Friday 24 June 2016

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU....

Wananchi wa Uingereza wameupitisha mswada wa kujitoa umoja wa ulaya hatua iliyopelekea WAZIRI MKUU kujiuzulu.

Hii ndo inaitwa UKOMAVU WA DEMOKRASIA ambao unapaswa kuigwa na mataifa ya kiafrika ambayo kuna ukandamizahi mkubwa wa demokrasia

Wednesday 8 June 2016

BIONIC MAN-Roboti aliekuwa na hisia na kutenda kama mwanadamu.

Bionic man ni roboti wa kwanza duniani ambaye ametengenezwa akiwa na uwezo wa kuongea,kutembea na kupumua.Ingawa si mwanadamu lakini pia roboti huyu ana moyo wa bandia
Wataalamu wa mambo ya robot Rich Walker na Mathew Godden wa kampuni ya shadow robot ndio walioifanya kazi hii ya kumtengeneza robot huyu aitwae bionic man.
"Kazi yetu ilikua kukusanya sehemu mbali mbali za mwili ikiwa ni pamoja na organ za bandia,miguu,macho ,kichwa kwa muda wa wiki 6 na kuvitumia kutengeneza bionic man"walker alieleza alipokua akihojiwa na livescience
Anasema kazi hiyo haikua rahisi kwani hawakua na binadamu bali walitengeneza kitu ambacho kitafanana na mwanadamu.

