalama kwanzakabla ya kufikiria urembo na kupendeza.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa urembo na utanashati bila afya njema ni sawa na kujificha katika kichaka cha karanga,” anaonya kwa usemi huo wa Kiswahili.

Karanga ni mmea unaoota kwa mfano wa kichaka lakini urefu wake hauzidi sentimita 20 hivyo hauwezikumsitiri mtu, ili ajifiche, asionekane.

Je, tabia hii yaweza kukoma?Ni vigumu kubadili mitindo ya mavazi ambayo inashabikiwa hasa ikizingatiwa kuwa athari zake si za wazi. Mtu anaweza kusema kuwa amevaa mavazi ya namna hiyo kwa muda mrefu lakini hajaona madhara. Lakini ukweli ni kwamba athari zake zinaweza zisionekane wazi lakini zikawa ni za polepole na ambazo zitasababisha madhara makubwa miaka ijayo.Suala la kubadili tabia ni la mtu binafsi na ni jambo ambalo litatokana na mhusika baada yakupima faida na madhara ya mavazi haya yanayopendwa zaidi.

Ni suala la mtu kujiuliza; nionekane mtu wa kisasa kwa wakati huu mbele za watu na baadaye niwe na matatizo ya kiafya au niachane na mambo ya kuiga ili niwe na afya njema maishani.Kuonekana nadhifu na mtanashati siyo lazimakuvaa mavazi yanayobana sana. Waweza kuvaa mavazi yanayoruhusu mwili kutoathirika na ukaonekana nadhifu.Tatizo hapa ni ile hali ya kuvaa mavazi yanayobana mwili na wengine ingawa wanajihisi vibaya huvumilia. Kumbuka kuwa na afya bora kwa sasa na siku za baadaye za maisha yako ni jambo muhimu katika kukufanya uishi miaka mingi duniani.