Tuesday 26 April 2016

UNYAMA WA KUTISHA,MFANYAKAZI WA NDANI AUNGUZWA NA MAJI YA MOTO SEHEMU ZA SIRI!!!

Jaman mume afumaniwa na house girl mke akawamagia maji ya moto, ila mke hakufanya feya kw house girl cz anaonyesh ni mdogo huyo mam hasira angemaliza kw mume wake sio kw house girl hana makosa hako kanaonyesha ni kadogo San unawez kukuta alimbaka angesubir amuuliz maswal kwanz thn amrudishe kwao...

Huu ni unyama wa kutisha sana haijalishi ni kosa gani wahusika wamefanya.


UTU KWANZA NDOA BAADAE.

Sunday 24 April 2016

MAMBO 10 YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA MCHUMBA AU MPENZI MPYA❤❤


Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.
Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.
Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.
Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.
Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.
Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.
Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ramla aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.
Na leo my best friend na mdau wangu mkubwa wa Blog hii  Rayha ametaka kujua vigezo gani vya kuzingatia ili kumpata mume/mpenzi borana mwenye mapenzi ya kweli na ya dhati , hii ameiandika kwenye ukurasa wake wa facebook.
Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.
Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.
Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.
Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.
Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.
Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.
Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.
Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.
Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.
Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.

Saturday 16 April 2016

ROBOTI LENYE HISIA ZA KIBINADAMU LATENGENEZWA CHINA!!!😂


Je unaweza tambua roboti kati ya hawa watu kwa hizi picha ? Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya China katika mji mkuu wa Hefei, mashariki mwa China kimezindua roboti kwa jina "Jiajia" ambayo ina uwezo wa mwingiliano na binadamu.

Jiajia ni huyo mwenye mwanamke mwenye nguo nyekundu, anaweza kila kitu ambacho mwanamke anaweza kasoro kubeba mimba tu, lakini hisia za kupenda na kuchukia, hisia za kulala na mwanaume na mengi kama hayo.
Roboti hizo zinauwezo wa kutongoza au kutongozeka, zinaweza kukataa au kukubali inategemea na uwezo wako wa kushawishi.

Bado bei yake haijapangwa, na yapo yanayotengenezwa maalum kwaajili ya Afrika, je yakija Tanzania utanunua?? yakiume pia yatatengenezwa kwaajili ya kazi mbalimbali kama kulima nk.
Watu watabisha lakini mbona wanakula mayai kizungu, kuku za kizungu, sasa kuna ubaya gani mkila na nyapu/zakari za kichina? Au wachina hamuwaamini?

JAMANI MPENZI WANGU

NILIKUWA NA MPENZI MTUNZI:
 George Iron Mosenya SIMU: 0655 727325

Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..Nilij isikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale. Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule, nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine. Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili atanitangazaje kwa marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidh uru lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotak a kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria yake, kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale nilipokuwa. Sikuwa nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafia wasamalia wema, binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa zimenitoka na niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu. Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu ya kustaajabisha niliyokutana nayo. “Mpenzi Christopher mwanaume wa maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi wangu …nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu, nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE MTUMWA!!!!

 SHARE KWA WENGINE MWISHO!

Monday 11 April 2016

MADUKA ZAIDI YA 150 YAUNGUA MOTO!!!


Moto mkubwa umezuka na kuteketeza vibanda vya madukazaidi ya 150 katika mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoawa Kagera magharibi mwa Tanzania. Moto huo ambao ulianza Jumatatu majira ya sa 2:00 usiku umeteketeza mali na bidhaa za aina mbalimbali kama mchele, sukari, nguo, simu, pamoja na bidhaa zingine.Gloria Kilio ambaye alikuwa akiuza vyakula vya nafaka, amesema stoo zake zote tatu (3) za nafaka zimeungua, “Stoo zilikuwa na magunia ya unga, mchele na sukari lakini vyote vimeteketea,” amesema Gloria huku akilia. Anasema wakati moto unatokea alikuwa tayari amekwisha kwenda nyumbani na kuwaacha wafanyakazi wake wakimalizia kufunga vibanda.Wafanyabiashara wengi wanasema walikuwa na mikopo nawengi wao hawana bima ya mali zao. Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao: “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta,: anasema Jonas na kuongeza, “kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.” Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika benki.Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wavifaa vya kuzima moto. Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta maduka mengi yamekwishateketea.Diwani wa kata ya Kanoni wilaya karagwe Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewastua na ni tukio la kwanza la moto kuunguza soko wilayani humo. Anasema tatizo la ukosefu wa gari la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha. “Mara nyingi katika bajeti yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema maombi yao yako serikali kuu.Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinwiro amesema kuwa Serikali ya wilaya yake itapata gari la zima moto hivi karibuni, “Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza kuwa, “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”Hata hivyo baadhi ya wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya kwa sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi ili kuchangia huduma za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa nini hawapati elimu ya kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la dharura.Mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna Mamalishe mwenyekibanda sokoni hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika nguo zilizokuwa katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.

Friday 8 April 2016

HUWEZI AMINI!!!MBWA ANUNULIWA VIATU NA VIFAA VINGINE VYA KISASA😂😂😂


MBWA mwenye umri wa miaka saba anayeitwa Scooby ni miongoni mwa mbwa 35 maarufu wanaotumiwa na Jeshi la Ulinzi la Uingereza amenunuliwa vifaa malum vya kumkinga hasa awapo kazini.

Scoobyamenunuliwa miwani maalum ambayo itamsaidia kuzia vumbi kuingia machoni, viatu maalum kuzui miba na vitu vingine vinavoweza kumletea madhara awapo kazini pamoja headphone maalum kwa ajiri ya kunasa sauti mbalimbali zikiwemo za wahalifu na waongozaji wake.

Scooby ni miongoni mwa mbwa wakongwe kwenye kambi ya Jeshi ya Jeshi kikosi maalum cha mbwa (105 Military Working Dog Squadron). Amefanya kazi kwa miaka mitano tangu 2012 kwenye mapigano ya Afghanistan. Kazi yake kubwa ni ukaguzi wa mizigo, vyombo vya moto na kunusa ili kutambua kama kwenye kuna madawa ya kulevya.

Vifaa hivyo vitamsaidia wakati wa mafunzo maalum ya miezi mitatu nchini humo. “Mbwa huyo hang’ati hovyo. Amefundishwa vizuri na amezoea mazingira hasa ya kazi.” Alisema Steve Hood ambaye ni mkufunzi wa mbwa