MAANA YA FUNGA(SAUMU) NA BARAKA ZAKE


Maana ya funga (Saum)
MAANA ya kufunga (saum) ni kujizuilia. Neno Saumu kwa maana ya kujizuilia linaweza kutumika katika kujizuia kufanya jambo lolote la kawaida mtu alilozoea kulifanya. Katika Qur'an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa Nabii Issa (a.s.) alijizuia (alifunga) ili asiseme na mtu neno lolote juu ya mtoto wake.
"...Na kama ukimwona mtu yoyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya kufunga, kwa hiyo leo sitasema na mtu". (19:26).
Katika Uislamu kufunga (saumu) ni kujizuilia kula, kunywa, kuvuta sigara, kuingiza kitu chochote katika matundu mengine mawili kama vile pua na masikio, kujizuia na kujamii, kujitoa manii kwa makusudi au kwa matamanio na kujizuia kujitapisha kwa ajili ya Allah (s.w.), kwa kipindi cha kati ya Al-fajri ya kweli mpaka kuingia magharibi. Hii ndio maana ya nje ya Saumu katika Uislamu.
Kufunga katika Uislamu kuna maana ya ndani zaidi, ambayo kama haikufikiwa, kuzuilia kufanya vitendo hivyo vilivyoelezwa hakutakuwa na maana yoyote kwa mfungaji.
Kufunga kwa maana ya ndani ni pamoja kujizuilia kutenda maovu yote yaliyokatazwa na Allah (s.w). Ili saumu ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu- pamoja na fikra na hisia zake na matendo aliyokataza Allah (s.w.).
Funga ya macho ni kujizuilia na kuangalia aliyoyakataza Allah (s.w.); Funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w.) kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana na kadhalika, funga ya masikio ni kujizuia kufanya yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w.); funga ya miguu ni kujizuilia na kuendea yale yote aliyoyakataza Allah (s.w.) funga ya fikra na hisia ni kujizuia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w.). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w.) anasema katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuwa anaacha chakula chake na kinywaji chake (yaani Allah (s.w.) hana haja na funga yake. (Bukhari).
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Ni wangapi wanaofunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu ni wangapi wanao swali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).
Hadithi hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuia na mambo maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.
Umuhimu wa funga katika Uislamu
Funga ya Ramadhani ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na ni faradhi kwa Waislamu kama inavyobainika katika aya ifuatayo:
Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga (saumu) kama walivyofaradhishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. (2:183)
Kama ilivyo katika nguzo nyingine za Uislamu, mtu atakapoivunja makusudi nguzo hii hatabakia kuwa Muislamu japo atajiita Muislamu na watu wakaendelea kumwita hivyo. Katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Abbas, Mtume (s.a.w.) amesema:
Kuna viungo vitatu vinavyomuunganisha Muislamu na dini ya Uislamu na yeyote yule atakayevunja kiungo kimoja katika hivi atakuwa amekana Uislamu na kuuawa kwani ni halali. Viungo hivi ni: Kushuhudia kuwa hapana Mola ila Allah, Kusimamisha Swala tano na kufunga mwezi wa Ramadhani.
Katika Hadithi nyingine Abu-Hurairah (r.a.) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w.) amesema:
Yeyote yule atakaye acha makusudi kufunga siku moja ya mwezi wa Ramadhani, hawezi kuifidia siku hiyo hata akifunga kila siku katika umri wake wote (uliobakia). (Abu-Daud)
Funga ni ibada maalum iliyo muhimu sana katika kumuandaa mja kuwa mcha Mungu kwa kule kukataa kwake matamanio ya kimwili. Hivyo Allah (s.w.) kwa ukaribu wake ameahidi malipo makubwa kwa wenye kutekeleza ibada hii ili iwe motisha kwao ya kuwawezesha kutekeleza ibada hii kwa hima kubwa na kwa ukamilifu unaotakikana kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Mwenye kufunga Ramadhani akiwa na imani na akawa na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allah dhambi zake zote zilizopita husamehewa, Na mwenye kusimama kwa swala (tarawehe) katika mwezi wa Ramadhani akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo (kutoka kwa Allah), dhambi zake zote zilizopita zitasamehewa. Na yule atakayesimama (kwa swala) katika usiku uliobarikiwa (Lailatul-Qadri) akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allah (s.w.) dhambi zake zote zilizotangulia zitasamehewa. (Bukhari na Muslim).
Pia Abu-Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Kila amali njema anayoifanya mwanaadamu italipwa mara kumi (Al-Qur'an 6:160) mpaka kufikia mara mia saba (Al-Qur'an 2:261). Allah (s.w.) amesema:
Ila kufunga kwa sababu funga ni kwa ajili Yangu, na ni mimi mwenyewe nitakayeilipa. Mwenye kufunga anakata matamanio yake ya kimwili na anaacha chakula kwa ajili yangu. Kwa mwenye kufunga kuna furaha mbili, furaha moja anaipata wakati wa kufuturu na nyingine wakati atakapokutana na Mola wake. Na hakika harufu ya mdomo wa mwenye kufunga ni bora mbele ya Allah (s.w.) kuliko harufu ya miski. Na funga ni ngao. Kwa hiyo atakayefunga miongoni mwenu hataongea maneno ya upuuzi wala hatagombana. Kama itatokea achokozwe na yeyote, au mtu atakakupigana naye, na aseme: Nimefunga. (Bukhari na Muslim).
Vile vile Mtume (s.a.w.) katika kusisitiza umuhimu wa funga ya Ramadhani alitoa khutuba mwishoni mwa mwezi wa Shaaban kama ilivyonukuliwa katika hadithi ifuatayo:
Salman al-Farisy ameeleza: Mtume (s.a.w.) alituwaidh mwisho mwa siku ya Shaabani akasema: Enyi watu! Hakika umekujieni mwezi mtukufu, mwezi uliobarikiwa, mwezi ambao ndani yake kuna usiku uliobora zaidi kuliko miezi elfu moja. Allah (s.w.) amefaradhisha kufunga katika mwezi huu na kusimama (kwa swala ya tarawehe) katika mausiku yake ni sunnah. Atakayetekeleza kitendo kizuri kisicho faradhi atapata ujira wa mtu aliyetekeleza kitendo cha faradhi katika miezi mingine, na yule atakayetekeleza kitendo cha faradhi atapata ujira wa mara 70 wa ujira wa kitendo hicho katika miezi mingine. Na ni mwezi wa subira, na ilivyo, subira malipo yake ni pepo. Na ni mwezi wa kuhurumiana na mwezi ambao mahitaji (mapato) ya muumini huongezwa. Atakayetoa futari kwa mwenye kufunga katika mwezi huu kuna kusamehewa dhambi zake na kuwekwa huru na moto, na atapata malipo sawa na ya yule aliyefunga bila ya yeye kupunguziwa chochote. Tukauliza: Ee Mtume wa Allah! Hakuna yeyote kati yetu mwenye uwezo wa kumfuturisha mtu aliyefunga. Alijibu Mtume: Allah atamlipa yule mwenye kumfuturisha aliyefunga kwa funda la maziwa, au tende moja au funda la maji. Na yule anayekidhi haja ya mtu Allah atamnywesha kutokana na Birika (Kawthar) langu na hatakuwa na kiu mpaka atakapoingia peponi.
Na (Ramadhani) ni mwezi ambao mwanzo wake kuna kurehemewa, katikati yake kuna kusamehewa na mwisho wake kuna kuachwa huru na moto. Na yule atakayempunguzia kazi mtumwa (mfungwa vita) wake, Allah atamsamehe, na atamuacha huru na moto.
Historia ya kufunga
Funga, kama ilivyo katika ibada nyingine kama tulivyoona katika kusimamisha swala na kutoa zakat, imetekelezwa na Mitume wote pamoja na umma zao. Allah (s.w.) ametukumbusha hili wakati alipotupa amri ya kutekeleza ibada hii maalum, kama tunavyorejea katika Qur'an:
Enyi mlioamini! Mmeandikiwa (mmefaradhishiwa) kufunga kama walivyofaridhishiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. (2:183)
Katika historia tunajifunza kuwa, kila Mtume alipoondoka, baada ya kipindi kupita, watu waliacha mafundisho yake na kuingia katika ushirikina. Lakini bado tunakuta funga, japo si katika madhumuni na asili yake iliyoachwa na Mitume wa Allah (s.w.), imebakia katika jamii za kishirikina kwa kipindi chote cha historia. Hebu tuangalie mifano michache ya dini za ushirikina ambapo funga, kwa maana ya kushinda na njaa na kiu, imekuwa miongoni mwa ibada muhimu za dini hizo.
Jamii ya Nabii Ibrahim
Nabii Ibrahim (a.s.) aliinuliwa katika jamii ya washirikina. Walikuwa wakiabudu jua, mwezi, nyota na masanamu chungu nzima waliyoyachonga wenyewe. Pamoja na ushirikina wao huo walikuwa wakifunga siku 30 mfululizo katika kila mwaka kwa heshima ya mwezi
Wahindu (Hinduism)
Dini ya Kihindu ni miongoni mwa dini za kishirikina katika bara la India. Katika dini hii funga, ni kitendo kilichosisitizwa sana japo si lazima, katika siku maalum kama vile kupatwa kwa jua, kumbumbuku ya kuzaliwa mwanzilishi wa dini yao na kadhalika. Funga kwao ni kujizulia na kula na kunywa kuanzia alfajiri mpaka saa tisa mchana.
Mayahudi (Judaism)
Dini ya Kiyahudi ni dini waliyoibuni Mayahudi baada ya Nabii Musa (a.s.) ambapo walimfanya Uzairi mwana wa Mungu. Pamoja na hivyo wachaji wa Kiyahudi walikuwa wakifunga Alhamisi na Jumatatu kama kumbukumbu ya kwenda na kurudi kwa Nabii Musa (a.s.) katika safari yake ya Sinai kwenda kuchukua Taurati. Kutokana na kumbukumbu ya historia, Nabii Musa alikwenda kwenye mlima Sinai siku ya Alhamisi na kurejea siku ya Jumatatu baada ya siku arobaini kupita.
Pia Mayahudi hufunga kwa saa 24 katika kila mwezi 10 Muharamu, kwa kumbukumbu ya siku Wanaisraili ( Mayahudi) walipookolewa na Allah (s.w) kutokana na udhalimu wa Firaun. Siku hii ambayo hata Waislamu wamesuniwa kufunga huitwa siku ya Ashuurah.
Pamoja na funga hizi, pia Mayahudi wana tabia ya kufunga mara kwa mara kulingana na haja. Kwa mfano mtu anaweza kuamua kufunga siku kadhaa kama kumbukumbu ya matukio fulani katika maisha yake, au anaweza kufunga funga kama kitubio cha madhambi yake, au anaweza kufunga wakati akiwa na matatizo ili kupata huruma ya Mungu.
Ukiacha siku ya Ashuura ambapo funga huchukua saa 24, funga za Mayahudi huanza alfajiri na huishia pale inapojitokeza nyota ya kwanza usiku.
Wakristo
Dini ya Ukristo imebuniwa baada ya Nabii Issa (a.s.). Katika dini hii Nabii Issa (a.s.) amefanywa mwana wa Allah (s.w.) na kwamba yeye ndiye mkombozi wa Wakristo. Pamoja na hivyo, Wakristo wanakiri kuwa kufunga ni kitendo cha uchaji - katika dini yao. Wakristo wa mwanzo walikuwa wakifunga siku 40 mfululizo kasoro siku za Jumapili kama kumbukumbu ya siku zile alizofunga Yesu (Nabii Issa a.s.) kama inavyobainishwa katika Biblia.
Historia inatuonyesha vile vile kuwa funga hizi za Washirikina zimetofautiana sana katika mfumo na funga ya Kiislamu aliyoiamrisha Allah (s.w.). Ambapo Waislamu wakifunga hujizuia kula, kunywa na kujamii mchana kutwa kuanzia alfajiri mpaka kuchwa kwa jua, funga za washirikina zilichukua mifumo mbalimbali. Wengine walijizuilia kula na kunywa tu lakini waliendelea kujamii, wengine walijizulia kunywa na kula kuanzia alfajiri mpaka saa 9 alasiri, wengine walijizulia kula aina fulani tu ya chakula kama vile nyama, wengine walijizulia kwa kunywa tu maji yaliyochanganywa na chumvi au maji ya ndimu, na kadhalika.

Friday 3 June 2016

BONDIA MAARUFU MUHAMMAD ALI AFARIKI DUNIA.



Aliekuwa bondia maarufu duniani,Muhammad Ali amefariki kwa mujibu wa msemaji wa familia yao.Ali amefariki akiwa na umri wa miaka 74.

Bingwa huyo wa mara tatu wa dunia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa tangu mwaka 1984 miaka mitatu baada ya kustaafu mchezo wa masumbwi.

Siku moja kabla ya kukubwa na umauti,Ali,alipelekwa hospitali ya Phoenix,Arizona akiwa na matatizo ya upumuaji.Tatizo hili lilipelekea matatizo ya neva za fahamu yaliyoathiri pia mfumo wake mzima wa upumuaji.

Mazishi yake yatafanyika katika mji aliozaliwa wa Louisville,Kentucky.
 
         "Familia ya Ali inapenda sana kuwashukuru sana kwa mawazo,sala na sapoti mliotuonyesha kwa kipindi chote cha kumuuguza Ali"Alimalizia msemaji wa familia.

Rest in peace MUHAMMAD ALI,THE BEAST


Asante kwa kutembelea ukurasa huu.

Share kadili uwezavyo.

Wednesday 18 May 2016

KIJANA WA MIAKA 31 AZAMIA KATIKA PENZI LA BIBI WA MIAKA 91.


Kila mmoja anaamini kuwa umri ni namba tu katika mapenzi.Kama unampenda mtu umri wake hauna nafasi katika mapenzi yenu.Je ni kweli imani hii ina ukweli ndani yake katika kila penzi??

Kutana na Kyle Jones 31,ambaye yuko katika penzi la dhati na bibi kizee mwenye umri wa miaka 91 anaemzidi takribani miaka 60 kijana huyo.Unaweza kusema Kyle yuko katika mapenzi na mtu ambae anapaswa kumwita BIBI.

Kyle anasema anampenda sana MPENZI BIBI huyo ambae tunaweza sema SUGAR BIBI kwa lugha ya vijana wa town.

SHARE NA WENZIO WAPATE HABARI HII.

@viroshare

Wednesday 11 May 2016

IJUE NYOTA YAKO NA TABIA ZAKE


Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.
Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.
Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.
Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu. Hii si haba,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa.
[Soma pia: Madhara ya Mwezi Katika Hisia na Tabia za Binadamu:Kuna Ukweli? , Nyota na Kazi Zenye Mafanikio ]
Tabia Za Watu Na Alama Za Nyota
Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.
Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.
Alama hizi ni kama ifuatavyo:

1. Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20
2. Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19
3. Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21
4. Mapacha :(Gemini ): Mei 22 – Juni 20
5. Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22
6. Simba (Leo): Julai 23 – Agosti 22
7. Mashuke (Virgo):Agosti 23 – Sept 22
8. Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22
9. Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21
10. Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21
11. Mbuzi (Capricorn):Des 22 – Jan 19
12. Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18

Makundi Ya Alama Za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama:
Moto: Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
Maji: Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
Hewa: Imara na yenye kukuza au kuendeleza
Udongo: Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha
Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.

Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
Moto : Kondoo, Simba,Mshale
Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi

ZIFUATAZO NI NYOTA MBALI MBALI NA TABIA ZAKE







SHARE KADRI UWEZAVYO NDUGU. .ASANTE KARIBU TENA KWA HABARI ZA KIPEKEEE

Wednesday 4 May 2016

TANZANIA YAONGOZA KWA UKUAJI WA UCHUMI EAC

Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.
Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .
Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.
IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.
Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.
Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
1. Ivory Coast 8.5%
2. Tanzania 6.9%
3. Senegal 6.6%
4. Kenya 6%
5. Zambia 3.4%
6. Nigeria 2.3%
7. Afrika Kusini 0.6%

Source:bbc